MASAUNI AFANYA ZIARA NIDA ZANZIBAR, ATEMBELEA WAGONJWA NA KUFANYA USAFI HOSPITALI YA MNAZI MMOJA

  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimkabidhi Kitambulisho cha Taifa cha Wageni, Leonie Schol...






 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimkabidhi Kitambulisho cha Taifa cha Wageni, Leonie Schollmeyer (kulia), wakati kiongozi huyo alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Zanzibar leo. Masauni licha ya kupewa elimu kuhusiana na utendaji wa kazi wa ofisi hiyo, pia alizungumza na watumishi wa Mamlaka hiyo na kuwataka kufanya kazi kwa weledi kwa kuwahudumia wananchi ili kuiletea mamlaka hiyo mafanikio zaidi. 
 
 
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akifanya usafi na wanachama wa Baraza la Vijana Shehia ya Miembeni katika Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar. Masauni alialikwa na Baraza hilo kushiriki kufanya usafi nao na baadaye aliwatembelea wagonjwa wa hospitali hiyo akiwa na Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mgeni Hassan Juma (hayupo pichani) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Marina Joel Thomas (hayupo pichani).  
 
 
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Watumishi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Zanzibar wakati kiongozi huyo alipofanya ziara ya kikazi ya kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka hiyo. Masauni licha ya kupewa elimu kuhusiana na utendaji wa kazi wa ofisi hiyo, pia alizungumza na watumishi wa Mamlaka hiyo na kuwataka kufanya kazi kwa weledi kwa kuwahudumia wananchi ili kuiletea mamlaka hiyo mafanikio zaidi. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo, Zanzibar, Hassan Haji Hassan.
 
 
 
 Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mgeni Hassan Juma (kushoto), Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa kofia) wakimsikiliza Nesi Msaidizi Mkuu wa Wodi ya Upasuaji wa Uti wa Mgongo na Kichwa katika Hopsitali ya Mnazi Mmoja, Hadia Mmadi, wakati alipokuwa anawafafanulia kuhusu wagonjwa wanavyopasuliwa. Viongozi hao walifanya ziara katika eneo hilo, mara baada ya kufanya usafi mazingira mbalimbali ya hospitalini hapo.
 
 
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (watatu kushoto mstari wa mbele), Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Zanzibar, Hassan Haji Hassan (watatu kulia)  wakiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Mamlaka hiyo, mara baada ya Masauni kumaliza ziara yake ya kikazi kuitembelea Mamlaka hiyo.
 
 
 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa kofia) akiwa katika picha ya pamoja na Wanachama wa Baraza la Vijana Shehia ya Miembeni, Kikwajuni, Zanzibar, mara baada ya kumaliza kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Hospitali ya Mnazi Mmoja. Vijana hao walimwalika Mbunge wao ili wajumuike naye katika kuweka safi zaidi mazingira ya Hospitali hiyo.  (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MASAUNI AFANYA ZIARA NIDA ZANZIBAR, ATEMBELEA WAGONJWA NA KUFANYA USAFI HOSPITALI YA MNAZI MMOJA
MASAUNI AFANYA ZIARA NIDA ZANZIBAR, ATEMBELEA WAGONJWA NA KUFANYA USAFI HOSPITALI YA MNAZI MMOJA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi3EVGJrJFlQN7GOWZ29Hj-pe9BLBtAphs6ngfBCAxzRRwzqF0Xw7KmF80UGuAwTMqSb64YPHMbuqEEhR0zNnJdB5ThtV6OMo1JNxxHdtaH6UKu2liPj8p5aaGgjqr0ldEnVueSUfHpvn73/s640/PIX+01.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi3EVGJrJFlQN7GOWZ29Hj-pe9BLBtAphs6ngfBCAxzRRwzqF0Xw7KmF80UGuAwTMqSb64YPHMbuqEEhR0zNnJdB5ThtV6OMo1JNxxHdtaH6UKu2liPj8p5aaGgjqr0ldEnVueSUfHpvn73/s72-c/PIX+01.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2016/12/masauni-afanya-ziara-nida-zanzibar.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/12/masauni-afanya-ziara-nida-zanzibar.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy