DKT. HARRISON MWAKYEMBE AWATAKA VIJANA KUTENGA MUDA WAO KUJISOMEA VITABU

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mkwakyembe (kulia) akiwa amepokelewa na Mwandishi wa kitabu cha "...


Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mkwakyembe (kulia) akiwa amepokelewa na Mwandishi wa kitabu cha "Colour of Life", Bi. Ritha Tarimo siku ya uzinduzi wa kitabu hicho leo 30 Aprili, 2017 Jijini
Dar es Salaam.


Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mkwakyembe pamoja na wageni waalikwa wakiangalia video inayoelezea maduhui ya kitabu cha "Colour of Life"
kilichoandikwa na Mwandishi wa vitabu Bi. Ritha Tarimo, 30 Aprili, 2017 Jijini
Dar es Salaam.






Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mkwakyembe akiongea na wageni
waalikwa wakati wa uzinduzi wa kitabu cha "Colour of Life"
kilichoandikwa na Mwandishi wa vitabu Bi. Ritha Tarimo 30 Aprili, 2017 Jijini
Dar es Salaam.




Mwandishi wa vitabu Bi. Ritha Tarimo akiongea na wageni
waalikwa wakati wa uzinduzi wa kitabu chake cha "Colour of Life"leo 30 Aprili, 2017 Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mkwakyembe akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kitabu cha "Colour of Life"
kilichoandikwa na Mwandishi wa vitabu Bi. Ritha Tarimo. 30 Aprili, 2017 Jijini
Dar es Salaam.


Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mkwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na familia ya Mwandishi wa vitabu Bi. Ritha Tarimo mara baada ya uzinduzi wa kitabu hicho 30 Aprili, 2017 Jijini
Dar es Salaam.


Waziri
wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mkwakyembe akiwa katika
picha ya pamoja na familia ya Mwandishi wa vitabu Bi. Ritha Tarimo pamja na wageni waalikwa mara baada
ya uzinduzi wa kitabu hicho 30 Aprili, 2017 Jijini
Dar es Salaam.
(PICHA/HABARI NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM)




Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt.
Harrison Mwakyembe amewataka vijana kutumia muda wao kujenga utamaduni wa
kujisomea vitabu badala ya kupoteza muda wao mwingi katika mitandao ya kijamii
kwakuwa kusoma vitabu ndiyo msingi mzuri wa elimu.





Kauli hiyo ameitoa leo Jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa
akizindua Kitabu cha “Colour of Life” kilichoandikwa na Mwandishi Bi. Ritha
Tarimo  ambapo katika hotuba yake
aliyoitoa mbele ya wageni waalikwa amesisitiza suala la vijana kujenga
utamaduni wa kupenda kusoma vitabu ili kukuza elimu yao.





Mhe. Mwakyembe ameeleza kuwa, baadhi ya vijana siku hizi wamekuwa
wakitumia muda wao mwingi katika mitandao ya kijamii badala ya kujisomea, hivyo
amewashauri wajifunze kutoka kwa Mwandishi wa Kitabu hicho ili waje kuwa
waandishi hodari wa kutegemewa na Taifa.





Sambamba na rai hiyo, Waziri Mwakyembe amempongeza Bi. Ritha
Tarimo kwa juhudi zake kubwa na maarifa katika kutunga na kuandika kitabu hicho
ambacho amesema kuwa kitabu hicho ni kizuri na kina maudhui mazuri kwa vijana
hususani wanafunzi, hivyo ameitaka jamii kumuunga mkono kwa kukisoma ili jamii
ipate kuelimika.





“Ukimkuta mtu kama Ritha Tarimo anaandika kitabu katika
kipindi hiki ambapo vitabu vinaonekana kuondolewa kwasababu ya maendeleo ya
teknolojia, ni vema kumpa moyo na kumuunga mkono kwakuwa yeye ametuonyesha
Watanzania kuwa hata sisi tunaweza, na kitabu hiki niwaambie ukweli kina
maudhui ya kumtia moyo kijana ya kutokata tamaa katika maisha”, alisema Dkt.
Mwakyembe.





Ameongeza kuwa, Serikali inauunga mkono juhudi zake za
uandishi wa vitabu vyake na amechukua baadhi ya nakala za kitabu hicho kwa
ajili ya kuzipelekeka kwa Waziri husika wa masuala ya Elimu Sayansi na
Teknolojia ili kuona namna gani kitabu hicho kinaweza kuisaidia jamii.





Kwa upande wake Mwandishi Ritha Tarimo ameishukuru Serikali
kwa kukubali wito wa kukizindua kitabu chake na pia utayari wa Serikali katika
kumuunga mkono ili uandishi wake uwe wenye tija kwa jamii ya Watanzania.





Ameeleza kwamba, kazi ya uandishi ameinza muda mrefu na leo
ameweza kupata nafasi ya kuungwa mkono na Serikali pamoja na Watanzania
mbalimbali ikiwemo familia yake na hatimaye kukamilisha kitabu hicho na
kukizindua rasmi.





“Nakushukuru Mhe. Waziri kwa kutumia muda wako kuja
kukizindua kitabu hiki, nakushukuru sana na sasa naamini ndoto zangu zinatimia,
kitabu hiki nimekitengeneza katika umbo dogo ili kiweze kuwavutia watu wengi
kwani kina maudhui mazuri kwa vijana na jamii nzima ya Kitanzania”, alisema
Ritha.





Kitabu cha Colour of Life ni moja kati ya vitabu saba
alivyoandika Mwandishi huyo ambacho pia kimepata fursa ya kuzinduliwa na Waziri
Dkt. Harrison Mwakyembe na kwa mujibu wa mwandishi huyo, kitabu hicho kina
maudhui mazuri kwa vijana katika kuwajenga kimaisha.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: DKT. HARRISON MWAKYEMBE AWATAKA VIJANA KUTENGA MUDA WAO KUJISOMEA VITABU
DKT. HARRISON MWAKYEMBE AWATAKA VIJANA KUTENGA MUDA WAO KUJISOMEA VITABU
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgR1tKY-00B2zBMz26AMoEfvKUy5v3JrcZnJsO2qim59-WtA4vVSXEIAWva-6DjG3q0SC-l2yWStzFmiCv2cNqz3jV3mIMRpKne021ywOb43bkw9LmHfWumKiPvM5nqAqTcaYP5Ow0w/s640/PICHA+1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgR1tKY-00B2zBMz26AMoEfvKUy5v3JrcZnJsO2qim59-WtA4vVSXEIAWva-6DjG3q0SC-l2yWStzFmiCv2cNqz3jV3mIMRpKne021ywOb43bkw9LmHfWumKiPvM5nqAqTcaYP5Ow0w/s72-c/PICHA+1.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/dkt-harrison-mwakyembe-awataka-vijana.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/04/dkt-harrison-mwakyembe-awataka-vijana.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy