DIRA YAOMBA RADHI KWA MKUU WA MAJESHI NA JWTZ KWA HABARI YENYE KICHWA "KIFARU CHA KIVITA CHA JWTZ CHAIBWA"

UONGOZI  wa kampuni ya  DIRA NEWSPAPER COMPANY LTD  wachapishaji wa gazeti  DIRA YA MTANZANIA  unamwomba radhi Mkuu wa Majes...









UONGOZI wa kampuni ya DIRA NEWSPAPER COMPANY LTD wachapishaji wa gazeti DIRA YA MTANZANIA unamwomba radhi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa nchi na jeshi la wananchi wa Tanzania kwa ujumla kwa habari iliyochapishwa kwa bahati mbaya katika gazeti letu;  toleo Na.424 la Juni,20-26 ,2016 iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho “KIFARU CHA KIVITA CHA JWTZ CHAIBWA”.
Tunapenda kueleza kwa masikitiko kuwa habari hiyo ilichapishwa kwa bahati mbaya baada ya mtayarishaji wa kurasa (graphic designer) kuipanga habari ambayo ilikuwa haijakamilika kiuchunguzi na kuiacha iliyotakiwa ichapishwe siku hiyo.
Tunapenda JWTZ na watanzania wote kwa ujumla kuwa wafahamu kuwa gazeti la DIRA YA MTANZANIA halikulenga kuchafua Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kama ambavyo baadhi ya watu walivyofikiria. 
Tunafahamu mchango mkubwa wa jeshi la wananchi wa Tanzania kwa taifa letu na namna jeshi hilo linavyoshirikiana kwa kiasi kikubwa na vyombo vya habari hasa utoaji wa taarifa mbalimbali na kamwe jeshi hili tokea kuanzishwa kwake halijawahi kukwaruzana na vyombo vya habari jambo ambalo ni heshima kubwa kwetu na taifa kwa ujumla.
Hivyo uongozi wa gazeti hili umeonelea kuomba radhi kwa Mkuu wa majeshi (CDF), askari wote wa JWTZ na watanzania wote walioshitushwa na habari hiyo na hasa mkuu wa kikosi cha 83 KJ cha Kiluvya mkoani Pwani ambaye kikosi chake kilitajwa kama chanzo cha habari hiyo.
Na tunaomba ifahamike kuwa tumeomba radhi kwa ridhaa yetu na tunaamini kuwa “kuomba radhi” ni kitendo cha kiungwana kwa utamaduni wa waafrika na hasa watanzania tuliokulia katika misingi ya amani, upendo na utulivu na pia tunaamini kuomba kwetu radhi kutazidisha mahusiano mema na ya karibu kati yetu na JWTZ.
Tunatanguliza shukrani zetu.
Musiba Esaba …………………………..
Meneja utawala na Fedha.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: DIRA YAOMBA RADHI KWA MKUU WA MAJESHI NA JWTZ KWA HABARI YENYE KICHWA "KIFARU CHA KIVITA CHA JWTZ CHAIBWA"
DIRA YAOMBA RADHI KWA MKUU WA MAJESHI NA JWTZ KWA HABARI YENYE KICHWA "KIFARU CHA KIVITA CHA JWTZ CHAIBWA"
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjhrsQB1AmDISPbTsC7Ov_f2BFIU60bR2LPi4vOpTzmFLwO_P3UTNKQHSB1yxGCwkr4S9dr5YyfgtqqVxU6okx8Pl7mnvundp6xn0cyFw7183jakCkgR2rBR5q2NnJIVlu6algooZo32ls/s640/DIRA.PNG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjhrsQB1AmDISPbTsC7Ov_f2BFIU60bR2LPi4vOpTzmFLwO_P3UTNKQHSB1yxGCwkr4S9dr5YyfgtqqVxU6okx8Pl7mnvundp6xn0cyFw7183jakCkgR2rBR5q2NnJIVlu6algooZo32ls/s72-c/DIRA.PNG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2016/10/dira-yaomba-radhi-kwa-mkuu-wa-majeshi.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/10/dira-yaomba-radhi-kwa-mkuu-wa-majeshi.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy