HALMASHAURI NCHINI ZASHAURIWA KUACHANA NA MFUMO WA KUTUMIA WAZABUNI KATIKA KUKUSANYA USHURU MDOGOMDOGO.

Na: Frank Shija - MAELEZO Halmashauri nchini zimeshauriwa kupunguza mlolongo katika mchakato wa ukusanyaji wa ushuru mdogomdogo unaot...




Na: Frank Shija - MAELEZO
Halmashauri nchini zimeshauriwa kupunguza mlolongo katika mchakato wa ukusanyaji wa ushuru mdogomdogo unaotokana na kutumia mfumo wa kutumia wazabuni
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mhe. George Simbachawene akisisitiza jambo
badala yake kazi hiyo ifanywe na watendaji wa Halmashauri husika.


Ushauri huo umetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Boniphace Simbachawene katika mahojiano na mtangazaji wa Kituo cha luninga cha ITV kupitia kipindi cha Dakika 45 hivi karibuni.
Simbachawene alisema kuwa kumekuwa na kasumba ya Halmashauri nchini kutumia wazabuni katika ukusanyaji wa ushuru jambo linalochangia kusababisha mianya ya ubadhirifu wa fedha za umma.
“Mawakala wa ukusanyaji ushuru wamekuwa wadanganyifu na mara zingine wamekuwa wakiwasumbua wafanyabiashara ni vyema sasa Halmashauri nchini zikafikiria kutumia watendaji wake katika zoezi zima la ukusanyaji ushuru,” alisema Simbachawene.
Aliongeza kuwa sambamba na ukusanyaji wa ushuru kufanywa na watendaji wa Halmashauri husika aliagiza fedha hizo kuhifadhiwa katika akaunti za halmashauri hizo.
Katika hatua nyingine Waziri Simbachawene amewapongeza watumishi wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa utendaji wao ambapo amesema umeanza kutia faraja.
Hata hivyo alitoa rai kwa watumishi hao kuendelea kubadilika na anayeona hawezi kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano ni vyema akapisha ili Watanzania wengine waweze kuajiriwa.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: HALMASHAURI NCHINI ZASHAURIWA KUACHANA NA MFUMO WA KUTUMIA WAZABUNI KATIKA KUKUSANYA USHURU MDOGOMDOGO.
HALMASHAURI NCHINI ZASHAURIWA KUACHANA NA MFUMO WA KUTUMIA WAZABUNI KATIKA KUKUSANYA USHURU MDOGOMDOGO.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhjQTz5pv3Jdb2jf0P7J8VW9ZwNzjLdHhxDJ5DUVqeeC_5WoA_6h5NFNqJTP7TlANEvQzJBsxswVYnIDV016Yb6e29UdP6icgHiWbWx5rA8RTObEB3JgO-tDXpoq-4dTwiXpjHkKRli1l0/s640/George+Simbachawene.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhjQTz5pv3Jdb2jf0P7J8VW9ZwNzjLdHhxDJ5DUVqeeC_5WoA_6h5NFNqJTP7TlANEvQzJBsxswVYnIDV016Yb6e29UdP6icgHiWbWx5rA8RTObEB3JgO-tDXpoq-4dTwiXpjHkKRli1l0/s72-c/George+Simbachawene.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/02/halmashauri-nchini-zashauriwa-kuachana.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/02/halmashauri-nchini-zashauriwa-kuachana.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy