KAMATI YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI YATEMBELEA MRADI WA UMEME WA KINYEREZI JIJINI DAR ES SALAAM

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt.  Juliana Pallangyo, (aliyesimama), akizung...








Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo, (aliyesimama), akizungumza mbele ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, wakati wa ziara ya kamati hiyo kutembelea Mradi wa
Umeme wa Kinyerezi jijini Dar es Salaam, leo Machi 23, 2017







Meneja Msimamizi wa Mradi wa Kinyerezi I, Yuka Mukaibo kutoka kampuni inayojenga mradi huo ya Sumitomo kutoka Japan, akizungumza mbele ya wajumbe wa Kamati walipotembelea eneo la Mradi jijini Dar es Salaam, Machi 23, 2017. Wakwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Palangyo, na wakwanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka.


 Naibu Mkurugenzi wa TANESCO, Mhandisi Khalid James, (aliyesimama), akitoa ufafanuzi wa utekelezaji wa Mradi huo mbele ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini waliotembelea kujionea maendeleo ya Mradi huo.







NA K-VIS BLOG

SHIRIKA la Umeme Tanzania, (TANESCO), limeomba Kamati
ya Bunge ya Nishati na Madini ishauri Mamlaka iruhusu mizigo yake iliyokaa bandarini kwa muda mrefu kutokana na swala la kodi iruhusiwe ili iweze kukamilisha Mradi wa ujenzi wa Mradi wa Umeme wa Gesi wa Kinyerezi. Hayo yamesemwa na uongozi wa TANESCO wakati wa ziara ya Kamati hiyo iliyofanya kwenye Mradi huo jijini Dar es Salaam, Machi 23, 2017 ili kujionea maendeleo ya ujenzi wa Mradi huo  muhimu.

“Mashine na vifaa vilivyozuiwa bandarini viruhusiwe ili vikakamilishe mradi wa umeme wa Kinyerezi I&II na kodi
zinazopaswa kulipia mashine hizo zilipwe baadaye ili kuruhusu kazi ya kufunga mitambo hiyo kwenye Mradi huo iweze kukamilika kwa wakati.” Alisema Meneja wa
Mradi kutoka TANESCO akiiambia kamati hiyo

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka, naye aliongeza  kwa kusema, “inatupa shida wakati mwingine, wakati hela inatakiwa tulipe kule bandarini, uwezo wa TANESCO
katoka makusanyo sio mzuri sana kutokana na madeni, hivyo kama tungeweza kuruhusiwa kutoa vifaa hivyo bandarini, ingekuwa vema kwani kasi ya ukusanyaji mapato ya TANESCO inapoongezeka ndivyo tunavyoweza kulipa lakini Mradi utakuwa
umeendelea.” Alisema Dkt. Mwinuka.

Mradi wa Kinyerezi I&II utakapokamilika,
utaweza kuzalisha umeme wa Megawati 425, Naibu Mkurugenzi wa TANESCO, Mhandisi Khalid James aliwaambia wajumbe wa Kamati hiyo. “Megawati hizi zitaunganishwa kwenye Gridi ya Taifa na hivyo kuongeza umeme.” Alisema Mhandisi James.

Mradi wa Kinyerezi I utagharimu kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 188 huku Mradi wa Kinyerezi II ukigharimu kiasi cha Dola
za Kimarekani Milioni 344, aliongeza Mhandisi James.









Meneja Mkazi wa Mradi wa Umeme wa Gesi wa Kinyerezi II,  Markku Repo kutoka kampuni ya Jacobsen Elektro(aliyenyoosha mkono), akifafanua mambo mbele ya wajumbe
wa Kamati wakati wa ziara yao. Wakwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu Nishati na Madini, Dkt. Juliana Palangyo.


 Wajumbe wakitembelea Mradi huo huku wakiongozwa na Meneja Msimamizi wa Mradi, kutoka kampuni ya Japani ya Sumitomo.

Baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo, waksikiliza kwa makini maelezo yaliyokuwa yanatolewa na wataalamu wa TANESCO na wajenzi wa mradi huo.


COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: KAMATI YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI YATEMBELEA MRADI WA UMEME WA KINYEREZI JIJINI DAR ES SALAAM
KAMATI YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI YATEMBELEA MRADI WA UMEME WA KINYEREZI JIJINI DAR ES SALAAM
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjE63tG0G34-PfkuxHeITVe777xmBuFb8drJXeDDviJX_PCHRph00sSYA4j_BtzvtnO86TRLuIAcQUcgM3d2wJnbrHtgakYzMj1KE-qs04XLJkQPN0l58_zmppDmOWTUnegaiu8Ccm0w-8/s640/wab-09.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjE63tG0G34-PfkuxHeITVe777xmBuFb8drJXeDDviJX_PCHRph00sSYA4j_BtzvtnO86TRLuIAcQUcgM3d2wJnbrHtgakYzMj1KE-qs04XLJkQPN0l58_zmppDmOWTUnegaiu8Ccm0w-8/s72-c/wab-09.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/03/kamati-ya-bunge-ya-nishati-na-madini.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/03/kamati-ya-bunge-ya-nishati-na-madini.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy