MBUNGE wa Simanjiro, Mheshimiwa James Ole Millya ametoa pongezi kwa viongozi wa serikali ya awamu ya tano kwa jinsi wanavyojali na kuwahud...
MBUNGE wa
Simanjiro, Mheshimiwa James Ole Millya ametoa pongezi kwa viongozi wa serikali ya
awamu ya tano kwa jinsi wanavyojali na kuwahudumia wananchi.
Ametoa
pongezi hizo jana (Alhamisi, Februari 16, 2017) kwenye mikutano miwili ya
hadhara iliyofanyika Orkesumet na Mererani wilayani Simanjiro, Manyara, baada
ya kupewa nafasi asalimie wananchi kabla Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
hajazungumza na wakazi wa maeneo hayo.
“Serikali hii
ina viongozi wachapakazi akiwemo Waziri Mkuu. Kwa mara ya kwanza katika jimbo hili,
wananchi watapata maji safi kupitia mradi wa maji kutoka mto Ruvu unaoendelea
kujengwa hivi sasa,” alisema kwenye mkutano wa hadhara wa Orkesumet.
Alitumia
fursa hiyo kumuomba Waziri Mkuu afuatilie suala la ujenzi wa hospitali ya
wilaya kwani sasa hivi wanategemeakituo cha afya na hali ikibadlika inabidi
mgonjwa apeekewe Arusha mjini ambako ni umbali wa km. 150 kutoka Orkesumet
yalipo makao makuu ya wilaya hiyo.
Pia aliomba
ijengwe barabara ya lami ya kuunganisha wilaya hiyo pamoja wilaya jirani za Hai
na Kiteto.
Akiwa
Mererani, Bw. Ole Millya aliipongeza Serikali kwa kujenga barabra ya lami
kutoka uwanaja wa ndege wa KIA hadi Mererani. Hata hivyo, aliiomba serikali
iongeze juhudi ili barabara hiyo iweze Mererani na Orkesumet.
Akihibu hoja
hizo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alimpongeza mbunge huyo kwa uungwana wake wa
kutambua juhudi ambazo Serikali imezifanya kwa wananchi wa jimbo lake.
Waziri Mkuu ambaye
alikuwa katika siku ya pili ya ziara yake mkoani Manyara, aliwaambia wakazi hao
kwamba Serikali itaendelea kufanya nao kazi bila kumbagua mtu yeyote kwa sababu
ya itikadi za kisiasa.
“Mmempa yeye
dhamana ya kuwawakilisha kama mbunge wenu lakini dhamana ya kuongoza nchi
mmempa Mheshimiwa Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa kuwapigia kura. Kwa hiyo,
kazi yetu ni kuwatumikia ili tutatue kero zinazowakabili wana-Simanjiro,”
alisema.
Akizungumzia
sekta ya afya, Waziri Mkuu alisema kituo cha afya cha Orkesumet kimepokea sh. milioni
49 kati ya sh. milioni 57 zilizoombwa ili kukiimarisha katika utoaji wa huduma
za tiba.
“Tumeshatuma
fedha nyingine sh. milioni 163 kati ya sh. milioni 190 zilizoombwa ili
kununulia dawa, vifaa tiba na vitendanishi. Pia kun ash, milioni 483 zimetengwa
kwa ajili ya kuimarisha huduma za afya vijijini,” alisema.
“Nia yetu ni
kujenga hospitali kubwa ya wilaya lakini ni lazima tuimarishe miundombinu ya utoaji
tiba ili wananchi wapate huduma stahiki. Ombi la hospitali ya wilaya
nimelipokea na nitafuatilia kujua limefikia hatua gani,” alisema.
Kuhusu ujenzi wa barabara za
kuunganisha wilaya, Waziri Mkuu alisema Serikali itaanza kufanya upembuzi na
usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya kutoka Arusha – Kiteto – Kongwa
ili ijengwe kwa kiwango cha lami.
Kuhusu migogoro ya ardhi iliyotajwa
na wananchi kwenye mabango yao, Waziri Mkuu alimwagiza Mkuu wa wilaya ya
Simanjiro, Eng. Zephania Chaula aende na mbunge huyo kwenye maeneo
yanayolalamikiwa na wananchi ili akabaini chanzo cha migogoro na aitafutie
ufumbuzi.
Kuhusu umeme, Waziri Mkuu alisema
vijiji 18 katika ya 57 vya wilaya vimeshapatiwa umeme na vilivyoakia
vimeshaingizwa kwenye mpango wa serikali wa kuvipatia umeme vijiji 8,000.
Aliwaonya wakazi wa Mererani wachukue
tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwani takwimu zinaonyesha kuwa
kasi ya maambukizi katika mji huo iko asilimia 18 kiwango alichosema ni kikubwa
kuliko kiwango cha kitaifa.
IMETOLEWA
NA:
OFISI YA
WAZIRI MKUU,
IJUMAA,
FEBRUARI 17, 2017.
COMMENTS