F RC MAKONDA AKABIDHI ORODHA YA MAJINA 97 YA WAUZA MADAWA YA KULEVYA KWA KAMISHNA MKUU WA MAMLAKA YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA JIJINI DAR LEO | RobertOkanda

Monday, February 13, 2017

RC MAKONDA AKABIDHI ORODHA YA MAJINA 97 YA WAUZA MADAWA YA KULEVYA KWA KAMISHNA MKUU WA MAMLAKA YA KUZUIA NA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA JIJINI DAR LEO

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akionyesha majina mengine 97 ya wauza Dawa za Kulevya awamu ya tatu kwa Bw. Rogers William Sianga Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya ili yaanze kushughulikiwa. RC Makonda amesema awamu hii itaitikisa nchi kwani wameanzia toka awamu ya pili iliyoongozwa na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi na kuendelea mpaka awamu ya sasa ya Rais Dkt John Pombe Magufuli, , Katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Kimataifa wa Julius Nyerere (JNCC).
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akikabidhi majina mengine 97 kwa kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa Bw. Rogers William Sianga, kuwa ili yaanze kushughulikiwa. RC Makonda amesema awamu hii itaitikisa nchi kwani wameanzia toka awamu ya pili iliyoongozwa na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi na kuendelea mpaka awamu ya sasa ya Rais Dkt John Pombe Magufuli.
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza katika mkutano huo, ambapo amekabidhi majina mengine 97 ya awamu ya tatu kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers William sianga ili yaanze kushughulikiwa. 
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza jambo na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Rogers William Sianga katika mkutano maalum wa kutoa tathmini ya kampeni ya kutokomeza biashara haramu ya madawa ya kulevya katika mkoa wa Dar es Salaam na nchi nzima kwa ujumla.
 
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Khaleed Mohammed almaarufu TID akitoa ushuhuda wa namna alivyokuwa akitumia Dawa za kulevya,na sasa amekiri hadharani kuacha kutumia na kuunga mkono juhudi za kupambana na Dawa za kulevya.
 
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro akizungumza wakati akitoa taarifa ya kampeni hiyo leo.
 

0 comments:

Post a Comment