Gwiji wa soka duniani kutoka klabu ya Liverpool nchini Uingereza, John Barnes jana amewanoa wachezaji wa timu ya taifa ya vijana chini y...
Gwiji
wa soka duniani kutoka klabu ya Liverpool nchini Uingereza, John Barnes
jana amewanoa wachezaji wa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 15
(Serengeti Boys) katika siku yake ya kwanza nchini katika kuadhimisha
miaka 100 ya benki ya standard Chartered tangu kuanzishwa kwake.
“ni
muhimu sana kwa kuwafundisha vijana wadogo soka katika umri huo ni wito
kwa viongozi wa soka hapa Tanzania na wadau wote wa michezo kuweka
nguvu zao za kutosha kwa vijana maana ni tegemeo la siku za usoni.
,,,,,,
ni muhimu kama taifa kuwekeza kwa vijana kuwaweka mazingira na
miundombinu ya kutosha kabisa ili kuweza kuinua vipaji vyao vya soka na
ndio staili inayotumiwa na mataifa yaliopiga hatua kubwa kwenye
maendeleo ya mpira wa miguu,” amesema Barnes
Gwiji
wa soka duniani kutoka klabu ya Liverpool nchini Uingereza, John Barnes
akizungumza jambo na walimu wa viwanja vya JK Youth Park mara baada ya
kuwasili uwanjani hapo kwa ajili ya kuifunda timu ya taifa ya vijana
chini ya miaka 15 (Serengeti Boys) akiwa kwenye ziara ya siku tatu
nchini.
Katika
siku yake ya tatu (leo) nchini gwiji huyo wa soka atashuhudia fainali
ya timu tatu kutoka nchini za Tanzania, Uganda na Kenya ambao
watapambana vikali kuwania kombe la Standard Chartered 2017 safari ya
kuelekea Anfield mjini Liverpool nchini Uingereza.
Barnes
amesistiza muhimu wa kuwafunda vijana wadogo wakiwa katika umri mdogo
kabisa kama njia bora ya kuwaandaa kuwa wachezaji bora siku za usoni na
kuwa tegemeo katika nchini yao. Mkuu wa kitengo cha Mahusiano na Masoko
wa Benki hiyo, Bi Juanita Mramba amesema kwamba Azania Group of
Companies kutoka Tanzania, Capital Fm-Kenya na Coca Cola ya Uganda
watamenyana vikali kwenye fainali hizo kesho kwenye viwanja vya Jk Youth
Park, Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam.
“Tumeweza
kumleta John Barnes kushiriki kwenye mazoezi ya vijana chini ya miaka
15 kwa ajili ya kuwaanda kwenye mashindano ya AFCON ya vijana mwakani,
lakini pia amekuja kwa ajili ya tukio la benki hiyo kutimiza miaka 100
tangu kuanza shughuli zake mwaka 1917 za kibenki nchini,” amesema Mramba
Gwiji
wa soka kutoka klabu ya Liverpool, John Barnes akizungumza machache na
timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 15 (Serengeti Boys) kabla ya
kuelekea uwanjani kuwafunda kwa vitendo katika viwanja vya JK Youth
Park, Gerezani, jijini Dar es Salaam.
Aliongeza
kwamba takribani timu 32 zilishiriki kwenye mashindano ya awali ya
kutafuta mwakilishi wa Tanzania katika fainali zitakazofanyika kesho na
timu mbili kutoka Uganda na Kenya.
Mramba
alifafanua kwamba gwiji huyo wa soka aliyetamba miaka ya 1990 atakuwa
nchini kwa siku tatu na kushiriki kwenye program ya kuwafundisha vijana
wa umri chini ya miaka 15 kuwapa mbinu za soka tangu wakiwa vijana
wadogo.
Kwa
upande wake, Msemaji wa Shirikisho la soka nchini (TFF) Bw Alfred Lucas
amesema kwamba hii ni fursa adimu kwa vijana kupata nafasi ya
kufundishwa soka na mmoja wa magwiji wa soka wa dunia.
“hii
ni nafasi yao muhimu sana katika kujifunza mambo ya soka na kupanua
uelewa wao kuhusu mpira wa miguu wakiwa bado vijana wadogo kabisa maana
ni mastaa wa taifa wa baadaye,”
Gwiji
wa soka kutoka klabu ya Liverpool, John Barnes (kulia), Mkuu wa
Mahusiano na Masoko wa benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba (wa
pili kushoto) pamoja na Mkuu wa Idara ya Fedha wa Benki ya Standard
Chartered, Abdulrahaman Said (wa kwanza kushoto) wakionyeshana jambo
kwenye viwanja vya JK Youth Park vilivyopo Kidongo Chekundu, jijini Dar
es Salaam.
