MSHINDI WA TIGO REACH FOR CHANGE KUTANGAZWA MACHI 9

Washiriki Wa Tigo Reach For Change Waliofanikiwa kuingia Katika Mchujo wa Mwisho wakiwasilisha wazo lao ubunifu Mbele ya Majaji Mapema w...

Washiriki Wa Tigo Reach For Change Waliofanikiwa kuingia Katika Mchujo wa Mwisho wakiwasilisha wazo lao ubunifu Mbele ya Majaji Mapema wiki hii katika Ofisi za Makao Makuu Ya  Tigo, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Majaji wa Tigo Reach for Change wakimsikliza kwa makini mmoja wa washiriki aliyefanikiwa kuingia katika mchujo 

Na Mwandishi Wetu

  Mashindano ya mwaka huu  ya Waleta mabadiliko ya kidijitali wa Tigo yamefikia katika hatua ya juu  ya kuchagua washindani watano  kufuatia mchakato wa mapitio ambao ulijumuisha waombaji 358. Shindano hili hufanyika kila mwaka na liko wazi  kwa waombaji kutoka  nchi nzima  limejielekeza katika  kuibua vijana mahiri  walio na ubunifu wa miradi ya kidijitali inayoboresha maisha ya watu, hususani watoto kwa kutumia programu za kidijitali.

  Vijana watano wanaoingia katika hatua ya fainali  hupata nafasi ya kuhudhuria warsha  ya maendeleo ya maudhui ya siku mbili pamoja na kuwasilisha miradi yao wakisubiri uthibitisho wa mwisho  kutoka kwa jopo la wataalamu wa ndani na nje katika ujasiriamali na stadi za  kidijitali.

  Waleta mabadiliko  wa Kidijitali wa Tigo ni wazo  la Kampuni ya Tigo kwa kushirikiana na asasi isiyo ya kiserikali ya Reach-for- Change ikiwa ni programu ya ushauri na  kuunga mkono  ambayo inawapa washindi fursa ya kuanzisha ujasiriamali endelevu katika maeneo ya elimu,  ujumuishwaji wa kidijitali na shughuli za ujasiriamali.

  Meneja wa Huduma za kijamii wa Tigo, Halima Okash alisema kuwa  washindi wawili wa kwanza  watapata  fedha taslimu dola 20,000 (takribani shilingi milioni 44,000,000) kuwezesha utekelezaji wa maudhui yao.


  “Miradi hii ina matokeo makubwa kijamii, inatoa masuluhisho halisi  kwa matatizo  yanayoikabili jamii  na yana umuhimu katika  kuboresha moja kwa moja maisha na hususani maisha ya watoto,” alisema Okash, akibainisha kuwa kampuni hiyo ya simu  tayari imeshawasaidia  wajasirimali kijamii tisa kupitia mkakati wa waleta mabadiliko wa Tigo (Tigo Digital Changemakers).

Huu ni mwaka wa sita  ambapo Tigo na Reach-for-Change wanaendesha shindano la kutafuta  wajasiriamali kijamii.Mshindi wa mwaka huu  atatangazwa Machi 9.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MSHINDI WA TIGO REACH FOR CHANGE KUTANGAZWA MACHI 9
MSHINDI WA TIGO REACH FOR CHANGE KUTANGAZWA MACHI 9
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgZg6l9Zkx_RDlmvzCw6UmWtIrJYs7vjNiKBdm9tfUD7M1C8BTxfLABkutHig7HTGWAWJgGGZwepFQAZaRiCD0BO5zow2dzCo3FZJT-UfRyi9yjAj-ahXoDtpc4c4hUO_cszdky2zMQXwQ/s640/photo78.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgZg6l9Zkx_RDlmvzCw6UmWtIrJYs7vjNiKBdm9tfUD7M1C8BTxfLABkutHig7HTGWAWJgGGZwepFQAZaRiCD0BO5zow2dzCo3FZJT-UfRyi9yjAj-ahXoDtpc4c4hUO_cszdky2zMQXwQ/s72-c/photo78.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/03/mshindi-wa-tigo-reach-for-change.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/03/mshindi-wa-tigo-reach-for-change.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy