VURUGU kubwa zimeibuka baina ya Mkuu wa Mkoa Arusha Mrisho Gambo na mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema katika hafla y...
VURUGU
kubwa zimeibuka baina ya Mkuu wa Mkoa Arusha Mrisho Gambo na
mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema katika hafla ya uwekaji wa
jiwe la msingi katika hospitali ya mama na mtoto inayojengwa eneo ya Buruka nje kidogo ya jiji la Arusha.
Vurugu
hiyo zimeibuka baada ya mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kuvuruga
ratiba iliyokuwa imepagwa na waandaaji wa hafla hiyo ambapo kwa mujibu
wa ratiba hiyo ilikuwa imepagwa kuwa hotuba ya mkuu wa mkoa
ingetanguliwa na waandaji wa shughuli hiyo akiwemo waandaji wa hafla
hiyo, wafadhili pamoja na Mbunge Lema.
Kabla
ya vurugu hizo mkuu wa Mkoa wa Arusha alikaribishwa na mkuu wa wilaya ya
Arumeru, Alexzanda Mnyeti swala ambalo liliibua mzozo mkubwa kwa
wananchi walikuwa wamefika kushuudia tukio hilo la uzinduzi wakiwemo
wafadhili waliofadhili mradi ambao ni shirika la kuhudumia afya ya mama
na mtoto (Maternity Afrika ).
Baada
ya kuanza kuhutubia mkuu huyo wa mkoa akielezea historia ya mradi huo
ikiwepo upatikanaji wa eneo la kujenga mradi wa hospitali hiyo ghafla
mbunge Lema alisimama na kupinga hotuba hiyo na kudai imejaa
upotoshwaji na siasa ndani kwani yeye ndiye aliyetafuta eneo hilo la
ujenzi wa hospitali hiyo kutoka kampuni ya mawala Advocate na siyo
kweli eneo hilo limetokana na maono aliyokuwa nayo Marehemu Advocate
Nyaga Mawala ya muda mrefu .
Picha
ikionyesha wa (kushoto) mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema
akiwa anatulizwa na mchungaji, Wilfred Mlayi, wakati mkuu
wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo (kulia) akiwa anatulizwa na mfadhili wa Mradi huo
ambaye ni daktari bigwa wa magonjwa ya kina mama na Mtoto Duniani Edru
Broun.
Wananchi
waliohudhuria uzinduzi wa ujenzi wa hospitali ya mama na mtoto ambaye
akupenda kutaja jina lake akiwa anamuomba mbunge wa jimbo la Arusha
mjini Godbless Lema kutulia na kumuaacha mkuu wa mkoa aendelee kutoa
hutuba. (Habari picha na Woinde Shizza, Arusha).
Kwa
upande wake mwenyekit wa Tasisi ya maendeleo ya jiji la Arusha (ARDF)
Elifuraha Mtowe Alisema kuwa eneo la kujegwa hospitali hiyo lilitolewa
na marehemu Nyaga Mawala nakwa ARDF kupitia ofisi ya mbunge wa jimbo la
Arusha mjini ndipo taasisi yao ya ARDF ikamamua kutafuta mfadhili ndipo
walipompata Martenity Afrika.
Alisema
kuwa tangu wampate mfadhili waliingia mkataba na wakakubaliana
hospitali iishe ndani ya mika mitano lakaini mfadhili mwenyewe
aliwaakikishia kuwa hospitali hiyo itaisha mapema iwezeka kwani
itakamilika ndani ya mwaka mmoja tu ili mama na mtoto aweze kupata
huduma kwa araka zaidi.
Awali
mbunge Lema aliwaambia waandishi wa habari kuwa mkuu wa mkoa huyo
alikuwa amegoma kuja kuzindua hospitali hiyo hadi pale mbunge huyo
alipoamua kumpiga simu katibu mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi na kumwambia
kuwa mkuu wa mkoa kagoma kuja kuzindua hospitali hiyo ndipo katibu mkuu
alipoamua kupiga simu wizara ya TAMISEMI ambapo ndio walimpigia simu
mkuu wa mkoa ili aweze kufika kwenye uzinduzi huo.
COMMENTS