Aidha,
kocha wa timu ya Serengeti Boys, Kim Poulsen aliwashukuru benki ya
Standard Chartered kwa kufanikisha ujio wa gwiji hilo la soka kuja
kushiriki kwenye mazoezi na kutoa mchango wa mafunzo kwa vijana wake.
Aliongeza
kwamba ni muhimu kwa wadau wengine wa michezo kuiga mfano wa benki hiyo
na kuweza kuwaleta magwiji wa soka duniani kama chachu ya maendeleo ya
soka kwa nchini zinazoendelea kama Tanzania.
Gwiji
hilo la soka kutoka klabu ya Liverpool anatarajiwa kuondoka leo jioni
baada ya fainali hizo kwenye viwanja vya JK Youth Park mjini Dar es
Salaam.
Mkuu
wa kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered,
Juanita Mramba akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
wakati pia akimtambulisha gwiji wa soka kutoka klabu ya Liverpoool John
Barnes (hayupo) wakati wa kliniki fupi kwa timu ya taifa ya vijana chini
ya miaka 15 (Serengeti Boys) iliyoendeshwa na gwiji huyo katika viwanja
vya JK Youth Park vilivyopo Kidongo Chekundu, jijini Dar es Salaam.
Gwiji
wa soka kutoka klabu ya Liverpool, John Barnes akizungumza na
wanahabari (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa kuwawekea mazingira na
miundombinu ya kutosha watoto ili kuweza kuinua maendeleo ya soka
nchini.
Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Kim Poulsen akifafanua jambo kwa wanahabari (hawapo pichani) juu
ya umuhimu wa kuendelea kuweka mazingira mazuri kwenye soka la watoto
chini ya umri wa miaka 15 kama njia bora ya kukuza vipaji nchini wakati
wa kliniki fupi iliyoendeshwa na Gwiji wa Soka wa timu ya Liverpool,
John Barnes katika viwanja vya JK Youth Park vilivyopo Kidongo Chekundu, jijini Dar es Salaam.
Msemaji
wa TFF, Alfred Lucas akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujio wa
John Barnes na umuhimu wa kuinua vipaji kwa watoto chini ya miaka 15.
Pichani
juu na chini ni John Barnes akiwapa mbinu mbalimbali wakati wa mazoezi
kwa watoto chini ya umri wa miaka 15 (Serengeti Boys) baada ya kupata
fursa ya kuwepo nchini kushuhudia fainali za mashindano ya Kombe la
Standard Chartered 2017 safari ya kuelekea Anfield katika kuadhimisha
miaka 100 tangu benki ya hiyo kuanzishwa nchini yatakayofanyika leo
katika viwanja vya JK Youth Park jijini Dar es Salaam.
Timu
ya taifa ya vijana chini ya miaka 15 (Serengeti Boys) wakitoana jasho
baada ya kliniki fupi iliyoendeshwa na Gwiji wa soka wa timu ya
Liverpool, John Barnes (hayupo pichani) katika viwanja vya JK Youth
Park, jijini Dar es Salaam.
Gwiji
wa soka kutoka klabu ya Liverpool, John Barnes na Kocha Mkuu wa
Serengeti Boys, Kim Poulsen wakiwatazama timu ya taifa ya vijana chini
ya miaka 15 (Serengeti Boys) baada ya kliniki fupi iliyoendeshwa na
Gwiji huyo jana katika viwanja vya JK Youth Park jijini Dar es Salaam.
Gwiji
wa soka kutoka klabu ya Liverpool, John Barnes akibadilishana uzoefu na
Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Kim Poulsen (kushoto) wakati wa kliniki
fupi kwa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 15 (Serengeti Boys)
kwenye viwanja vya JK Youth Park jijini Dar es Salaam.
Gwiji
wa soka kutoka klabu ya Liverpool, John Barnes katika picha ya pamoja
na baadhi ya watoto wa wateja wa benki ya Standard Chartered waliopata
nafasi ya kukutana na gwiji huyo katika viwanja vya JK Youth Park.
COMMENTS