SERIKALI YAAHIDI KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VYA HABARI KATIKA KUJENGA TANZANIA YA VIWANDA

Na: Genofeva Matemu – WHUSM Serikali imeahidi kuendelea kutengeneza mazingira rafiki kwa kushirikiana na vyombo vya habari il...


Na: Genofeva Matemu – WHUSM

Serikali imeahidi kuendelea kutengeneza mazingira rafiki kwa kushirikiana na vyombo vya habari ili kwa pamoja kuweza kuhamasisha, kuunda na kujenga nchi ya viwanda katika kuunga mkono azma ya Rais Mhe. John Pombe Magufuli ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Mchezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokutana na wamiliki na watendaji waandamizi wa vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa mkutano huo Mhe. Nnauye amesema kuwa serikali na vyombo vya habari wakishirikiana na kuwa na lengo moja wataweza kuileta Tanzania pamoja na kuiweka katika mwelekeo ulio sahihi. 

“Tukiamua leo kila chombo cha habari kikawa na dawati maalumu linalozungumzia Tanzania ya viwanda kama ilivyo kwa madawati mengine ndani ya vyombo vyetu vya habari, na serikali ikaendelea kutoa hamasa za uanzilishwaji wa viwanda ambavyo vitasukumwa na dawati hilo maalumu la viwanda, tutaweza kutimiza ndoto yetu ya Tanzania ya Viwanda” amesema Mhe. Nnauye

Akizungumza wakati wa mkutano huo Bw. Francis Nanayi kutoka Kampuni ya Magazeti ya Mwananchi amesema kuwa ili vyombo vya habari viweze kutangaza habari vinahitaji kupata ushirikiano wa kutosha kutoka serikalini kuonyesha mikakati na malengo ya serikali kuwezesha vyombo vya habari kujenga Tanzania ya viwanda na kuwapa fursa wananchi kupata taarifa sahihi za nchi. 

Naye Mtendaji kutoka Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) Mabeli Masasi amesema kuwa Mapinduzi ya viwanda yanaweza kufanyika kama vyombo vya habari vitatoa taarifa sahihi za upatikanaji wa malighafi za uwekezaji kulingana na mahitaji yaliyopo katika maeneo husika na kuwekeza katika viwanda vidogovidogo vitakavyozalisha viwanda vikubwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari Dkt. Hassan Abbas amesema kuwa atahakikisha maafisa habari wa serikali hususani maafisa wanaohusika na Sekta ya viwanda wanatoa ushirikiano wa kutosha kwa vyombo vya habari ili kuweza kuelimisha umma namna Tanzania ya Viwanda inavyojengwa.
 
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akiongea na wamiliki wa vyombo vya Habari (hawapo katika picha) wakati wa mkutano wa Wadau Tuzungumze kuhusu namna vyombo vya habari vinavyoshiriki katika kufanikisha azma ya Tanzania kuwa nchi ya viwanda leo Jijini Dar es Salaam. katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel na kushoto ni  Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Dkt. Jimy Yonazi.
 

 Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Dkt. Hassani Abbas akitoa ufafanuzi kwa wamiliki wa vyombo vya habari namna uratibu wa matangazo utakavyokuwa ukiendeshwa  na Serikali wakati wa mkutano wa Wadau Tuzungumze leo Jijini Dar es Salaam. 
 
 
 Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Dkt. Jimy Yonazi akifafanua jambo wakati wa mkutano wa Wadau Tuzungumze uliowakutanisha wamiliki wa vyombo vya Habari  nchini kujadili nafasi ya vyombo vya habari katika kujenga Tanzania ya viwanda. Wanaomsikiliza kulia ni Katibu Mkuu Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel,Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye pamoja na . Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Dkt. Hassani Abbas.
 
 Mkurugenzi wa Vipindi kutoka Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akichangia wakati wa mkutano uliowakutanisha wamiliki wa Vyombo vya Habari ikiwa ni muenedelezo wa vipindi vya Wadau Tuzungumze kinachoratibiwa  na Wizara wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo lengo likiwa ni kuimarisha ushirikaiano baina ya Wizara na wadau wa sekta zake.
 
 Mdau wa Habari, Hamza Kasongo akifafanua jambo wakati wa mkutano wa Wadau Tuzungumze uliowakutanisha wamiliki wa Vyombo.
 
Baadhi ya Wadau waliohudhuria mkutano wa Wadau Tuzungumze kuhusu namna vyombo vya habari vinavyoshiriki katika kufanikisha azma ya Tanzania kuwa nchi ya viwanda leo Jijini Dar es Salaam. (PICHA NA MICHUZI JR)
 
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa habari mara baada ya kumaliza mkutano wa Wadau Tuzungumze ambapo uliwakutanisha wamiliki wa vyombo vya habari huku mada kuu ikiwa ni nafasi ya vyombo vya habari katika kuijenga Tanzania ya Viwanda leo Jijini Dar es Salaam.
 

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa habari mara baada ya kumaliza mkutano wa Wadau Tuzungumze ambapo uliwakutanisha wamiliki wa vyombo vya habari huku mada kuu ikiwa ni nafasi ya vyombo vya habari katika kuijenga Tanzania ya Viwanda leo Jijini Dar es Salaam.
 

 Katibu Mkuu Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel.
 
 
Bw. Francis Nanayi kutoka Kampuni ya Magazeti ya Mwananchi.
 
 
 
 Mwakilishi wa ITV/Radio One Steven Chuwa.
 
 
 Mdau wa vyombo vya habari, Theophil Makunga akitoa maoni yake.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: SERIKALI YAAHIDI KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VYA HABARI KATIKA KUJENGA TANZANIA YA VIWANDA
SERIKALI YAAHIDI KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VYA HABARI KATIKA KUJENGA TANZANIA YA VIWANDA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj5Ifs_JbavCsTq9sK45OxSgwhy6CAuGa9ohEX3tuIxYwcBMV9s6MhaIvaWIyonOU6geKPfPOjejvXpQAMllcJhJqOIcivSDXXB8tkNBDemnRNbG8g1qvcCd8bNZ4I1hcv7eCb4Mkng6Eo/s640/6.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj5Ifs_JbavCsTq9sK45OxSgwhy6CAuGa9ohEX3tuIxYwcBMV9s6MhaIvaWIyonOU6geKPfPOjejvXpQAMllcJhJqOIcivSDXXB8tkNBDemnRNbG8g1qvcCd8bNZ4I1hcv7eCb4Mkng6Eo/s72-c/6.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/03/serikali-yaahidi-kushirikiana-na-vyombo.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/03/serikali-yaahidi-kushirikiana-na-vyombo.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy