Mkuu wa Mkoa wa Dar es S alaam, Paul Makonda akisalimiana na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Simon...
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akisalimiana na Kamanda wa
Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Simon Sirro, wakati alipowasili
kwenye ukumbi wa Karimjee kulikofanyika hafla ya kuapishwa kwa Wakuu wa
Wapya wa Wilaya za Jiji la Dar leo Julai 4, 2016. (PICHA ZOTE
NA OTHMAN MICHUZI - MMG).
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akisalimiana na Mwenyekiti wa
CCM Mkoa wa Dar es salaam, Ramadhan Madabida, wakati alipowasili kwenye
ukumbi wa Karimjee kulikofanyika hafla ya kuapishwa kwa Wakuu wa Wapya
wa Wilaya za Jiji la Dar es salaam leo Julai 4, 2016.
Na
Jacquiline Mrisho - MAELEZO
Mkuu wa Mkoa wa Dar
es Salaam, Mhe. Paul Makonda amewataka Wakuu wapya wa Wilaya kuimarisha ulinzi
na usalama kwa wananchi waliopo katika Wilaya zao ili kudumisha amani.
Makonda alisema hayo leo
jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Wakuu wa Wilaya juu ya kuwalinda
wananchi na mali zao na kuhakikisha usalama unakuwepo katika Wilaya wanazozisimamia.
Alieleza kuwa kwa kuwa
wao ndio wanaomuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli katika Wilaya zao, wanatakiwa kuhakikisha wametekeleza
ahadi zilizotolewa na Mhe. Rais wakati wa kampeni.
“Ningependa wakuu
wangu wa Wilaya mchukiwe kwa kusimamia Haki na Sheria kuliko kukumbatia uovu
kwa kuhitaji furaha ya muda mfupi, hakikisheni Sheria na Kanuni zilizopo kwenye
Katiba ndio ziwe muongozo wenu”, alisema Makonda.
Mkuu huyo wa Mkoa wa
Dar es Salaam aliwataka Wakuu wa Wilaya zake kuwasimamia Wakurugenzi wao ili
kuhakikisha wanatumia bajeti waliyopewa katika kutatua changamoto zilizopo
katika Wilaya zao.
Aidha, Makonda
amewasisitiza kuhakikisha kuwa kuanzia Julai 11 mwaka huu maeneo yote yanayofanya
biashara ya shisha kufungwa na kuweka maeneo maalumu kwa ajili ya kuvutia
sigara.
Wakuu wa Wilaya wapya
wamepewa wiki mbili za kutengeneza mpango kazi kwa kusoma ilani ya Chama cha
Mapinduzi (CCM), Hotuba ya Mhe.Rais John Magufuli aliyoisoma wakati wa ufunguzi
wa Bunge la 11 la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na mazingira ya kazi katika
maeneo yao.
Sehemu ya Wakuu wa Ulinzi na Usalama wa Jiji la Dar es salaam wakiwa kwenye hafla hiyo.
Sehemu ya Wageni mbalimbali waliohudhulia hafla hiyo.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akihutumia wananchi katika hafla
ya kuapishwa kwa Wakuu wa Wapya wa Wilaya za Jiji la Dar es salaam leo
Julai 4, 2016.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akimuapisha Mkuu wa Wilaya ya
Ilala, Sophia Mjema, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo
Julai 4, 2016.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akisaini hati ya kiapo cha Mkuu
wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema mara baada ya kumuapisha, katika Ukumbi
wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo Julai 4, 2016.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akimkabidhi Katiba ya nchi na
Ilani ya CCM Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema mara baada ya
kumuapisha, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo Julai 4,
2016.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akimuapisha Mkuu wa Wilaya ya
Kigamboni, Hashim Mgandilwa, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es
salaam leo Julai 4, 2016.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akimkabidhi Katiba ya nchi na
Ilani ya CCM, Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa mara baada
ya kumuapisha, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo Julai
4, 2016.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akimuapisha Mkuu wa Wilaya ya
Kinondoni, Ally Hapi, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo
Julai 4, 2016.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akisaini hati ya kiapo cha Mkuu
wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi mara baada ya kumuapisha, katika
Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo Julai 4, 2016.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda (kulia) akimkabidhi Katiba ya
nchi na Ilani ya CCM, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi mara baada
ya kumuapisha, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo Julai
4, 2016.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akimuapisha Mkuu wa Wilaya
ya Temeke, Felix Lyaviva, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam
leo Julai 4, 2016.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akisaini hati ya kiapo cha Mkuu
wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva mara baada ya kumuapisha, katika
Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo Julai 4, 2016.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda (kulia) akimkabidhi Katiba ya
nchi na Ilani ya CCM, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva mara baada
ya kumuapisha, katika Ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam leo Julai
4, 2016.
Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akiwa pamoja na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Simon Sirro.
Wakuu
wapya wa Wilaya wa Jiji la Dar es salaam, toka kushoto ni Mkuu wa
Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim
Mgandilwa, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi pamoja na Mkuu wa
Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva. Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Humphrey Polepole hakuweza kuhudhulia hafla hiyo kutokana na kupatwa na dharula. hivyo ataapishwa pindi atakapomaliza dharula yake.
Mapitio kigo katika hati ya Kiapo.
COMMENTS