Mkurungezi mtendaji wa Asasi ya Fedha, Jafari Selemani akisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa warsha iliyofanyika hivi karibuni, ...
Mkurungezi mtendaji wa Asasi ya Fedha, Jafari Selemani akisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa warsha iliyofanyika hivi karibuni, katika Chuo cha Kilimanjaro Insitute College (KIC) na kuwakutanisha wanavyuo zaidi ya 200 hapa jijini Dar es Salaam. Alitumia fursa hiyo kuwaasa vijana kuwa na tabia ya kuweka akiba na kujiandaa na maisha ya uzee. Moto wa asasi hiyo ni "UHURU WA KIFEDHA NI WAJIBU WAKO ". Kulia ni mtaalamu wa biashara na mhamasishaji wa vijana, Fasili Boniface.
|
Mhamasishaji wa vijana Mussa Mashauri akitoa mada kuhusu Vijana na Utendaji kazi katika warsha iliyoandaliwa na Asasi ya Fedha iliyofanyika katika chuo cha Kilimanjaro Insitute College (KIC) na kuwakutanisha wanachuo zaidi ya 200 toka chuo cha UDSM, Ustawi wa jamii, Teku , St. Joseph na KIC. Kushoto ni Murungezi Mtendaji wa KONCEPT na Mhamasishaji wa Vijana, Krantz Mwantepele. |
|
Mmoja wa wanachuo waliohudhuria warsha hiyo akiuliza swali kwa mwongoza Mada Musa Mashauri. |
|
Mtaalamu wa Biashara na Mhamasishaji wa vijana Fasili Boniface akiongoza mada kuhusu "Siri za jinsi ya kupata Ajira " katika warsha iliyoandaliwa na Asasi ya Fedha katika chuo cha Kilimanjaro Insitute College hivi karibuni. Wanachuo zaidi ya mia 200 walikuatna na kujaidili jijini Dar es Salaam. |
|
Mkurungezi Mtendaji wa KONCEPT na mhamasishaji wa vijana Krantz Mwantepele akisitiza jambo wakati akiongoza mada kuhusu "Siri za uhuru wa kifedha na fursa ambazo zipo nchini vijana wanaweza kujiajiri na kutengeneza thamani kwa jamii inayowazunguka, katika warsha iliyofanyika katika chuo cha KIC hivi karibuni. |
|
Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo wakisiliza kwa makini mada toka kwa Mkurungezi Mtendaji wa Koncept Krantz Mwantepele hivi karibuni. |
|
Mkurungezi Mtendaji wa Koncept akiongoza washiriki wa warsha hiyo kula kiapo kuwa wanaamini nguvu ya mafanikio ipo ndani yao na ni wajibu wao kutafuta fursa na kutimiza ndoto zao |
|
Mkurungezi wa Asasi ya Fedha, Jafari Selemani akitoa neno la kufunga warsha hiyo iliyofanyika katika chuo cha KIC na kukutanisha zaidi 200 kutoka vyuo vya UDSM , TEKU, USTAWI WA JAMII , ST JOSEPH NA KILIMANJARO INSTITUTE COLLEGE (KIC) wiki iliyopita katika makazi ya KIC. |
COMMENTS