DIWANI KATA YA BUGURUNI MHE. ADAM AWAAGIZA VIONGOZI WA KUWAKAMATA NA KUWACHUKULIA HATUA WANANCHI WASIOFANYA USAFI.

Diwani wa Kata ya Buguruni,Adamu Fugame (Cuf) akishirikiana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Msongela Palela na Katibu Ta...



Diwani wa Kata ya Buguruni,Adamu Fugame (Cuf) akishirikiana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Msongela Palela na Katibu Tawala wa wilaya hiyo,Edward Mpogolo (kulia) wakifanya usafi katika maeneo ya buguruni kwa malapa kutimiza kauli ya Rais Dk.John Magufuli ya kufanya usafi kila mwisho wa wiki ya mwezi jijini Dar es Salaam juzi. (PICHA NA ELISA SHUNDA)


Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala,Msongela Palela akizungumza na wananchi wa eneo la Buguruni kwa Malapa na Darajani kuhusu kufanya usafi katika maeneo yanayowazunguka ili kujikinga na kujiepusha na magonjwa ya milipuko kama Kipindupindu baada ya kufanya usafi kutekeleza agizo la Rais Dk.John Magufuli ya kufanya usafi kila mwisho wa wiki ya mwezi jijini Dar es Salaam juzi. Kulia ni Diwani wa Kata ya Buguruni,Adamu Fugame (Cuf) na Katibu tawala wa wilaya hiyo, Edward Mpogolo.
 

NA EMERISIANA ATHANAS
DIWANI wa Kata ya Buguruni wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Adam Fugame ameagiza viongozi wa kata akiwemo Ofisa Afya, kuwakamata na kuwachukulia hatua watu wasiofanya usafi au kuchangia kwaajili yakuzolewa uchafu.

Akizungumza jijini hapa jana, wakati wa zoezi la ufanyaji usafi ulioshirikisha viongozi mbalimbali wa Manispaa ya Ilala akiwemo Mkurugenzi Msongela Palela, alisema ni vema viongozi wakafanya kazi kwa mujibu wa sheria ili kuwashughulikia watu hao.

"Suala hili sio rai bali tufanye kama sheria ili kufanikisha zoezi la kuimarisha usafi katika maeneo yetu, kwani tusipofanya hivi hakuna litakalotekelezwa, watu hawafanyi usafi," alisema.

Kutokana na umuhimu wa kufanya usafi alisema ni vema watakaokutwa hawachangii wala kujishughulisha na kufanya usafi wakachukuliwa hatua na kutozwa fedha.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Palale alisema kuwa katika kata tisa zilizoko katika manispaa hiyo kata ya Buguruni ndiyo imekuwa na ugonjwa wa kipindu pindu ambacho husababishwa na hali ya uchafu.

Alitumia nafasi hiyo kuwataka wakazi wa kata ya Buguruni kuhakikisha wanafanya usafi na kuwa walinzi katika kuhakikisha wanalinda mazingira na kuimarisha usafi kwenye maeneo yao.
 
Imeandaliwa na Mtandao wa WWW.ELISASHUNDA.BLOGSPOT.COM/0719976633

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: DIWANI KATA YA BUGURUNI MHE. ADAM AWAAGIZA VIONGOZI WA KUWAKAMATA NA KUWACHUKULIA HATUA WANANCHI WASIOFANYA USAFI.
DIWANI KATA YA BUGURUNI MHE. ADAM AWAAGIZA VIONGOZI WA KUWAKAMATA NA KUWACHUKULIA HATUA WANANCHI WASIOFANYA USAFI.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjc-wHQBsc41yLiWABtsXfystk8L2vCWsW5eB2rSpflyF82g2IuaUQHedTd5zzPTrIdjA7yJFoNA8JGtiSI7d4Ph01nex7x_fy8PmNP4h76AG74G_qqQ4dE3Cw-JUHavwU56ZZYjXlw5BY/s640/DSC_0162.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjc-wHQBsc41yLiWABtsXfystk8L2vCWsW5eB2rSpflyF82g2IuaUQHedTd5zzPTrIdjA7yJFoNA8JGtiSI7d4Ph01nex7x_fy8PmNP4h76AG74G_qqQ4dE3Cw-JUHavwU56ZZYjXlw5BY/s72-c/DSC_0162.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2017/02/diwani-kata-ya-buguruni-mhe-adam.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/02/diwani-kata-ya-buguruni-mhe-adam.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy