Ikiwa wateja mbalimbali wa Vodacom Tanzania wakiendelea kunufaika na bonasi za M-PESA zinazotolewa na kampuni hiyo, Kumetokea na mat...
Ikiwa wateja mbalimbali wa Vodacom Tanzania wakiendelea kunufaika na bonasi za M-PESA zinazotolewa na kampuni hiyo, Kumetokea na matapeli wakiwalaghai wateja wa kampuni hiyo kana kwamba ni washindi wa bonasi hizo zinazoendelea kutolewa.Vodacom Tanzania imetoa tahadhari kwa wateja wake wote popote walipo nchini kuwa macho na matapeli ambao wanajifanya ni wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa kuwapigia simu na kuwafahamisha kuwa wamefanikiwa kupata mgao wa fedha za gawio la huduma ya M-Pesa uliotangazwa na kampuni mapema wiki hii.”KAMA WANAVYOSIKIKA KWENYE SAUTI HIYO”
Akiongea na Mtandao huu,Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Jacqueline Materu alisema“Natoa
wito kwa wateja
wetu kuwa makini na matapeli wanaowapigia simu na kuwafahamisha kuwa
wameshinda fedha za bonasi ya M-Pesa.Vodacom Tanzania haina utaratibu wa
kuwapigia simu wateja kuhusiana na mgao wa fedha hizi bali inatoa mgao
kwa kadri ya mteja alivyotumia huduma hii
na rekodi zote za matumizi kampuni inazo. Wanaowapigia simu wateja ni
matapeli ambao wanataka kupata namba zenu za siri na kuwatajia kiasi
gani cha fedha mlizonazo ili wapate frusa ya kuwaibia fedha na msitoe
namba za siri kwa mtu yeyote”.
Wateja
watakaonufaika na mgao wa fedha za bonasi ya M-pesa awamu hii
wanawekewa fedha zao kwenye akaunti
zao za M-Pesa moja kwa moja na utaratibu wa kuwapigia wateja simu huwa
unatumika kwenye promosheni tu kama vile promosheni inayoendelea
ya”Nogesha Upendo”.
COMMENTS