Kaimu Kamishna wa Nishati na Madini, Ally Samaje (anayetoa maelezo) akielezea Mpango wa Serekali wakati wa kufunga Mgodi wa Buzwagi. Wen...
Kaimu
Kamishna wa Nishati na Madini, Ally Samaje (anayetoa maelezo) akielezea
Mpango wa Serekali wakati wa kufunga Mgodi wa Buzwagi. Wengine katika
picha ni Wabunge kutoka Kamati ya Kudumu ya Nishati na Madini, Watumishi
wa Wizara ya Nishati na Madini na Viongozi Waandamizi kutoka Mgodi wa
Buzwagi.
Na Rhoda James – Kahama.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa ameuongoza
ujumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Wizara ya Nishati na Madini ili
kukagua na kuhoji utendaji na ushiriki wa mgodi wa Buzwagi katika
masuala ya kijamii mkoani Shinyanga hivi karibuni.
Katika
ziara hiyo, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeutaka
Uongozi wa Mgodi wa Buzwagi kuwashirikisha wananchi pamoja na
wafanyakazi wa Mgodi huo Mpango wa kuufunga Mgodi huo (Mining Closure
plan) unaotarajia kufunga shughuli zake za uzalishaji wa Dhahabu ifikapo
Desemba 2017, huku shughuli za uchejuaji zitaendelea kwa miaka miwili.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Nishati na Madini, Doto Mashaka Biteko (wa pili
kushoto) akimsikiliza Meneja wa Mgodi wa Buzwagi, Assa Mwaipopo (hayupo
pichani) akielezea shughuli za uzalishaji wa Dhahabu katika Mgodi huo.
Kushoto kwake ni Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally Samaje na
wengine ni wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Nishati na Madini,
Watumishi kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Wafanyakazi wa Mgodi wa
Buzwagi.
Haja
hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Nishati na Madini,
Doto Mashaka Biteko mara baada ya kuwasili na kukutana na uongozi wa
mgodi huo wakati wa ziara hiyo ya ukaguzi wa mgodi huo.
Biteko
alisema kuwa Wananchi na wafanyakazi lazima wawe sehemu ya ufungaji wa
Mgodi huo kwa kuwa jambo hilo ni kubwa kwani litatikisa Uchumi wa
wananchi wa Kahama na pia Halmashauri ya Kahama itakosa Ushuru wa Huduma
ambazo Mgodi huo umekuwa ukilipa kila mwaka.
“Mgodi
huo unalipa Ushuru wa Huduma kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kahama na
wafanyakazi katika mgodi huo wana ajira kwa hiyo mipango ya kufunga
mgodi huo iwe sehemu ya wananchi kwa asilimia mia” alisisitiza Biteko.
Muonekano wa Mgodi wa Buzwagi katika Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.
Aidha
Biteko alitaka ufafanuzi zaidi kutoka kwa Uongozi wa Mgodi huo ni sababu
zipi zinazopelekea mgodi huo kufungwa. Vilevile, alitaka Uongozi
kuijulisha kamati hiyo jambo ambalo mgodi huo unawaachia wanannchi wa
Kahama mara baada ya shughuli za uzalishaji kufungwa.
Akijibu
hoja hizo Meneja wa Mgodi wa Buzwagi, Assa Mwaipopo alisema kuwa
Serikali na wananchi wamekuwa wakishirikishwa kikamilifukakita shughuli
mbalimbali za mgodi huo ikiwemo kuhusu nini kifanyike baada ya kufunga
mgodi. Alieleza kuwa, Mgodi na Serikali wanansubiri maoni ya wananchi
kuhsu shughuli sahihi za kufanya katika eneo hilo la mgodi mara tu
utakapomaliza shughuli zake.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Nishati na Madini, Doto Mashaka Biteko (wa pili
kulia) akiwa na wanakamati wezake wakiongozana na Viongozi Waandamizi
kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Mgodi wa Buzwagi mara tu baada ya
kuwasili katika Mgodi huo.
Mwaipopo
alifafanua kuwa ingawa mgodi umekuwa ukipata faida kutokana na
shughuliza uchimbaji dhahabu bado mgodi hsujarudisha gharama za awali
ambazo zilitumika wakati wa uwekezaji huo.
Akijibu
swali la mjumbe mwingine wa kamati ya Bunge aliyehoji juu ya malalamiko
ya wafanyakazi wa mgodi huo kutokujua mwajiri wao kwa kuwa mikataba yao
inaonesha ni kati yao na Pangea Mining Gold, vitabulisho vyao vinatoka
African Barrick Gold Mine na malipo yao yanaonesha yanalipwa na Acacia
Mining Gold. Mwaipopo alisema kuwa mmiliki wa Mgodi huo ni Pangea na
ndiye anayewajibika na huyo ndiye mwaajiri wao.
Aidha
Kamati ya Kudumu ya Wizara ya Nishati na Madini iliitaka Wizara kutoa
ufafanuzi wake ni kwa nini Mgodi wa Buzwagi unaendelea kubadili majina
kama vile Pangea, African Gold Mine na Acacia Gold Mine.
Akitoa
ufafanui wa suala hilo, Kaimu Kamishna wa Madini, Ally Samaje alisema
kuwa mgodi unapobadili jina au anwani basi haina madhara lakini pale
unapobadili umiliki wake, lazima mchakato huo wote ushirikishe serikali
na upate ridhaa ya serikali kwa kuwa hapo kuna ulipaji wa Kodi na Mapato
mbalimbali kwa serikali.
Ziara
hii ni wiki moja inayowawezesha wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Wizara ya
Nishati na Madini kukagua na kuhakikisha wizara wanazozisimamia
zinatekeleza majukumu yao kama inavyowapasa.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Ntalikwa (katikati)
akiwa anafanya majadiliano na Kaimu Kamishna wa Madini, Ally Samaje na
Mbuge wa Kahama Jumanne Kishimba Mara baada ya kutembelea mgodi wa
Buzwagi.
Wataalamu kutoka Idara ya Madini wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutoka katika eneo la uzalishaji wa Dhahabu.
Kotena iliyofanyiwa maandalizi tayari kupokea makinikia ya Shaba ambayo yanachimbwa kwa asilimia kubwa katika Mgodi wa Buzwagi.
Kotena ambayo tayari imejazwa na makinikia ya Shaba tayari kwa ajili ya kufunga ili kusafirishwa nje.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Ntalikwa (wa pili
kushoto) akimsikiliza Kaimu Kamishna wa Madini Mhandisi Ally Samaje,
kabla ya kusikiliza mada kutoka kwa Meneja wa Buzwagi.
COMMENTS