Kamishna Mteule wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za kulevya,Rogers William akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa mazoez...
Kamishna
Mteule wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za kulevya,Rogers
William akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa mazoezi kwa wananchi
mkoa wa Kilimanjaro,uzinduzi uliofanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu cha
Ushirika Moshi.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
SIKU
chache baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt John Pombe Magufuli kuwa Kamishna wa mamlaka ya Kuzuia na Kupambana
na Dawa za Kulevya (Drug Control and enforcement Authority), Rogers
William ameanza kutema cheche dhidi ya Wafanyabiara na watumiaji wa dawa
za Kulevya.
Kamishna huyo ametangaza kushughulika kikamilifu na baadhi ya
wafanyabiashara mkoani Kilimanjaro,wanaowatumia wanawake wajasiriamali
wanaosafirisha mazao kwenda mikoani, kubeba Mirungi ama Bangi ndani ya
mizigo ya mazao.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro,Saidi Meck Sadiki akizungumza juu ya Dawa za
kulevya mara baada ya kumalizika uzinduzi rasmi wa siku ya mazoezi ikiwa
ni utekelezaji wa agizo la Makamu wa Rais ,Samia Suluhu Hassan.
William alitoa kauli hiyo wakati wa mazoezi katika uwanja wa Chuo kikuu
cha Ushirika Moshi (MoCU) baada ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro , Saidi
Mecky Sadiki kutoa nafasi kwa Mkuu huyo wa usalama wa taifa mkoa wa
Kilimanjaro , baada ya kumpongeza kwa kuteuliwa kwake.
“Tunayo
orodha ya wafanyabiashara wasio waaminifu na wengine wananchi wa
kawaida wanaowatumia wanawake wasio na hatia kusafirisha dawa za kulevya
kama Mirungi na Bangi kwenda mikoani….hilo nitahangaika nalo mara
nitakaporejea mkoani hapa katika mapambano dhidi ya vita hii”alisema
Sadiki.
Kauli ya William ilifuatia baada ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Saidi
Meck Sadiki kulitaka jeshi la Polisi kufaya uchungizi wa kina ili
kuwaachia baadhi ya wanawake watakaobainika kutokuwa na hatia ama
kufahamu kama walitumika kusafirisha dawa za kulevya bila ridhaa yao.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna msaidizi Mwandamizi wa
Polisi,Wilbroad Mutafungwa akitoa salamu za jeshi hilo katika uzinduzi
huo.
Akizungumzia
kuhusu Dawa za kulevya,Sadiki alisema vita dhidi ya dawa za kulevya za
aina mbalimbali kwa mkoa wa Kilimanjaro imeanza muda mrefu na tayari
zaidi ya watuhumiwa
689 wa dawa hizo wanashikiliwa katika kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Januari mwaka 2016 hadi Januari 2017.
Sadiki alisema vita hiyo ni ya kudumu yenye changamoto kubwa baada ya
mkoa wa Kilimanjaro kuwa na njia nyingi za Panya katika mipaka baina ya
Tanzania na Kenya, huku ikizingatiwa kwamba Kenya inalitumia zao la
Mirungi kama biashara halali.
“Watuhumiwa walikutwa na makosa 626 ambapo watuhumiwa 103 walifikishwa
mahakamani nakupata adhabu za aina mbalimbali ikiwamo vifungo na faini
ambapo wawili miongoni mwao walifungwa vifungo vya maisha gerezani na
kesi 136 zinaendelea mahakamani”alisema Sadiki.
Sadiki alisema kadhalika watuhumiwa wengine 296 walikamatwa na Tani nne
za Mirungi, watuhumiwa wengine 284 walikutwa na kilo 424 za bangi, huku
magari matano na pikipiki 20 zikishikiliwa na polisi kwa tuhuma za
kusafirisha dawa za kulenywa aina ya Mirungi na Bangi.
”Tumekuwa tukiendesha kampeni ya kukabiliana na dawa za kulevya kila
wakati na kampeni hii ni ya kudumu, nawaasa vijana kuachana na biashara
hiyo na badala yake watafute biashara halali”alisema Sadiki.
Aidha
mkuu wa mkoa aliwataka wafanyabiashara na watumiaji wa dawa za kulevya
wanaokimbia msako jijini Dar es salaam kutokimbilia mkoani mwake kwani
kampeni ni ile ile na watakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Viongozi
wa Serikali walioshiriki katika uzinduzi huo,kutoka kushoto ni Mkuu wa
wilaya ya Moshi,Kippi Warioba,Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Saidi Meck
Sadiki ,Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa na Katibu Tawala mkoa wa
Kilimanjaro, Mhandisi Aisha Amour.
Mwakilishi wa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi,Dkt Cyril Chami akitoa neno la ukaribisho katika uzinduzi huo.
Na
Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
SIKU
chache baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt
John Pombe Magufuli kuwa Kamishna wa mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za
Kulevya (Drug Control and enforcement Authority), Rogers William ameanza kutema
cheche dhidi ya Wafanyabiara na watumiaji wa dawa za Kulevya.
Kamishna huyo ametangaza kushughulika kikamilifu na baadhi ya
wafanyabiashara mkoani Kilimanjaro,wanaowatumia wanawake wajasiriamali
wanaosafirisha mazao kwenda mikoani, kubeba Mirungi ama Bangi ndani ya mizigo
ya mazao.
William alitoa kauli hiyo wakati wa mazoezi katika uwanja wa Chuo kikuu cha
Ushirika Moshi (MoCU) baada ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro , Saidi Mecky Sadiki
kutoa nafasi kwa Mkuu huyo wa usalama wa taifa mkoa wa Kilimanjaro , baada ya
kumpongeza kwa kuteuliwa kwake.
“Tunayo
orodha ya wafanyabiashara wasio waaminifu na wengine wananchi wa kawaida
wanaowatumia wanawake wasio na hatia kusafirisha dawa za kulevya kama Mirungi
na Bangi kwenda mikoani….hilo nitahangaika nalo mara nitakaporejea mkoani hapa
katika mapambano dhidi ya vita hii”alisema Sadiki.
Kauli ya William ilifuatia baada ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Saidi Meck
Sadiki kulitaka jeshi la Polisi kufaya uchungizi wa kina ili kuwaachia baadhi
ya wanawake watakaobainika kutokuwa na hatia ama kufahamu kama walitumika
kusafirisha dawa za kulevya bila ridhaa yao.
Akizungumzia
kuhusu Dawa za kulevya,Sadiki alisema vita dhidi ya dawa za kulevya za
aina mbalimbali kwa mkoa wa Kilimanjaro imeanza muda mrefu na tayari zaidi ya
watuhumiwa
689 wa dawa hizo wanashikiliwa katika kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Januari
mwaka 2016 hadi Januari 2017.
Sadiki alisema vita hiyo ni ya kudumu yenye changamoto kubwa baada ya mkoa wa
Kilimanjaro kuwa na njia nyingi za Panya katika mipaka baina ya Tanzania na
Kenya, huku ikizingatiwa kwamba Kenya inalitumia zao la Mirungi kama biashara
halali.
“Watuhumiwa walikutwa na makosa 626 ambapo watuhumiwa 103 walifikishwa
mahakamani nakupata adhabu za aina mbalimbali ikiwamo vifungo na faini ambapo
wawili miongoni mwao walifungwa vifungo vya maisha gerezani na kesi 136
zinaendelea mahakamani”alisema Sadiki.
Sadiki alisema kadhalika watuhumiwa wengine 296 walikamatwa na Tani nne za
Mirungi, watuhumiwa wengine 284 walikutwa na kilo 424 za bangi, huku magari
matano na pikipiki 20 zikishikiliwa na polisi kwa tuhuma za kusafirisha dawa za
kulenywa aina ya Mirungi na Bangi.
”Tumekuwa tukiendesha kampeni ya kukabiliana na dawa za kulevya kila wakati na
kampeni hii ni ya kudumu, nawaasa vijana kuachana na biashara hiyo na badala
yake watafute biashara halali”alisema Sadiki.
COMMENTS