MEYA WA JIJI LA DAR ES SALAAM ISAYA MWITA ZIARANI NCHINI IRAN KWA SIKU 10

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam ja...



Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam jana jioni tayari kwa safari kuelekea Nchini Iran kwa ziara ya kikazi ya siku kumi. (PICHA ZOTE NA ELISA SHUNDA)

 

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akiwasiliana na baadhi ya jamaa zake kabla ya kuondoka uwanjani hapo.


Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akiaga wakati akielekea ndani ya uwanja tayari kwa safari kuelekea Nchini Iran.

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akiwa katika utaratibu wa kuingia ndani ili aweze kukaguliwa kama abiria wengine wa kawaida tayari kwa safari kuelekea nchini Iran.


Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akipunga mkono kuaga wananchi wake wa jiji lake katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam jana jioni tayari kwa safari kuelekea Nchini Iran kwa ziara ya kikazi ya siku kumi (10), akiwa nchini humo atakutana na Rais wa Iran, Hassan Rouhani, Mwenyeji wake, Meya wa Jiji la Teheran, Muhammed Bakir Galbaf na kushuhudia kampeni za uchaguzi mkuu zinazoendelea nchini humo.

NA CHRISTINA MWAGALA, OMJ

Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita ,ameondoka Nchini jana kuelekea Iran kwa mualiko wa ziara ya kikazi ya siku 10 ikiwemo na mkutano wa siku mbili utakaofanyika katika mji wa Bashar.

Aidha Meya atapata nafasi ya kuzungumza na rais wa Jamhuri ya Kiislamu wa Iran Hassan Rouhani kabla ya kufanyika kwa mkutano wa siku mbili katika jiji la Bashar utakao husisha majadiliano mbalimbali kuhusu majiji.

Katika mkutano huo ambao utahusisha majadiliano mbalimbali kuhusu majiji, ambapo baada ya mkutano huo ataelekea mjini Teherani kwa mualiko maalumu wa Meya wa jiji hilo Muhammed Bakir Galbaf ambapo pamoja na mambo mengine watajadiliana fursa za kibiashara katika majiji hayo mawilI.

Aidha katika mazungumzo hayo, watajadiliana pia namna ya kutatua changamoto zilizopo kwenye majiji na namna ambavyo wanaweza kuyatatua.

“ Iran na Tanzania ni nchi marafiki kwa kipindi kirefu kwahiyo utaona kwamba mambo mengi wamekuwa wakishirikiana na sisi, kwahiyo ni fursa pia kwa majiji haya mawili kubadilishana uwezo wa kuendeleza jiji letu, nimechaguliwa na wananchi na wao wanataka maendeleo “ alisema Meya Isaya.

Aliongeza kwamba akiwa nchini humo atapata fursa ya kushuhudia kampeni za uchaguzi mkuu ambapo miongoni mwa wagombea wa nafasi ya urais Meya wa jiji la Teheran ni mmoja wapo.

“ Kushudia kwangu kampeni sio kwamba nataka kugombea nafasi ya uras hapa nchini , hapana ila ni moja ya kujifunza namna ambavyo wenzetu wanafanya kampeni zao” alifafanua.

Hata hivyo Meya aliwasi wakazi wa jiji la Dar es Salaam hususani wanaoishi mabondeni kuchukua tahadhari kwani bado mvua zinaendelea kunyesha na hivyo kujikinga na mafuriko.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MEYA WA JIJI LA DAR ES SALAAM ISAYA MWITA ZIARANI NCHINI IRAN KWA SIKU 10
MEYA WA JIJI LA DAR ES SALAAM ISAYA MWITA ZIARANI NCHINI IRAN KWA SIKU 10
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhbRrUPBMpCQllUqaham_Qk_IHJJj0RzEklIMT973NQpWwNe26dKogLXk4XVcKBxhHKMxvQYUSSTzTESjzZJ1PZL6ZVgUXv8lgVr_z3vNAPqwz9_wDMIjdtZBkX0JiLdRYdjAIhsPL70sI/s640/Q-6.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhbRrUPBMpCQllUqaham_Qk_IHJJj0RzEklIMT973NQpWwNe26dKogLXk4XVcKBxhHKMxvQYUSSTzTESjzZJ1PZL6ZVgUXv8lgVr_z3vNAPqwz9_wDMIjdtZBkX0JiLdRYdjAIhsPL70sI/s72-c/Q-6.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/meya-wa-jiji-la-dar-es-salaam-isaya.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/meya-wa-jiji-la-dar-es-salaam-isaya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy