JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO ...
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO
WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA FAMILIA YA JOSEPH EMILIO SENGA.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya Joseph Emilio Senga na wanahabari wote nchini kufuatia kifo cha aliyekuwa mpiga picha mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima na mwanahabari mkongwe Joseph Emilio Senga kilichotokea tarehe 27 Julai, 2016 nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa moyo.
Katika salamu zake Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) amesema tasnia ya habari imempoteza mtu aliyetoa mchango mkubwa katika kuleta maendeleo ya tasnia ya habari nchini.
“Joseph Senga alikuwa mwanahabari shupavu na hodari, ambaye siku zote alisimama kidete kupigania maendeleo ya tasnia ya habari na kutenda haki katika tasnia hiyo.
“Napenda kutoa salamu zangu za pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wote wa marehemu”
Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb) pia amewaombea wote walioguswa na kifo cha Joseph Emilio Senga kuwa na moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki cha kuondokewa na mpendwa wao.
RAHA YA MILELE UMPE EHE BWANA, NA MWANGA WA MILELE UMWANGAZIE
APUMZIKE KWA AMANI
AMINA.
Jeneza
lenye Mwili wa Marehemu Joseph Senga liwa katika Uwanja wa TP, Sinza
Uzuri jijini Dar es salaam wakati wakiamuaga kwenda Kwimba, Mwanza kwa
Maziko. Mwili wa Marehemu Joseph Senga unatarajiwa kuzikwa mara baada ya
kufika.
Jeneza la Mwili wa Joseph Senga likipewa heshima ya mwisho.
Wanahabari waliofika kumuaga mwenzao.
Mpiga Picha Mkuu wa Kampuni ya The Guardiun, Suleiman Mpochi akitoa salamu za rambirambi.
Waziri
Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akiteta jambo na Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye wakati wakiwa kwenye shughuli
ya kuaga Mwili wa Aliekuwa Mpiga Picha Mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima,
Marehemu Joseph Senga, iliyofanyika katika Uwanja wa TP, Sinza Uzuri,
Jijini Dar es salaam leo.
Mhariri Mtendaji wa Gazeti ya Tanzania Daima, Neville Meena akizungumza.
Familia ya Marehemu Joseph Senga ikiwa ni yenye huzuni kubwa kuondokewa na Mpendwa wao.
Mbunge wa Jimbo la Kibamba, John Mnyika akitoa salamu za Rambirambi.
Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Said Kubenea akizungumza.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe akizungumza.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akitoa salamu.
Waziri
Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa
Marehemu Joseph Senga, aliekuwa Mpiga Picha Mkuu wa Gazeti la Tanzania
Daima, aliefariki Dunia hivi karibuni, wakati wa shughuli ya kuaga mwili
huo, iliyofanyika katika Uwanja wa TP, Sinza Uzuri, Jijini Dar es
salaam.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akitoa heshima za
mwisho kwa mwili wa Marehemu Joseph Senga, aliekuwa Mpiga Picha Mkuu wa
Gazeti la Tanzania Daima, aliefariki Dunia hivi karibuni, wakati wa
shughuli ya kuaga mwili huo, iliyofanyika katika Uwanja wa TP, Sinza
Uzuri, Jijini Dar es salaam.
Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura akitoa
heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Joseph Senga, aliekuwa Mpiga
Picha Mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima, aliefariki Dunia hivi karibuni,
wakati wa shughuli ya kuaga mwili huo, iliyofanyika katika Uwanja wa TP,
Sinza Uzuri, Jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, akitoa
heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Joseph Senga, aliekuwa Mpiga
Picha Mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima, aliefariki Dunia hivi karibuni,
wakati wa shughuli ya kuaga mwili huo, iliyofanyika katika Uwanja wa TP,
Sinza Uzuri, Jijini Dar es salaam.
COMMENTS