Mjumbe wa Bodi ya TEMESA Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula Mashauri akikabidhi cheti kwa mmoja wa mafundi Bw.Said...
Mjumbe wa Bodi ya TEMESA Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi
Mabula Mashauri akikabidhi cheti kwa mmoja wa mafundi Bw.Saidi Waziri kutoka
Arusha wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo kwa mafundi hao iliyofanyika
katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Agosti 26,2016.
Mjumbe wa Bodi ya TEMESA Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi
Mabula Mashauri akikabidhi moja ya vifaa vilivyotolewa kwa ajili ya karakana za
TEMESA kwa Bw. Japhet Mwita mmoja wa washiriki wa mafunzo yaliyofanyika hivi
karibuni katika hafla ya kuhitimisha mafunzo hayo iliyofanyika katika Chuo cha
Taifa cha Usafirishaji (NIT) Agosti 26,2016.
Mjumbe wa Bodi ya TEMESA Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi
Mabula Mashauri akionesha moja ya vifaa vilivyokabidhiwa na mafundi wa TEMESA
kwa ajili ya karakana zao wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo kwa mafundi
hao iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Agosti 26,2016.
Kaimu Mtendaji TEMESA
Mhandisi Manase Ole Kujan(kulia) akitoa neno kwa mafundi wa TEMESA wakati wa
hafla ya kuhitimisha mafunzo kwa mafundi hao iliyofanyika katika Chuo cha Taifa
cha Usafirishaji (NIT) Agosti 26,2016 kushoto ni Mjumbe wa Bodi ya TEMESA
Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula Mashauri
NA THERESIA MWAMI TEMESA
Mafundi wa TEMESA wameshauriwa kutumia mafunzo waliyoyapata
kuendana na mabadiliko ya teknolojia katika utengenezaji magari na vifaa vya
umeme.
Ushauri huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mjumbe wa Bodi
ya Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula
Mashauri wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo kwa mafundi Wakala hao
iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).
Brigedia Jenerali Msataafu Mhandisi Mabula
Mashauri amesema kuwa Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA
imedhamiria na kuhakikisha kuwa magari na mitambo yote ya Serikali
inatengenezwa kitaalam ili kuleta tija na thamani halisi ya fedha iliyokusudiwa
pamoja na kukidhi kiu na matarajio ya wateja.
”Napenda kuwakumbusha kwamba mnayo dhamana
kubwa ya kutengeneza magari ya Serikali hivyo kwa mafunzo mliyoyapata ninaamini
mmejenga uwezo wa kutosha wa kuhudumia magari na vifaa vya umeme kwa kutumia mfumo
wa kisasa” alisema Mhandisi Mashauri.
Ameongeza kuwa ni fursa pekee kwa mafundi waliopata mafunzo hayo
kwenda kuwafundisha wenzao ambao hawakuweza kupata mafunzo hayo ili kuongeza
kasi ya kutengenza magari na vifaa vya umeme na kupunguza changamoto zilizopo
katika utengenezaji magari kwa kutumia mfumo wa Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (TEHAMA).
Aidha Kaimu Mtendaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Mhandisi
Manase Ole Kujan amewashukuru washirika wa TEMESA wakiwemo Chuo cha Taifa cha
Usafirishaji (NIT) na kampuni ya Superdoll kwa kuwezesha kufanyika kwa mafunzo
hayo ambayo yataleta chachu ya utendaji kazi wa mafundi na karakana za TEMESA
zilizopo nchini nzima.
Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA kwa kushirikiana na Chuo cha
Taifa cha Usafirishaji (NIT) na kampuni ya Superdoll waliandaa mafunzo ya siku
14 yaliyoanza
Agosti 9 na kumalizika Agosti 26, 2016 yaliyoshirikisha jumla ya mafundi 25
kutoka mikoa mbalimbali ili kuwapa uwezo wa kutengeneza magari kwa kutumia
mifumo ya kisasa.
Baadhi wa mafundi wa Temesa kutoka mikoa mbalimbali nchini
wakimsikiliza mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kuhitimisha
mafunzo kwa mafundi hao iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji
(NIT) Agosti 26,2016.
(PICHA ZOTE NA THERESIA MWAMI TEMESA)
COMMENTS