Tundu Lissu, akiw...
Tundu Lissu, akiwa ameketi sanjari na
polisi wa mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam,
Machi 7, 2017 muda mfupi kabla ya kufutiwa mashtaka na serikali na
kukamatwa tena na polisi.
MWANASHERIA
Mkuu wa CHADEMA, ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu,
amefutiwa mashtaka ya uchochezi, baada ya Ofisi ya mashtaka ya serikali
kuieleza mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, Machi 6,
2017 kuwa haina haja ya kuendelea na kesi hiyo ya uchochezi.
Hata
hivyo Mwanasheria huyo machachari, alikamatwa hata kabla ya kuondoka kwenye
mahakama hiyo na sasa anashikiliwa kwenye kituo kikuu cha polisi jijini Dar es
Salaam.
Habari
za kukamatwa kwake amethibitisha Tundu Lissu mwenyewe kwenye ukurasa wake wa Facebook, akiuarifu
umma wa Watanzania.
“Nimekamatwa tena hapa hapa mahakamani Kisutu mara tu baada ya waendesha mashtaka wa serikali kunifutia kesi iliyotokana na kukamatwa kwangu bungeni Dodoma mwezi uliopita.”. Ameandika Tundu Lissu.
“Nimekamatwa tena hapa hapa mahakamani Kisutu mara tu baada ya waendesha mashtaka wa serikali kunifutia kesi iliyotokana na kukamatwa kwangu bungeni Dodoma mwezi uliopita.”. Ameandika Tundu Lissu.
Amesema
serikali imeifuta kesi hiyo kwa maelezo kwamba haina nia tena ya kuendelea na
kesi hiyo. “Sikutoka hata nje ya mahakama nikakamatwa tena. Wamenileta Central kwa mahojiano. Mapolisi walionikamata
wamekataa kuniambia wananikamata kwa kosa gani.” Ameendelea kuandika Tundu
Lissu ambaye anagombea Urais kwenye uchaguzi Mkuu wa chama cha Wanasheria
Tanzania, (TLS), utakaofanyika wiki ijayo jijini Arusha.
Tundu Lissu katika maelezo yake amesema “Nadhani
sababu ina uhusiano wa moja kwa moja na Uchaguzi wa Rais wa TLS unaofanyika
wiki ijayo. Serikali hii, kwa kutumia mawakili wao, imekuwa na mkakati mkubwa
wa kunizuia kugombea urais wa TLS.” Amesema Mwanasheria huyo.
COMMENTS