Mkuu wa Wilaya Mh. Godwin Gondwe akizungumza na wannchi wa kijiji cha Chogo wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji ...
Mkuu wa Wilaya Mh. Godwin Gondwe akizungumza na wannchi wa kijiji cha Chogo wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji Bw. William Makufwe akifutiwa na Mh.Aabdalla Pendeza Diwani wa Kata ya Kabuku Ndani na wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa kijiji cha chogo.
Mkuu wa Wilaya ,Mkurugenzi Mtendaji na viongozi wengine kutoka
Halmashauri wakitazama moja ya eneo laKitalu cha kuoteshea miti ya
malimao mkulima baada ya kupitia shamba na kuona uharibifu uliofanyika.
Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya handeni akizungumza na wananchi wa kijiji cha Chogo kata ya Kabuku Ndani.
Mmoja kati ya wafugaji waliopo katika kijiji cha ChogoBw. Masanja
akifafanua jambo kwa Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi na wananchi wote kwa
ujumla.
====== ======= ======== Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe na Mkurugnzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe wamepiga marufuku ufugaji holela. Tamko hilo limetolewa baada ya uongozi wa kijiji cha Chogo Kata ya Kabuku Ndani kuomba Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji kuwasaidia kuondoa wafugaji waliovamia katika kijiji chao na kuharibu mazao ya kilimo ya wananchi wa kijiji hicho.
====== ======= ======== Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe na Mkurugnzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe wamepiga marufuku ufugaji holela. Tamko hilo limetolewa baada ya uongozi wa kijiji cha Chogo Kata ya Kabuku Ndani kuomba Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji kuwasaidia kuondoa wafugaji waliovamia katika kijiji chao na kuharibu mazao ya kilimo ya wananchi wa kijiji hicho.
Akizungumza na wananchi hao Mkuu wa wilaya aliwaeleza wananchi
kuwa kila sehemu kuna taratibu na sheria zake namna ya kuishi. “ni marufuku kuchunga mifugo kwenye maeneo
ya hifadhi ya misitu ya Serikali au ya Kijiji kwa maana ni kosa akipatikana mtu wa namna hiyo kamateni
peleka polisi na mimi nifahamu”alisema, na pia ni marufuku kuchukua mifugo
kwenda kuchunga kwenye shamba la
mwenzako kuwepo na mazao au hakuna ni kosa kamateni mtu wa namna hiyo peleka polisi, hata kama mwenye shamba
amekwisha vuna isipokuwa kwa idhini ya mwenye shamba pekeyake.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni aliwaeleza
wananchi kwamba ulinzi wa mali za
Chogo ni wanachogo wenyewe, na mgogoro
wa wakulima na wafugaji ni wetu sote, Aliwaeleza kwamba walishindwa kuchukua
tahadhari mapema pindi wafugaji hao walipoingia miezi mine iliyopita kwa sababu
eneo lao lina mpango bora wa matumizi ya ardhi.
Aidha aliwaeleza wananchi kuwa,
amewataka Watendaji wa Kata na Vijiji
kuleta orodha ya mifugo iliyopo kwenye maeneo yao na waeleze uwezo wa ardhi
iliyopo kuweza kuhimili idadi ya mifugo iliyopo kwa mujibu wa mpango wa ardhi
uliowekwa katika maeneo yao ili kugungua kama kunamifugo imezidi au haijazidi, “Tarehe 29/10/2016 nitapata orodha ya
Halmashauri nzima kwa kata 21 na Vijiji
91” alisema.
Mfugaji wa mwanzo ambae atakuwepo katika kijiji husika kwa
kumkaribisha ama la kama idadi ya mifugo aliyokuwa nayo inakidhi viwango
atabaki, lakini kwa mfugaji atakaye zidisha kiwango cha mifugo basi ataondolewa
ili aende kutafuta mahali kwingine na
marufuku kukaribisha mfugaji mwingine alisema Mkurugenzi.
Mwenyekiti wa kijiji cha Chogo aliwaeleza viongozi kuwa wafugaji
hao waliingia kwenye maeneo yao bila kufuata utaratibu, wameleta uharibifu wa
mazao napindi wanapohitajika kwenye vikao ili wapewe utaratibu wanakaidi
kufika. Alieleza kuwa eneo ambalo limetengwa kaajili ya mifugo lipo eneo la
Chang’ombe na kwa mujibu wa idadi ya mifugo iliyopo tayari imejitosheleza.
Mifugo iliyovamia ni zaidi ya 4000 na kwamba ardhi ya kijiji haiwezi kutunza
idadi kubwa ya mifugo.
Bw. Said Mmbelwa mwanakijiji wa Chogo kitongoji cha Kibamba
aliwaeleza wananchi wenzake kuwa walifanya makosa kuwakaribisha wafugaji hao
bila kufuata utaratibu na kwamba kama wananchi weneyewe wasipobadilika basi
migogoro ya wakulima na wafugaji haitakwisha.
Aidha Diwani wa kabuki ndani
Mh. Abdallah Pendeza aliwashukuru Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji
na Kuwataka wananchi kutekeleza yale ambayo viongozi wamewaelekeza kwa
kushirikiana, kwamba kila mmoja atimize wajibu wake kulingana na sheria,
taratibu na kanuni.
Mkuu wa Wilaya aliwataka viongozi wa vijiji kuhuisha kamati za
ulinzi na usalama na kuhakikisha wanaripoti kwenye vyombo vya sheria pindi
wanapoona kunamtu ameingia kwenye maeneo yao haeleweki ili kulinda amani.
Imetolewa na
Alda Sadango
Afisa Habari
Halamshauri ya Wilaya Handeni
COMMENTS