MAKALA; TANZANIA YAJIZATITI KUHIMILI MABADILIKO YA TABIA NCHI PWANI YA BAHARI YA HINDI.

                       Na. Lilian Lundo – MAELEZO Mabadiliko ya Tabianchi ni moja ya eneo ambalo limekuwa likileta athari kubwa katika...


                       Na. Lilian Lundo – MAELEZO
Mabadiliko ya Tabianchi ni moja ya eneo ambalo limekuwa likileta athari kubwa katika nchi nyingi Duniani
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zimeweka mikakati mbalimbali katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Moja ya mikakati hiyo ni pamoja na ujenzi wa kuta kwenye Pwani ya Bahari ya Hindi, upandaji wa mikoko ikiwa ni pamoja na uchimbaji wa mifereji ya maji ya mvua na maji machafu
 
Siku za hivi karibuni kumekuwa na mvua zisizo na majira na kupungua upatikanaji wa maji safi kwa watu wa Kijiji cha Namakongoro Mkoani Lindi, nchini Tanzania na Magharibi mwa bara la Afrika


Akitoa taarifa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Mkurugenzi Idara Mazingira, Ofisi ya Makamu wa Rais, Richard Muyungi anasema Mradi wa kujenga uwezo wa kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi katika Pwani ya Bahari ya Hindi jijini  Dar es Salaam unatekelezwa katika maeneo manane na unagharimu dola za kimarekani milioni tano..
Bwana Muyungi anasema maeneo ambayo mradi huo unatekelezwa kuwa ni eneo la Obama Ocean Road, Kigamboni kwenye Chuo cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere, Bungoni Ilala, Miburani Mtoni, Temeke, Salender Bridge, Kunduchi, Mbweni na Ununio Kinondoni.
Anasema jumla ya Dola za Marekani 3,489,482 zimetengwa  kwa ajili ya miundombinu ya ujenzi wa ukuta eneo la  Ocean Road na Kigamboni pamoja na mitaro iliyopo Bungoni, Ilala na Mtoni Temeke
Katika ziara hiyo Bwana Muyungi anazitaja shughuli nyingine zinazotekelezwa katika mradi huo ni pamoja na kukarabati ukuta wa bahari katika maeneo ya barabara ya Obama ambayo zamani ilijulikana kama Ocean Road wenye  urefu wa mita 820  na Kigamboni eneo la Chuo cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere, urefu wa mita 380, ambapo ukuta huo utadumu kwa zaidi ya miaka 73.
Pamoja na matengenezo hayo, fedha nyingine zitatumika kutoa mafunzo kuhusu nishati safi ya kurudisha mikoko ekari 40 ya mwambao wa Pwani ya Bahari ya Hindi katika maeneo ya Jiji la Dar es Salaam.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira Zanzibar (ZEMA), Sheha Mjaja anaeleza miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni pamoja na  mradi wa kujenga uwezo wa kuhimili athari za mabadiliko ya Tabianchi katika maeneo ya ukanda wa Pwani (mradi wa LDCF).
“Mradi huu unatekelezwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ofisi ya makamu wa Rais katika maeneo ya Bagamoyo, Pangani, Rufiji na Zanzibar na unafadhiliwa na Mfuko wa Dunia wa Mazingira (The Global Environmental Facility- GEF) kupitia dirisha la Mfuko wa Nchi Masikini Duniani (The Least Developed Countries Fund – LDCF) la Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi – UNFCCC,” anafafanua Sheha Mjaja.

Anafafanua kuwa fedha za Mradi huo zinapitia Shirika la Usimamizi wa Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) ambalo pia lina jukumu la kutoa ushauri wa kitaalamu na usimamizi wa fedha na Jumla ya Dola za Kimarekani milioni  3,356,300 zimepangwa kutumika katika mradi huu zikijumuisha fedha za usimamizi na ufuatiliaji za UNEP ambapo Utekelezaji wa Mradi huu ulianza mwaka 2013 na unategemewa kumalizika mwaka 2017.

Mkurugenzi mkuu huyo wa ZEMA amezitaja shughuli zitakazofanyika katika mradi huo ni upandaji wa mikoko/mikandaa na miti ya ukanda wa pwani katika maeneo 6 ya Unguja na Pemba pamoja na ujenzi wa kuta za bahari katika eneo la Kilimani mjini Unguja na Kisiwa Panza, wilaya ya  Mkoani Pemba.
Anafafanua kuwa, eneo la Kilimani ambalo ufukwe wake una urefu wa mita 538 litajengwa kuta mbili (2) za aina ya “gyrones”,ambapo kila ukuta  utakuwa na urefu wa mita 100 kutoka kwenye fukwe kuelekea baharini na  ukuta mwingine utajengwa eneo la Kisiwa Panza ambao utakuwa na  urefu wa mita 75.

Kuhusu mradi wa LDCF kwa upande wa Zanzibar, Bwana Muyungi anasema fedha zote za mradi huko, zimegawanyika katika maeneo matatu ambayo ni upande wa mikoko na miti ya ukanda wa Pwani ambapo jumla ya Shilingi 163,895,500 zimepangwa kutumika.
Eneo lingine ni fedha za ujenzi wa ukuta wa Kisiwa Panza na Kilimani, ambapo gharama halisi za kuta hizo bado hazijajulikana, ila zitajulikana baada ya zabuni zilizoitishwa kutangazwa. Zabuni hizo zitasimamiwa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia huduma za miradi (The United Nations Office for Project Services-UNOPS) ambao ndio washauri wa ujenzi wa kuta hizo.

Anasema eneo la mwisho ni fedha kwa ajili ya usimamizi na ufuatiliaji wa mradi ambapo kila Taasisi inayotekeleza mradi huo imetengewa jumla ya Dola za Kimarekani 8,600.0 kwa mwaka kwa ajili ya kuwalipa wasimamizi wa mradi  na kuendesha shughuli za mradi katika maeneo ya utekelezaji ikiwa ni pamoja na mafuta, ununuzi wa shajala (stationery) na gharama za ufuatiliaji.

Hata hivyo, SMZ imekamilisha Mradi wa ujenzi wa mitaro ya maji ya mvua na maji machafu kwa shehia za Msingini na Kichungwani katika mji wa Chake Chake Pemba kupitia Idara ya Mazingira Zanzibar kwa kushirikiana na wanajamii kupitia kamati za jamii za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF) za Shehia hizo.
Aidha, mradi huo umepata fedha kutoka Shirika la Umoja la Mpango wa Mazingira (UNEP), TASAF, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Aqua-4-All ya Uholanzi ambapo mradi ulianza mwaka 2009 na kumalizika mwaka 2013
Malengo ya SMZ ni kuwepo mtaro wa maji ya mvua yasiyochanganyika na maji machafu yanayotoka majumbani, kupunguza uchafuzi wa mazingira ya bahari pamoja na viumbe vyake unaotokana na maji machafu yanayotoka majumbani kwa kuyasafisha kabla ya kuingia baharini.

Nae, Abdul Juma mkazi wa Kinondoni Jijini Dar es Salaam anazipongeza Serikali ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa namna zinavyojizatiti kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa kutunza na kukarabati kuta za Pwani ya bahari ya Hindi.

Anasema, Serikali imefanya uamuzi mzuri wa kujenga kuta mpya katika kingo za Bahari ya Hindi ambapo kama kuta za zamani zingeendelea kuwepo zingeleta athari kwa nyumba zinazopakana na Bahari kutokana na kuta hizo kuchoka na kuwa na nyufa.

Anatoa rai kwa Watanzania kuiunga mkono Serikali katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kwa kutunza vyanzo vya maji, kupanda miti pamoja na kutunza miundombinu ambayo imejengwa kwa ajili ya kuzuia athari za mabadiliko ya tabianchi.

Kwa upande wake, Asha Said mkazi wa Chake chake Pemba ameipongeza SMZ kwa kutekeleza mradi wa ujenzi wa mitaro ya maji ya mvua na maji machafu kwa shehia za Msingini na Kichungwani ambapo kabla ya utekelezaji wa mradi huo wakazi wa maeneo hayo  walikuwa wakipata kero ya kuingiliwa na maji majumbani mwao katika kipindi cha mvua.

Ameendelea kwa kusema kuwa kukamilika kwa mradi huo kumeleta ukombozi kwa wananchi wa maeneo hayo ambapo kuna wakati iliwalazimu kuhama katika makazi yao kutokana na kero ya kujaa maji katika nyumba zao.

Matarajio ya SMZ na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuendelea kuimarisha mashirikiano, uzoefu na utaalamu wa kimazingira katika kuhakikisha kuwa Zanzibar na Tanzania Bara zinaendelea kutekeleza miradi ya kimazingira ya pamoja kwa faida endelevu ya kiuchumi, kijamii na kimazingira.COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAKALA; TANZANIA YAJIZATITI KUHIMILI MABADILIKO YA TABIA NCHI PWANI YA BAHARI YA HINDI.
MAKALA; TANZANIA YAJIZATITI KUHIMILI MABADILIKO YA TABIA NCHI PWANI YA BAHARI YA HINDI.
https://2.bp.blogspot.com/-_iiVfsVOd-E/WPodUUaSoFI/AAAAAAAA8YE/wbzKVCvy-zAn4GMWfDi0bSUTV0yTMQ2qQCLcB/s640/Tanzania-facing-Climate-c-001.jpg
https://2.bp.blogspot.com/-_iiVfsVOd-E/WPodUUaSoFI/AAAAAAAA8YE/wbzKVCvy-zAn4GMWfDi0bSUTV0yTMQ2qQCLcB/s72-c/Tanzania-facing-Climate-c-001.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/makala-tanzania-yajizatiti-kuhimili.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/makala-tanzania-yajizatiti-kuhimili.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy