RAIS DKT. MAGUFULI KUFUNGUA MAADHIMISHO YA WAHANDISI DAR

Na Mwandishi Wetu. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimi...




Na Mwandishi Wetu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya kumi na nne ya Siku ya Wahandisi yatakayofanyika Septemba mosi hadi pili jijini Dar es Salaam.
Maadhimisho hayo ya siku mbili yanatarajiwa kukutanisha zaidi ya wahandisi elfu mbili kutoka ndani na nje ya nchi ili kupata fursa ya kufanya majadiliano ya kitaaluma, kufanya maonesho ya kiufundi na kibiashara, kuwatambua na kuwazawadia wahandisi wahitimu waliofanya vizuri katika mafunzo yao ya mwisho na kuwaapisha wahandisi waliokidhi vigezo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Msajili wa Bodi ya Wahandisi nchini (ERB), Eng. Steven Mlote amesema mada kuu katika maadhimisho hayo itakuwa ni “TANZANIA KUELEKEA KUWA NCHI YA UCHUMI WA KATI NA KUWA NCHI YA VIWANDA: NINI JUKUMU LA WAHANDISI”.
“Tumejipanga Siku ya Wahandisi mwaka huu iwe na mvuto wa pekee kwa sababu mada yake ni ya kitaifa ikiangalia Dira ya Maendeleo ya Taifa na mwelekeo wa nchi kuwa nchi ya viwanda” amesema Eng. Mlote.
Maadhimisho ya wahandisi Tanzania yamekuwa yakifanyika tangu mwaka 2013, lengo likiwa ni kuiwezesha jumuiya ya wahandisi nchini kuionesha jamii kile ambacho wahandisi wanaweza kukifanya katika kuleta maendeleo ya nchi.
Takribani wahandisi elfu 17 wanakadiriwa kuwepo nchini katika sekta mbalimbali, lengo likiwa ni kuwa na wahandisi elfu 83 ili kukidhi mahitaji ya nchi kuwa ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Msajili wa Bodi ya Wahandisi nchini (ERB), Eng. Steven Mlote akiongea na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya 14 ya Siku ya Wahandisi Tanzania itakayoadhimishwa Septemba mosi jijini Dar es Salaam.

Msajili wa Bodi ya Wahandisi nchini (ERB), Eng. Steven Mlote akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu maadhimisho ya 14 ya Siku ya Wahandisi Tanzania itakayoadhimishwa Septemba mosi jijini Dar es Salaam.
(Picha na Benjamin Sawe - MAELEZO)



 


COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: RAIS DKT. MAGUFULI KUFUNGUA MAADHIMISHO YA WAHANDISI DAR
RAIS DKT. MAGUFULI KUFUNGUA MAADHIMISHO YA WAHANDISI DAR
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjEyzZkMmaptyLWVnnPrH-RF2nEhNWhlbTUD82gI-wWl1biWRrsL-itu4-ecThTsu3VpXqd9B-PBK1V3ucGsxZzWK3lEKG4UDJflalOxC_s0vJNrJXQzuS9tr11aB0ITUA-KwcyeBi1liM/s640/1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjEyzZkMmaptyLWVnnPrH-RF2nEhNWhlbTUD82gI-wWl1biWRrsL-itu4-ecThTsu3VpXqd9B-PBK1V3ucGsxZzWK3lEKG4UDJflalOxC_s0vJNrJXQzuS9tr11aB0ITUA-KwcyeBi1liM/s72-c/1.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2016/08/rais-dkt-magufuli-kufungua-maadhimisho.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/08/rais-dkt-magufuli-kufungua-maadhimisho.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy