Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameutaka uongozi wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA) kushirik...
Akizungumza
na waandishi wa habari mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa
kivuko kipya cha MV Kazi, Bandarini jijini Dar es Salaam, Waziri Prof.
Mbarawa amesema kuwa kupitia mafunzo hayo Serikali itaweza kuokoa fedha
nyingi ambazo kwa sasa inatumia kulipa kampuni binafsi zinazojenga na
kukarabati vivuko
“Hakikisheni
mnapata ujuzi kama walionao hawa, hatutaki kutumia fedha za Serikali
kwa ajili ya kukarabati au kutengeneza vivuko wakati nyinyi TEMESA mpo”,
amesema Waziri Prof. Mbarawa
Pamoja
na ujenzi wa kivuko hicho Waziri Mbarawa amewataka Temesa kuhakikisha
wanasimamia na kukitunza kivuko hicho ili kiweze kudumu kwa muda mrefu.
Aidha,
Profesa Mbarawa ameuagiza Wakala huo kuhakikisha wanakamilisha mifumo
ya ukusanyaji mapato kwa njia ya kielektroniki ili ili kudhibiti mianya
ya rushwa.
Kuhusu
huduma za kivuko mkoani Lindi Serikali imesema itahakikisha inapelekea
huduma haraka iwezekanavyo ili kurahisisha usafiri kwa wananchi wa mkoa
huo.
Kwa
upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala huo Dkt. Musa Mgwatu, amemtaka
mkandarasi wa kampuni ya Songoro Marine Transport kuhakikisha anafanya
kazi usiku na mchana ili kukamilisha kivuko hicho kwa muda uliopangwa.
Dkt.
Mgwatu amefafanua kuwa kukamilika kwa kivuko hicho kutarahisisha usafiri
kwa wakazi wa Kigamboni na maeneo mengine ya jiji la Dar es salaam
ambao wamekuwa wakitumia huduma hiyo katka shughuli zao za kila siku.
Nae,
Meneja Mradi wa Kampuni ya Songoro Marine Transport, Bw. Major Songoro
amemhakikishia Waziri Mbarawa kumaliza kivuko hicho kwa wakati ambapo
amesema ifikapo tarehe 15 mwezi huu kivuko hicho kitakabidhiwa kwa
Serikali.
Bw.
Songoro amefafanua kuwa kwa sasa mafundi wanamalizia kazi ndogo ndogo
zilizobaki pamoja na kusubiri injini ambazo zinatarajiwa kuwasili
mwishoni mwa wiki hii.
Kivuko
kipya cha MV Kazi kimegharimu kiasi cha shilingi bilioni Saba na kina
uwezo wa kubeba abiria 800 na magari 22 kwa wakati mmoja.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Kivuko
cha MV. Kazi kikiwa katika hatua za mwisho za ujenzi wake.Kiuvko hicho
kitakamilika na kuanza tarehe 15 mwezi huu na kina uwezo wa kubeba
abiria 800 na magari 22 kwa wakati mmoja.
Meneja
Mradi wa Kampuni ya Songoro Marine Transport inayojenga Kiuvko cha MV.
Kazi, Bw. Major Songoro, akitoa ufafanuzi wa mashine kwa Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, alipokagua Kivuko
hicho jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (kulia),
akiangalia moja ya vifaa vilivyoko kwenye chumba cha kuendeshea kivuko
katika kivuko cha MV. Kazi kinachojengwa jijini Dar es Salaam. Kivuko
hicho kitakabidhiwa tarehe 15 Mwezi huu. Wa pili kushoto ni Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA), Dkt. Musa Mgwatu.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa
(kulia), akifafanua jambo kwa Uongozi wa Wakala wa Ufundi na Umeme
nchini (TEMESA), mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kivuko
kipya cha MV Kazi ambacho kinatengenezwa jijini Dar es salaam na Kampuni
ya Songoro Marine Transport.
Mafundi
wa Kampuni ya Songoro Marine Transport, wakiendelea na kazi ya kufunga
mashine katika Kivuko cha MV Kazi. Kivuko hicho kitakamilika na
kukabidhiwa wiki ijayo na kina uwezo wakubeba abiria 800 na magari 22
kwa wakati mmoja.
…………………………………………………………
COMMENTS