MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA AMUAGIZA KAMISHNA MKUU WA TRA KUKUTANA NA WAFANYABIASHARA MARA KWA MARA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amemwagiza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charl...

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amemwagiza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere ahakikishe anaweka utaratibu wa kukutana na wafanyabiashara mara kwa mara kama njia ya kujadili na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara hao.
 
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere kuhusu namna bora ya kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara nchini kama hatua ya kuongeza kasi ya ukusanyaji wa kodi wa kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

Makamu wa Rais ameonyesha kusikitishwa na baadhi ya Maafisa wa TRA kuwanyanyasa wafanyabiashara na wengine kuwabambikizia kodi kubwa hali ambayo inazua malalamiko mengi kutoka kwa wafanyabiashara hao jambo ambalo amesema ni muhimu likatafutiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo.

Amesisitiza kuwa ni muhimu kama TRA itafanya mabadiliko yeyote ya ulipaji wa kodi ikawafahamisha wafanyabiashara hao mapema ili kuondoa usumbufu mkubwa unaoweza kutokea katika ulipaji wa kodi pindi wanapoagiza bidhaa mbalimbali kutoka nje ya nchi.

Makamu wa Rais amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha ulipaji wa kodi kwa ajili ya maendeleo ya Taifa unafanyika kwa kuzingatia kanuni, sheria na taratibu na sio kuwakandamiza Watanzania kwa kuwalipiza kodi mara mbili jambo ambalo amesema halifai hata kidogo.

Makamu wa Rais amemtaka Kamishna wa TRA kukomesha mara Moja tabia ya baadhi ya Maafisa wa mamlaka hiyo kutoa lugha chafu na kuudhi kwa wafanyabiashara bali watumie lugha nzuri ili kuhamasisha wafanyabiashara kulipa kodi kwa hiyari bila kulazimishwa na mtu.

Makamu wa Rais pia ameipongeza TRA kwa kazi kubwa inayoifanya katika ukusanyaji wa mapato na amewapa moyo wa kuongeza bidii katika ukusanyaji wa kodi hizo ambazo Serikali inatumia katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali nchini.
 
Kwa upande wake, Kamishna Mkuu wa TRA nchini Charles Kichere amemuahidi Makamu wa Rais kuwa atafanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha malalamiko mbalimbali yanayotolewa na Wafanyabiashara yanapata ufumbuzi haraka iwezekanavyo.

Kamishna Kichere amesisitiza kuwa kwa baadhi ya maafisa wa Mamlaka hiyo wanaokiuka maadili ya kazi ataendelea kuwachukulia hatua stahiki ili kurejesha nidhamu katika utendaji wa kazi na ukusanyaji wa mapato. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) Bw. Charles Kichere (kushoto) aliyemtembelea leo ofisini kwake, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Kamishna Mkuu wa TRA Bw. Charles Kichere (kushoto)ambaye aliongozana na Mkurugenzi wa Elimu ya Mlipa Kodi TRA Bw. Richard Kayombo (kushoto), Ikulu jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Afisa Mahusiano Mwandamizi wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Tanzania, Mariamu Mwayela mara baada ya kumaliza mazungumzo yake na Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo, Charles Kichere. Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere kuhusu namna bora ya kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara nchini kama hatua ya kuongeza kasi ya ukusanyaji wa kodi wa kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

Makamu wa Rais ameonyesha kusikitishwa na baadhi ya Maafisa wa TRA kuwanyanyasa wafanyabiashara na wengine kuwabambikizia kodi kubwa hali ambayo inazua malalamiko mengi kutoka kwa wafanyabiashara hao jambo ambalo amesema ni muhimu likatafutiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo.

Amesisitiza kuwa ni muhimu kama TRA itafanya mabadiliko yeyote ya ulipaji wa kodi ikawafahamisha wafanyabiashara hao mapema ili kuondoa usumbufu mkubwa unaoweza kutokea katika ulipaji wa kodi pindi wanapoagiza bidhaa mbalimbali kutoka nje ya nchi.

Makamu wa Rais amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha ulipaji wa kodi kwa ajili ya maendeleo ya Taifa unafanyika kwa kuzingatia kanuni, sheria na taratibu na sio kuwakandamiza Watanzania kwa kuwalipiza kodi mara Mbili jambo ambalo amesema halifai hata kidogo.

Makamu wa Rais amemtaka Kamishna wa TRA kukomesha mara Moja tabia ya baadhi ya Maafisa wa mamlaka hiyo kutoa lugha chafu na kuudhi kwa wafanyabiashara bali watumie lugha nzuri ili kuhamasisha wafanyabiashara kulipa kodi kwa hiyari bila kulazimishwa na mtu.

Makamu wa Rais pia ameipongeza TRA kwa kazi kubwa inayoifanya katika ukusanyaji wa mapato na amewapa moyo wa kuongeza bidii katika ukusanyaji wa kodi hizo ambazo Serikali inatumia katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali nchini.

Kwa upande wake, Kamishna Mkuu wa TRA nchini Charles Kichere amemuahidi Makamu wa Rais kuwa atafanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha malalamiko mbalimbali yanayotolewa na Wafanyabiashara yanapata ufumbuzi haraka iwezekanavyo.

Kamishna Kichere amesisitiza kuwa kwa baadhi ya maafisa wa Mamlaka hiyo wanaokiuka maadili ya kazi ataendelea kuwachukulia hatua stahiki ili kurejesha nidhamu katika utendaji wa kazi na ukusanyaji wa mapato.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akizungumza na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere,alipokutana nae leo Ikulu jijini Dar, kuhusu namna bora ya kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara nchini kama hatua ya kuongeza kasi ya ukusanyaji wa kodi wa kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA AMUAGIZA KAMISHNA MKUU WA TRA KUKUTANA NA WAFANYABIASHARA MARA KWA MARA
MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA AMUAGIZA KAMISHNA MKUU WA TRA KUKUTANA NA WAFANYABIASHARA MARA KWA MARA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiK23Zk6ziUSTFahHWXmCxE6LsJsVn3I9rmCdUOhpSMTjfEGt0BFQEYCMnV6EintSF3_yoxmS53VQEdBmoM1_-y4UJNmDcvAFKJVLfegiIDRU8ZgqTIo-X7cMbthW1p5O0aruTbiDyhJ6o/s640/2.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiK23Zk6ziUSTFahHWXmCxE6LsJsVn3I9rmCdUOhpSMTjfEGt0BFQEYCMnV6EintSF3_yoxmS53VQEdBmoM1_-y4UJNmDcvAFKJVLfegiIDRU8ZgqTIo-X7cMbthW1p5O0aruTbiDyhJ6o/s72-c/2.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/makamu-wa-rais-mama-samia-amuagiza.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/makamu-wa-rais-mama-samia-amuagiza.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy