RAIS MAGUFULI AIPA "MENO" TANESCO. ZANZIBAR NA TAASISI NYETI SASA KUKATIWA UMEME KWA MADENI.

Rais John Pombe Magufuli, akizindua Mradi wa ujenzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme wa Kilovolti 132kv, mkoani Mtwara leo Machi ...Rais John Pombe Magufuli, akizindua Mradi wa ujenzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme wa Kilovolti 132kv, mkoani Mtwara leo Machi 5, 2017. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo. (PICHA NA IKULU)
NA K-VIS BLOG

RAIS John Pombe Magufuli, amelipongeza Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO) kutokana na kasi yake ya kusambaza umeme nchini hususan vijijini.

Rais aliyasema hayo Machi 5, 2017 wakati akizindua Mradi wa ujenzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme wa 132kv mkoani Mtwara.


Mradi huo utakamilika Mei 30, 2017 na kitahudumia mikoa ya Mtwara na Lindi na hivyo kutatua kero ya upatikanaji umeme kwenye mikoa hiyo ambayo shughuli za kiuchumi zimeongezeka sana. Awali kituo hicho kwa sasa kina uwezo wa 33kv.


“TANESCO mmenifurahisha sana kwa kutekeleza vema ilani ya uchaguzi ya CCM, kwa kuhakikisha wanachi kote nchini wakiwemo wa vijijini wanapatiwa umeme.”
Alisema. Rais pia alisema, anatambua changamoto
zinazolikabili shirika hilo hususan madeni ya bili za umeme kwenye taasisi za serikali.

"Ninaagiza, wale wote wanaodaiwa bili za umeme na TANESCO, walipe madeni yao haraka, vinginevyo muwakatie umeme." Alisema Rais.
Alisema"Hata Ikulu kama inadaiwa we kata, najua pia kuna deni la shilingi Bilioni 162 Kule Zanzibar, nako kama hawatalipa kateni umeme. tunataka TANESCO iharakishe kusambaza umeme kwa wananchi sasa wasipolipwa madeni watawezaje
kuifanya kazi hiyo kwa ufanisi.?". Aliuliza Rais Magufuli. Aidha kutokana na kufurahishwa na kasi ya TANESCO kusambaza umeme kwenye maeneo Mengi ya nchi,
amesema ofisi yake iko tayari kusaidia fedha pale itakapoonekana kuna mkwamo wa kifedha katika utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya umeme.
 Rais Magufuli (wa pili kushoto), Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa tatu kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO, Dkt. Alexander Kiaruzi, na Mwenyekiti wa CCC mkoa wa Mtwara, wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa kituo hicho.
 Rais akiandika kitu, wakati akiteta na Profesa, Muhongo wakati wa uzinduzi huo.
 Rais akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa TANESCO baada ya kupiganao picha.
 Rais Dkt.John Pombe Magufuli akihutubia." Najua kule Zanzibar TANESCO inadai karibu shilingi Bilioni 162, nako kama hawatalipa kata umeme" Alisema Rais katika hotuba take.
 Rais Magufuli na Mmiliki wa kiwanda cha Dangote, Alhaji Aliko Dangote, (walioshika bendera), wakizindua safari za malori hayo ya kubeba saruji.
 Rais Magufuli akipeana mikono na Alhaji Dangote


 Rais akihutubia kwenye hafla ya uzinduzi Wa malori ya Dangote.COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: RAIS MAGUFULI AIPA "MENO" TANESCO. ZANZIBAR NA TAASISI NYETI SASA KUKATIWA UMEME KWA MADENI.
RAIS MAGUFULI AIPA "MENO" TANESCO. ZANZIBAR NA TAASISI NYETI SASA KUKATIWA UMEME KWA MADENI.
https://1.bp.blogspot.com/--cNnTur_duA/WLw2hYoziII/AAAAAAAAyuM/Ji4nZqJtzXQsqoHmFiDtfz4EbIqHUPsjACLcB/s640/11.jpg
https://1.bp.blogspot.com/--cNnTur_duA/WLw2hYoziII/AAAAAAAAyuM/Ji4nZqJtzXQsqoHmFiDtfz4EbIqHUPsjACLcB/s72-c/11.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/03/rais-magufuli-aipa-meno-tanesco.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/03/rais-magufuli-aipa-meno-tanesco.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy