MADAKTARI BINGWA KUTOKA CHINA WATOA MATIBABU MUSOMA VIJIJINI KWA AWAMU YA TATU

Na Mwandishi Wetu Madaktari Bingwa kutoka nchini China   wametoa   huduma ya matibabu kwa wananchi mbalimbali katika Zahanati ya Ny...







Na Mwandishi Wetu
Madaktari Bingwa kutoka nchini China   wametoa  huduma ya matibabu kwa wananchi mbalimbali katika Zahanati ya Nyakatende, Jimbo la Musoma Vijijini ikiwa ni mwaliko wa Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni  Waziri wa  Nishati na Madini,  Profesa Sospeter Muhongo.
Hii ni Awamu ya Tatu kwa Madaktari hao kutoa huduma hiyo ya matibabu wilayani  Musoma ambapo huduma kama hiyo ilitolewa mwezi Juni na Machi mwaka huu.
Akizungumza na wananchi wa Kata ya Nyakatende kabla ya kuanza kwa matibabu hayo, Profesa Muhongo alisema kuwa  matibabu na dawa hizo ni za bure hivyo wananchi wasisite kutibiwa.
“ Lengo letu ni kuhakikisha kuwa wananchi waliopo vijijini wanapata huduma bora za afya, maji, elimu,  miundombinu na umeme,  ndiyo maana hata hapa nimewaletea gari  ndogo ya wagonjwa ili iwasaidie katika kupata matibabu,” alisema Profesa Muhongo.
Madaktari hao wamebobea katika kutibu magonjwa mbalimbali kama ya Wanawake, Watoto, Meno, Vinywa, koo, macho, kisukari, presha, tumbo na kufanya upasuaji.
Aidha Ujumbe wa Madaktari hao wanaojitolea, walikabidhi vifaa kama kalamu,  vitabu vya Sayansi, Hisabati, Maarifa ya Jamii,  mipira na madafrari vyenye jumla ya shilingi milioni 4 ambavyo viligawiwa kwa shule mbalimbali za Msingi  na Sekondari wilayani humo.
Akiwa katika Zahanati hiyo Profesa Muhongo alichangia mifuko100 ya simenti na  mabati 100 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba na choo cha wafanyakazi wa kituo hicho.
Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Musoma, Flora Yongolo  alimpongeza Profesa Muhongo kwa juhudi mbalimbali anazofanya katika Jimbo la Musoma vijijini  hasa katika kuboresha elimu, afya na kilimo huku akitolea mfano ugawaji wa madawati na vitabu mashuleni na kilimo cha majaribio cha zao la alizeti ambacho kimeonyesha matokeo mazuri baada ya Profesa Muhongo kugawa bure mbegu hizo za alizeti kwa wakulima.
Aidha,  Yongolo alisema atahakikisha kuwa vifaa ambavyo Profesa Muhongo amevitoa katika Jimbo hilo  kama madawati na  gari Tano za kubebea wagojwa,  vinatunzwa na kulindwa ambapo alitoa wito kwa wananchi na watendaji wa shule na vituo vya afya kuhakikisha hilo linafanikiwa.
Awali Profesa Muhongo alisema kuwa vitabu alivyogawa jimboni humo vimeletwa na Rafiki zake kutoka nchini Marekani ambapo thamani ya vitabu hivyo ni Dola za Marekani 250,000.
Kuhusu zao la alizeti, Profesa Muhongo alisema kuwa wakulima watakaolima na kuvuna zao hilo kwa mafanikio, watanunuliwa mashine ndogo za kukamua alizeti ili waweze kuuza mafuta ya alizeti na kujiongezea kipato.


Waziri wa Nishati na Madini na Mbunge wa MusomaVijijini, Profesa Sospeter Muhongo (mwenye koti la Bluu) akiwa na Ujumbe wa Madaktari Bingwa kutoka China ambao walifika wilaya ya Musoma ili kutoa matibabu ya bure kwa wananchi katika Zahanati ya Nyakatende.

Waziri wa Nishati na Madini na Mbunge wa Musoma Vijiini, Profesa Sospeter Muhongo (mwenye koti la Bluu) akiwa na wananchi wa Kata ya Nyakatende wilayani  Musoma na Ujumbe wa Madaktari Bingwa kutoka China waliofika katika Zahanati ya Nyakatende ili kutoa matibabu ya bure kwa wananchi. 





COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MADAKTARI BINGWA KUTOKA CHINA WATOA MATIBABU MUSOMA VIJIJINI KWA AWAMU YA TATU
MADAKTARI BINGWA KUTOKA CHINA WATOA MATIBABU MUSOMA VIJIJINI KWA AWAMU YA TATU
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiYoNcsXJ6E4-ayNovftIl5B6ewtNxT1OcRsU6sOfDxSwA2F9WlNjr7zgu9StnrR1uT4KUnAP-WH_urAHGh8Hm4Vf0-jgBL-K4AasATQX9gasnTUUCiMGxoXLRCtJEXgBCKsq81LFD2pAc/s640/picha+mbili.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiYoNcsXJ6E4-ayNovftIl5B6ewtNxT1OcRsU6sOfDxSwA2F9WlNjr7zgu9StnrR1uT4KUnAP-WH_urAHGh8Hm4Vf0-jgBL-K4AasATQX9gasnTUUCiMGxoXLRCtJEXgBCKsq81LFD2pAc/s72-c/picha+mbili.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2016/07/madaktari-bingwa-kutoka-china-watoa.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/07/madaktari-bingwa-kutoka-china-watoa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy