MWALIMU NYERERE AENZIWE KWA VITENDO – NEC

 Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Kailima Ramadhani akiwasili nyumbani kwa familia ya Baba wa Taifa...





 Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Kailima Ramadhani akiwasili nyumbani kwa familia ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Butiama Musoma akiwa ameambatana na watumishi wa NEC  na baadhi ya wajumbe wa mkutano wa ALAT kutoka maeneo mbalimbali  kuzuru kaburi la Baba wa Taifa, Mwitongo wilayani Butiama. Tume ya Taifa ya Uchaguzi iko mkoani Mara kutoa elimu ya mpiga kura kwa wananchi.
 Muongoza wageni wa maeneo ya historia nyumbani kwa Baba wa Taifa, Mwitongo Butiama Bi. Gaudensia Waziri akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Bw. Kailima Ramadhani (mwenye kofia) kuhusu Kaburi na historia ya Chifu Burito aliyekuwa chiefu wa Kabila la Wazanaki.
 Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Kailima Ramadhani (Kushoto) akisalimiana na Msemaji Mkuu na kiongozi wa familia ya Baba wa Taifa Chifu Japhet Wanzagi (kulia) mara baada ya kuwasili eneo la Mwitongo wilayani Butiama. Wa Pili kutoka Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Butiama Bi. Annarose Nyamubi.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Kailima Ramadhani akiwasha mshumaa kwenye kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere eneo la Mwitongo, Butiama. Wengine wanaoonekana na baadhi ya wajumbe wa mkutano wa ALAT na watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Mwongoza wageni na Mhifadhi wa Makumbusho ya Mwalimu Nyerere Butiama, Jacob Thomas akitoa maelezo kuhusu picha za kumbukumbu za Baba wa Taifa kwa Mkurugenzi wa NEC Bw. Kailima Ramadhani na watumishi wa NEC walioitembelea makumbusho hiyo eneo la Mwitongo, Butiama –Musoma.
 Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa NEC waliotembelea nyumbani kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mwitongo, Butiama.    
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi waandishi wa habari wa mkoa wa Mara waliotembelea nyumbani kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Mwitongo, Butiama. Watendaji wa NEC wako mkoani Mara kutoa elimu ya mpiga kura kwa wananchi.
   
Na. Aron Msigwa – NEC, Musoma.

Viongozi wa vyama vya Siasa wametakiwa kuiga kwa vitendo uzalendo na moyo wa kujitoa  aliokuwa nao Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere enzi za uhai wake  ili kuliwezesha Taifa kupiga hatua kimaendeleo.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani  mara baada  kutembelea Kaburi na Makumbusho ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere eneo la Mwitongo wilayani Butiama.

Amesema kuwa kumbukumbu za Baba wa Taifa zilizohifadhiwa vizuri katika makumbusho hiyo zina mambo mengi ya kujifunza ambayo wanasiasa wanatakiwa kuyafanya kwa  vitendo hasa  uzalendo kwa nchi, uvumilivu, upendo  na moyo wa kujitoa kwa dhati kuwatumikia wananchi.

“Kupitia kumbukumbu hizi sisi watumishi wa Tume tumejifunza ukomavu wa demokrasia aliokuwa nao Mwalimu Nyerere akiwa ndani na nje ya Bara la Afrika,  wengi wanadhani Demokrasia ni wakati wa uchaguzi tu, kumbe demokrasia ni pamoja na kuheshimu watu wengine” Amesema Kailima.

Ameeleza kuwa maisha aliyoishi Baba wa Taifa ni mfano wa kuigwa na viongozi na watanzania wote hasa pale alipojitofautisha na viongozi wengi wa Bara la Afrika alipoepuka tamaa ya madaraka na mali kwa  manufaa ya taifa.

“Sote ni mashahidi kupitia kumbukumbu zake tumeona mahali alipokuwa anaishi mwalimu Nyerere kabla hajajengewa nyumba na Jeshi, kama Rais mstaafu wengi walitegemea asingeishi katika  eneo lile, kumbukumbu hii nzuri aliyoiacha inatufundisha watanzania kuwa mwalimu aliitanguliza Tanzania mbele kuliko maslahi yake binafsi” Amesisitiza Kailima.

Bw. Kailima amebainisha kuwa  NEC itaendelea  kumuemzi Baba wa Taifa kwa yale aliyoyafanya na kuyasimamia kwa manufaa ya taifa huku akitoa wito kwa  viongozi wa vyama vya Siasa wawe na kiasi na waridhike na vile walivyonavyo.

“Suala la kuridhika na kuwa na kiasi linapaswa kuzingatiwa, wanasiasa  wanapaswa kuwaheshimu wananchi wanaowachagua kupitia chaguzi mbalimbali,  matokeo yanapotoka kama ni sahihi basi wanasiasa wakubaliane na maamuzi yao”  Ameainisha Kailima.  

Kwa upande wake Mhifadhi wa Makumbusho ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Bw. Jacob Thomas amesema kuwa  watanzania wanayo mengi ya kujifunza kupitia vitu alivyoviacha Baba wa Taifa ambavyo vimehifadhiwa katika Makumbusho hiyo.

Amesema kuwa maisha ya uadilifu aliyoishi enzi za uhai wake na mchango wake katika kuiletea maendeleo Tanzania na Bara la Afrika vinapaswa kuenziwa kwa nguvu zote na viongozi wa Tanzania.


“Ninyi mliopata nafasi ya kuitembelea makumbusho hii mmejifunza vitu vingi kumhusu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwamba alikuwa ni mtu wa namna gani kwa viwango vya Afrika na dunia kutokana na kumbukumbu ya uadilifu aliyoiacha ndani na nje ya mipaka ya Tanzania”

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MWALIMU NYERERE AENZIWE KWA VITENDO – NEC
MWALIMU NYERERE AENZIWE KWA VITENDO – NEC
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhrYtjH6RlnTtja_58HK3xsxmlnrfXkJV-vL4WMVHIHDNtJMgEwQI2A0VJ-8BnhyphenhyphenH9494zcxlJc_UQJwvF77nayvLosKoEhcUsfPPjrOfzwrgmrWBJ2zRNhGpn-nNHUjxtXjovkpGzDKuFn/s640/Butiama+-+1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhrYtjH6RlnTtja_58HK3xsxmlnrfXkJV-vL4WMVHIHDNtJMgEwQI2A0VJ-8BnhyphenhyphenH9494zcxlJc_UQJwvF77nayvLosKoEhcUsfPPjrOfzwrgmrWBJ2zRNhGpn-nNHUjxtXjovkpGzDKuFn/s72-c/Butiama+-+1.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2016/09/mwalimu-nyerere-aenziwe-kwa-vitendo-nec.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/09/mwalimu-nyerere-aenziwe-kwa-vitendo-nec.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy