ULAJI WA VYAKULA NA KUTOFANYA MAZOEZI WACHANGIA ONGEZEKO LA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZWA NCHINI

 Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro akichukuliwa vipimo  mara baada ya kuzindua wiki ya wanawake duniani ambayo kwa mkoa wa Aru...



 Mkuu wa wilaya ya Arusha
Gabriel Daqqaro akichukuliwa vipimo  mara baada ya kuzindua wiki
ya wanawake duniani ambayo kwa mkoa wa Arusha imeathimishwa katika
viwanja vya Sheikh Amri Abeid
 Muuandaaji ya wiki ya wanawake
duniani kwa mkoa wa Arusha Phidesia Mwakitalima wa kwanza kulia
akishuhudua jinsi mkuu wa wilaya ya Arusha akiwa anachukuliwa vipimo
vya afya yake






Mgeni Rasmi Mkuu wa wilaya ya Arusha, Mhe. Gabriel Fabian Daqarro akiwa anaingia uwanjani tayari kwa  uzinduzi rasmi zoezi la kupima moyo, cancer, kisukari, macho, magonjwa Sugu ya mfumo wa hewa bure yanayofanyika Arusha katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid  yaliyoandaliwa na Phide Entertainment kushirikiana na wafadhili mbalimbali ambapo kilele chake ni siku ya wanawake duniani
tar 8/3/2017



Habari picha na
Woinde Shizza, Arusha


Tatizo la baadhi ya Watanzania kula vyakula bila mpangilio na kutofanya mazoezi ili kulinda afya zao limechangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la magonjwa ya kisukari, kansa,na
shinikizo la damu.

Hayo yalisemwa na mtaalamu wa magonjwa ya yasiyoambukizwa kutoka hospitali ya mkoa wa Arusha, Mt meru, Dk Beatrice Ngogi wakati wa zoezi la upimaji wa afya bure lililofanyika jana katika uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid jijini hapa.

Akihojiwa na waandishi wa habari mtaalamu huyo alisema asilimia kubwa ya kundi la watu walioathirika na magonjwa yasiyoambukizwa ni kati ya umri wa miaka 45-60 na kudai kuwa  mtindo wa maisha ya watu umechangia kwa kiasi
kikubwa  ongezeko la magonjwa hayo.

“mtindo wa maisha umekuwa ni tatizo kubwa kwetu ndio maana tunawasihi watanzania tufanye mazoezi  na kuzingatia mlo wenye utaratibu”alisema mtaalamu huyo

Hatahivyo,mtaalamu wa magonjwa ya kisukari katika hospitali ya rufaa ya KCMC mkoani Kilimanajaro, DK Valeria Matei alisema kwamba  katika siku za karibuni watoto wadogo wanazaliwa wakiwa na ugonjwa wa kisukari mbali na wazee ambao ilikuwa imezoeleka.


Alisema kwamba elimu ya afya ni muhimu sana itolewe katika jamii ya watanzania kwa kuwa wengi wanakumbwa na ugonjwa huo bila kujijua na wakishajitambua ugonjwa huo unakuwa umeshawathiri kwa kiasi kikubwa.

Doroth Kuziwa, ambaye
ni mwathirika wa ugonjwa wa kisukari alisema ya kwamba alikuwa kubaini kuathirika na ugonjwa huo kwa muda mrefu huku akisisitiza kwamba vyakula vya wagonjwa wengi wa kisukari vimekuwa ghali hali ambayo inawafanya washindwe
kumudu gharama hizo.

Hatahivyo,Hiza Omary ambaye ni mgonjwa wa macho alisema kwamba aliacha kazi ya udereva kutokana na
kusumbuliwa na matatizo ya macho huku akisema kwamba vyombo vya habari vina jukumu kubwa la kuhabarisha umma kuhusu elimu ya afya katika jamii.

Mkurugenzi wa kampuni ya Phide Entertainment, Phidesia Mwakitalima alisema kwamba kampuni yake imeingia mkataba na hospitali za KCMC na Mt Meru kwa lengo la kufadhili  zoezi la upimaji wa afya bure kwa wakazi wa mkoa  wa Arusha  katika kuelekea siku ya wanawake duniani.

Alisema kwamba zoezi hilo litahitimishwa siku ya kilele cha siku ya mwanamke duniani  huku akisisitiza kundi la wanawake kuzingatia mfumo wa ulaji wa vyakula mbalimbali ili kuepuka magonjwa yasiyoambukizwa.


 Mmoja wa madaktari wanaotoa huduma akiwa anachukuwa damu salama kutoka kwa mwananchi ambaye amejitolea kuchangia damu
 Mmoja wa daktari akimpongeza mamaa mara baada ya kupimwa na kukutwa anaugongwa wa presha.
Dokta kutoka katika hospiotali ya kcmc akitoa elimu kwa wamama waliouthuria kupata huduma ya kupimwa bure.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mh Gabriel Fabian Daqarro Akisaini Daftari la Wageni la Phide Entertainment baada ya Uzinduzi wa Zoezi la kupima buree wananchi Moyo, Cancer, Kisukari, Macho na Magonjwa sugu ya
mfumo wa Hewa. Pamoja na changizo la Damu kwa ajili ya Ward za Wazazi Mkoani Arusha.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: ULAJI WA VYAKULA NA KUTOFANYA MAZOEZI WACHANGIA ONGEZEKO LA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZWA NCHINI
ULAJI WA VYAKULA NA KUTOFANYA MAZOEZI WACHANGIA ONGEZEKO LA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZWA NCHINI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiZR3MbDx1dX04SExjEAsf43F4FzmWtaP5gYyRcB7d_bwX9p1F51240tA5EXqiNYo18MCBBe_R1CAhpODY5nUh6VizfysHzneho3tq0pVWRNYfIHTGdk2s9BNm97HiI5XYIvFhL-m8uKVyG/s640/DSC00658.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiZR3MbDx1dX04SExjEAsf43F4FzmWtaP5gYyRcB7d_bwX9p1F51240tA5EXqiNYo18MCBBe_R1CAhpODY5nUh6VizfysHzneho3tq0pVWRNYfIHTGdk2s9BNm97HiI5XYIvFhL-m8uKVyG/s72-c/DSC00658.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/03/ulaji-wa-vyakula-na-kutofanya-mazoezi.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/03/ulaji-wa-vyakula-na-kutofanya-mazoezi.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy