RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA MRADI WA UJENZI WA HOSTELI ZA WANAFUNZI WA UDSM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kabla ya kuweka jiwe la msingi katika mradi ...







Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kabla ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Hosteli za Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi watatu kutoka (kulia), Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojiana Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako (wanne kulia), Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (wa tatu kushoto), Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Rwekaza Mukandara (wa nne kushoto), Mtendaji mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch. Elius Mwakalinga wakwanza (kulia) Pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Joseph Nyamhanga wa (kushoto). 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Hosteli za Wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Elimu, Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandara. Hosteli hizo zitakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 3840 na ujenzi wake umefikia asilimia 75 na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia kabla ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa hosteli za wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandara mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Hosteli hizo za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. 
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania TBA Arch. Elius Mwakalinga akitoa ufafanuzi kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu ujenzi wa Hosteli hizo za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga tumba katika bendi ya Msondo Ngoma mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Hosteli za wanafunzi katika chuo kikuu cha Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mke wake Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojiana Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandara wakipiga makofi wakati brass bendi ya JKT ilipokuwa ikitumbuiza mara baada ya kukamilika kwa tukio la kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Hosteli za wanafunzi katika chuo kikuu cha Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono wakati akiwasili katika viwanja vya hosteli mpya za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. 


Taaswira ya moja ya moja ya hosteli hizo za wanafunzi ambazo ujenzi wake umefikia asilimia 75 na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu. (PICHA NA IKULU)
**************
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULUDescription: Description: Description: Description: Description: Coat of Arms
Simu: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz               

Faksi: 255-22-2113425


OFISI YA RAIS,
     IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,   
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 21 Oktoba, 2016 ameweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa mabweni 20 ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 3,840 ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa Mwezi Juni mwaka huu wakati wa sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa maktaba ya kisasa ya chuo hicho.
Wakati Rais Magufuli akiweka jiwe la msingi la mradi huo, tayari ujenzi umefikia asilimia 75 ambapo majengo 20 yaliyounganishwa kimuundo yamefikia ghorofa ya nne na ujenzi huo unaofanywa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) unatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 30 Desemba, 2016.
Akizungumza kabla ya kuweka jiwe la msingi Rais Magufuli aliyeambatana na Mkewe Mama Janeth Magufuli ameipongeza TBA na wadau wote wanaoshiriki katika ujenzi huo zikiwemo Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa hatua kubwa ya ujenzi iliyofikiwa tangu ujenzi uanze tarehe 01 Julai, 2016 na amebainisha kuwa kwa kutumia TBA mradi huo utatumia kiasi kidogo cha fedha.
"Nawapongeza sana TBA kwa kazi nzuri mliyoifanya mpaka sasa, mradi huu utatumia Shilingi Bilioni 10 tu, Wakandarasi kutoka nje walitaka kujenga mabweni haya ya wanafunzi kwa Shilingi Bilioni 100, sasa mtaona wenyewe tumeokoa Shilingi ngapi" amesema Rais Magufuli.
Aidha, Rais Magufuli ameahidi kuwa, kwa kuwa majengo hayo yanauwezo wa kubeba ghorofa sita, Serikali itafanya utaratibu wa kutumia moja ya likizo za wanafunzi kuongeza ghorofa nyingine mbili ili kuwawezesha wanafunzi wengi zaidi kupata nafasi.
Kuhusu mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu Dkt. Magufuli amesema Serikali imetenga Shilingi Bilioni 483 kwa mwaka huu ambapo wanafunzi takribani 93,000 wanaoendelea na masomo na wanafunzi takribani 25,000 watakaoanza masomo watapatiwa mikopo lakini ameweka bayana kuwa mikopo hiyo itatolewa kwa wanafunzi ambao wanatoka kwenye familia masikini.
Rais Magufuli ameiagiza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kurekebisha dosari zilizopo katika mfumo wa utoaji wa mikopo ikiwa ni pamoja na upangaji mbaya wa wanafunzi katika vyuo, kutoa mikopo kwa upendeleo, kutozingatia sifa za mkopaji, kutoa mikopo hewa na kufungua vyuo kabla ya mikopo ya wanafunzi kutolewa na pia amewaonya wanafunzi kujiepusha na vitendo visivyofaa wakati Serikali inarekebisha dosari hizo.
"Na ndio maana wakati mwingine na wabaya wanapitia humo humo, mara fanye hivi fanyeni vile, wakati wanajua kuwa mkifanya yasiyofaa Serikali itawafukuza tu ili mkafanyie mambo yenu huko.
"Kwa sababu huwezi kuwa unahangaika kutafuta fedha za kuwapa mikopo, wakati huo huo unahitaji kujenga reli, wakati huo huo unahitaji kujenga barabara, wakati huo huo unahitaji kulipa mishahara, wakati huo huo unahitaji kutoa elimu bure, wakati huo huo Karagwe kuna njaa, wakati huo huo watu wanahitaji dawa hospitali, halafu watu wengine wanataka kukuendesha kana kwamba hela unayokusanya ni kwa ajili yao tu, ni lazima tuelewane na mimi ninataka kuwaeleza kwa dhati lazima twende katika njia iliyonyooka, ni bora uwe Rais usiye maarufu lakini utimize uliyoyaahidi, asitokee mtu wa kukuendesha, ninajua mmenielewa" amesisitiza Dkt. Magufuli.
Dkt. Magufuli ameiagiza Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) kujipanga vizuri kukusanya marejesho ya mikopo kwa wote waliokopeshwa na bodi hiyo ambapo mpaka sasa bodi inadai takribani Shilingi Trilioni 2.6.
Awali akitoa taarifa ya mradi huo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof. Rwekaza Mukandala amesema wakati ujenzi huo ukiendelea chuo kimetenga Shilingi Bilioni 4.5 kutoka kwenye mapato yake kwa ajili ya kununua samani ikiwa ni pamoja na vitanda vya wanafunzi na pia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia itashughulikia ujenzi wa uzio, jiko na bwalo la chakula.
Hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Wabunge, Makatibu Wakuu na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Paul Makonda.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
21 Oktoba, 2016

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA MRADI WA UJENZI WA HOSTELI ZA WANAFUNZI WA UDSM
RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA MRADI WA UJENZI WA HOSTELI ZA WANAFUNZI WA UDSM
https://i.ytimg.com/vi/f82zOEnld4c/hqdefault.jpg
https://i.ytimg.com/vi/f82zOEnld4c/default.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2016/10/rais-dkt-magufuli-aweka-jiwe-la-msingi.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/10/rais-dkt-magufuli-aweka-jiwe-la-msingi.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy