Na Daudi Manongi-MAELEZO Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali Bw.Mohamed Mtonga ametoa wito kwa wastaafu wanaolipwa Pensheni na Wizara ...
Na Daudi
Manongi-MAELEZO
Mkaguzi Mkuu wa Ndani
wa Serikali Bw.Mohamed Mtonga ametoa wito kwa wastaafu wanaolipwa Pensheni na
Wizara ya Fedha na Mipango ambao ni wagonjwa na hawawezi kufika katika viwanja
vya Karimjee na Mwalimu Nyerere(Sabasaba) kwa ajili ya uhakiki wa nyaraka zao
kutoa namba za simu na majina yao ili waweze kuhakikiwa pale walipo kama ni
Hospitali au nyumbani.
Bw.Mohamed Mtonga
ametoa wito huo leo Jijini Dar es Salaam wakati akiongea na waandishi wa habari
juu ya zoezi la uhakiki wa taarifa za wastaafu wanaolipwa pensheni na Wizara ya
Fedha na Mipango linalofanyika katika Jiji la Dar es Salaam kuanzia leo tarehe
6-10 Machi.
“Kwa sasa ninavyozungumza
zoezi hili liko kwenye hatua ya mwisho katika Mkoa wa Dar es Salaam,Zoezi hili
lilianza Mkoa wa Pwani na tumelifanya nchi nzima na limefanyika kwa ufanisi
mkubwa sana na wastaafu wengi wamejitokeza na kama mnavyoona zoezi limekuwa
likiendelea kwa utaratibu mzuri sana”, Aliongeza Bw.Mtonga.
Mtonga amesema wastaafu
hao wengi ni watumishi wa Serikali ambao walifanya kazi kabla ya mwaka 1999
ambapo walikuwa hawapo katika mifuko ya pensheni ndio ambao wanalipwa pensheni
na Serikali wakiwemo watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama.
Aidha amesema lengo
kubwa la kuhakiki wastaafu hao ni kuboresha daftari la wastaafu ili kusaidia
kujua ni kiasi gani cha wastaafu wapo katika kumbukumbu ya daftari la pensheni
na kusisitiza wastafu ambao hawatajitokeza watafutwa katika daftari hilo.
Ukaguzi huu kwa mara
ya mwisho ulifanyika mwaka 2014 na ukaanza tena mwezi Octoba mwaka 2016.
COMMENTS