WAZIRI MKUU MAJALIWA KUHUDHURIA MKUTANO WA SADC BOTSWANA LEO

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameondoka jana kwenda Gaborone, Botswana kuhudhuria Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali ...







WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameondoka jana kwenda Gaborone, Botswana kuhudhuria Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini  mwa Afrika wa Double Troika ya Asasi ya Siasa Ulinzi na Usalama (SADC Double Troika Summit)   utakaofanyika leo, Juni 28, 2016.

 
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
Mhe. Waziri Mkuu anamuwakilisha Mhe. Rais Dk. John Pombe Magufuli kwenye mkutano huo utakaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Gaborone (GICC).

Mkutano huo utafunguliwa na Rais wa Jamuhuri ya Botswana Mhe. Lt. Jen. Seretse Khama Ian Khama ambaye ni SADC, utajadili hali ya siasa, ulinzi na usalama nchini Lesotho. Mkutano huu   utatanguliwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu ambao utafanyika leo (Jumatatu, 27 Juni, 2016).
Pia mkutano huo utahudhuriwa na Marais wa Afrika Kusini, Mwenyekiti aliyetoka (outgoing chair) wa Asasi ya Siasa Ulinzi na Usalama Mhe. Jacob Zuma , Mhe. Jacinto Filipe Nyusi, Rais wa Jamuhuri ya Msumbiji na Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Siasa, Ulinzi na Usalama.
Wengine ni Mfalme Mswati III, Mfalme wa Swaziland ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa SADC, Mhe. Robert Mugabe, Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe na Mwenyekiti anayeondoka wa SADC.
Waziri Mkuu amefuatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Augustine Mahiga, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dk. Aziz Mlima na Maofisa wengine waandamizi.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM.
JUMATATU, JUNI 27, 2016.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI MKUU MAJALIWA KUHUDHURIA MKUTANO WA SADC BOTSWANA LEO
WAZIRI MKUU MAJALIWA KUHUDHURIA MKUTANO WA SADC BOTSWANA LEO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhRBVp58RNCLNG3fFJ8FL8r4-yXaIZyTFIO81sj8N0spRT74ZHuobCxB3Tv4lkbd2Cgq84PYmxhwdhWhUwnm5w6V6XljdBBtal9uZdPZRps8snF5571VmxBq12m9H_zzH-rFbqfS6uaGbI/s640/WAZIRI+MKUU%252C+KASSIM+MAJALIWA+MAJALIWA.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhRBVp58RNCLNG3fFJ8FL8r4-yXaIZyTFIO81sj8N0spRT74ZHuobCxB3Tv4lkbd2Cgq84PYmxhwdhWhUwnm5w6V6XljdBBtal9uZdPZRps8snF5571VmxBq12m9H_zzH-rFbqfS6uaGbI/s72-c/WAZIRI+MKUU%252C+KASSIM+MAJALIWA+MAJALIWA.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2016/06/waziri-mkuu-majaliwa-kuhudhuria-mkutano.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/06/waziri-mkuu-majaliwa-kuhudhuria-mkutano.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy