Msimamizi wa Biashara wa Kampuni ya Simu Tigo Dar es Salaam na Zanzibar, Nderingo Materu (wa pili kushoto), akikata utepe kuashir...
Msimamizi wa Biashara wa Kampuni ya Simu Tigo Dar es Salaam na Zanzibar, Nderingo Materu (wa pili kushoto), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka dogo la Tigo Tandika Devis Corner leo. Kutoka kulia ni Meneja Mauzo wa Tigo Wilaya ya Temeke, Fadhila Saidi, Mwendeshaji wa duka hilo, Khadija Matambo na kushoto ni Meneja Huduma kwa Wateja wa kampuni hiyo, Isack Shoo.
Hawa ndio waendeshaji wa duka hilo. Kutoka kushoto ni Victor Juma, David Ngwale na kiongozi wao Khadija Matambo.
Meneja wa Tigo Uendeshaji wa huduma za Wateja, Isaack Shoo akihojiwa na wanahabari.
Picha ya pamoja.
Picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa duka hilo.
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI ya Tigo inayoongoza kwa maisha ya kidijitali Tanzania, leo imezindua rasmi mpangbo mdogo wa maduka ya huduma kwa wateja unaofahamika kama maduka ya Team Leaders ambayo yatatoa huduma za kampuni moja kwa moja kutoka maeneo wanayokaa wateja.
Kwa mujibu wa Meneja wa Tigo Uendeshaji wa huduma za Wateja , Isaack Shoo maduka hayo kimsingi yatakuwepo katika maeneo ya makazi na yatatoa huduma zote za Tigo na miongoni mwake ni pamoja na kurudisha kadi za simu zilizopotea, mauzo ya muda wa maongezi, huduma za Tigo Pesa, mauzo ya kadi za Tigo na mauzo ya simu za kisasa (Smartphones).
Katika mkutano huo wa waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam leo Shoo alisema, “Kupitia maduka ya team leaders Tigo imejikita kuhakikisha kuwa bidhaa zakehuduma zake zimo karibu na wateja, kuwezesha wateja wetu kufurahia huduma namba moja ambayo imo moja kwa moja katika kujikita kwetu katika mabadiliko ya kuboresha mtindo wa maisha ya kidijitali.”
Shoo alisema kuwa kila duka litakuwa na mawakala watano wa huduma kwa mteja ambao watakuwa wamepata mafunzo yanayohusiana na huduma kwa mteja kutoka Tigo ili kukidhi mahitaji ya wateja.
Aliongeza kuwa hadi sasa maduka yapo maduka matano ambayo yapo Mbande, Tandika, Tabata, Segerea na Ukonga (yote yapo Dar es Salaam) na tayari yanafanya kazi.
Shoo aliongeza, “Maduka zaidi yanatarajiwa kuanzishwa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ambapo yatakuwa katika maeneo ya Kawe, Mawasiliano Towers, Kimara, Kigogo na Mwananyamala.”
Mbali na mafunzo Tigo pia itatoa vifaa muhimu kwa ajili ya biashara kwa mawakala wake katika hatua ya mwanzo ya kuanzisha biashara katika maduka, jambo ambalo ni muhimu na linalothibbitisha kujikita kwa kampuni hiyo ya simu katika kuisaidia serikali kstiks juhudi zake za kiupunguza ukosefu wa ajira nchini.
Hivi sasa Tigo ina maduka maduka makubwa 50 kwa ajili ya huduma kwa wateja yaliyoasambaa kote nchini yakiwa na uwezo wa kuhudumia wateja kati ya 200 na 300 kwa siku.
COMMENTS