RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA WAKUU WA WATATU WA MIKOA NA KUZUNGUMZA NA WAKUU WAPYA WA WILAYA IKULU DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Juni, 2016 amewaapisha wakuu wa Mikoa watatu aliowa...

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Juni, 2016 amewaapisha wakuu wa Mikoa watatu aliowateua Jumapili iliyopita tarehe 26 Juni, 2016.

Wakuu wa Mikoa walioapishwa leo Ikulu Jijini Dar es salaam ni Dkt. Binilith Satano Mahenge ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Charles Ogesa Mlingwa ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mara na Bi. Zainab Rajab Telack ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Hafla ya kuapishwa kwa wakuu hao wa Mikoa imehudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama na wakuu wa wilaya wateule ambao waliteuliwa na Rais Magufuli Jumapili iliyopita tarehe 26 Juni, 2016.

Aidha, miongoni mwa wakuu wa wilaya 139 walioteuliwa, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko madogo katika wilaya tatu ambapo ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Rombo Mteule Mhe. Fatma Hassan Toufiq na badala yake amemteua Bi. Agness Elias Hokororo kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo, ametengua uteuzi wa Mkuu wa wilaya ya Serengeti Mteule Bw. Emile Yotham Ntakamulenga na badala yake amemteua Bw. Nurdin Hassan Babu kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo na ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mteule Bw. Fikiri Avias Said na badala yake amemteua Bw. Miraji Mtaturu kuwa Mkuu wa wilaya hiyo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka wakuu wa wilaya wateule kwenda kuchapa kazi na kutatua kero za wananchi katika wilaya zao huku wakizingatia kufanya kazi kwa uadilifu na uaminifu.

Rais Magufuli pia amewataka kusimamia ukusanyaji mapato ya serikali na matumizi ya fedha na rasilimali nyingine za umma, kuhakikisha wananchi wapo salama na pia kuhakikisha wananchi wanafanya kazi za uzalishaji mali.

"Katika kazi hizi wapo watakaowakejeli, katika kazi hizi wapo watakaowadhihaki, nyinyi kavumilieni na mmuweke Mungu mbele na mkawaweke watanzania mbele, mkafanye kazi kadiri Mungu atakavyokuwa amewaongoza.

"Nataka kuwahakikishia tunawaunga mkono kwa nguvu zote, mkafanye kazi bila uwoga wowote, katembeeni kifua mbele, kwa sababu tumewaamini wala msiwe na wasiwasi, ukifanya kitu kizuri kwa dhamira yako iliyo njema kitazaa matunda mazuri, ukifanya kitu kwa unafiki hakitafanikiwa" Amesema Rais Magufuli

Katika hafla hiyo, wakuu wa mikoa walioapishwa na wakuu wa wilaya wateule wamekula kiapo cha ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma, zoezi ambalo limeongozwa na Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Salome Kaganda.

Katika hatua nyingine, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya Mazungumzo na mwenyekiti mwenza wa taasisi ya Bill and Melinda Gates ya Marekani Bi. Melinda Gates ambapo Rais Magufuli amemuhakikishia mwenyekiti mwenza huyo kuwa serikali ya awamu ya tano itaendeleza na kuimarisha zaidi uhusiano wake na taasisi hiyo ambayo imekuwa ikishirikiana na Tanzania katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Afya, Uongozi na Kilimo.

Kwa upande wake Bi. Melinda Gate amempongeza Rais Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya katika kukabiliana na rushwa na kuongeza ukusanyaji wa mapato ya serikali, na pia kwa nia yake thabiti ya kuinua sekta ya kilimo inayotegemewa na idadi kubwa ya watanzania na ameahidi kuwa taasisi ya Bill and Melinda Gates itaendelea kushirikiana na Serikali ya awamu ya tano katika kuongeza tija ya uzalishaji wa mazao ya kilimo.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
29 Juni, 2016 .
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Binilith Satano Mahenge kuwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi vitendea kazi Dkt. Binilith Mahenge baada ya kumwapisha kuwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akimuapisha Dkt. Charles Mlingwa kuwa mkuu wa mkoa wa Mara Ikulu jijini Dar es Salawanaoshuhudia ni Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi na Naibu Katibu wa Baraza la Mawaziri, Hassan Shebuge. (Picha zote na Robert Okanda)
 Rais Dkt. John Magufuli akitia sahihi kiapo cha  Zainab Telack Mkuu mpya wa mkoa wa Shinyanga baada ya kumwapisha Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
  Dkt. Charles Mlingwa mkuu mpya wa mkoa wa Mara.

  Zainab Telack mkuu wa mkoa wa Shinyanga akiwa katika hafla ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam leo.

  Zainab Telack mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Dkt. Charles Mlingwa (katikati) na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Dkt. Binilith Magenge wakiwa katika hafla ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam leo.

 Dkt. Binilith Satano Mahenge mkuu wa mkoa wa Ruvuma akiwa katika hafla ya kuapishwa Ikulu  Dar es Salaam leo.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiongea na Wakuu wa Mikoa pia Wakuu wa Wilaya wakati wa hafla hiyo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wakuu wa mikoa pamoja na Wakuu wa Wilaya wateule mara baada ya kumaliza kuwaapisha wakuu wa mikoa ya Shinyanga, Mara na Ruvuma Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - TAMISEMI, Mhe George Simbachawene, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mhandisi Mussa Iyombe wakiwa na sehemu ya Wakuu wapya wa Wilaya waliofika Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 29, 2016 kula kiapo cha maadili ya viongozi kabla ya kwenda kuapishwa na wakuu wa Mikoa katika vituo vyao vya kazi

Wakuu wa wilaya wapya wakiwa tayari kwa kiapo cha maadili ya viongozi Ikulu jijini Dar es Salaam leo Juni 29, 2016  kabla ya kwenda kuapishwa na wakuu wa Mikoa katika vituo vyao vya kazi.

Wakuu wa wilaya wapya wakila kiapo cha maadili ya viongozi Ikulu jijini Dar es Salaam leo Juni 29, 2016  kabla ya kwenda kuapishwa na wakuu wa Mikoa katika vituo vyao vya kazi.

Wakuu wa wilaya wapya wakila kiapo cha maadili ya viongozi mbele ya Kamishna wa maadili ya Utumishi wa Umma nchini Tanzania Jaji Mstaafu Salome Kaganda (kushoto) waliofika Ikulu jijini Dar es Salaam leo Juni 29, 2016 kabla ya kwenda kuapishwa na wakuu wa Mikoa katika vituo vyao vya kazi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela baada kuwaapisha Wakuu wa mikoa mara baada ya kumaliza kuwaapisha wakuu wa mikoa ya Shinyanga, Mara na Ruvuma Ikulu jijini Dar es Salaam.

Wakuu wa wilaya wapya wakiwa tayari kwa kiapo cha maadili ya viongozi Ikulu jijini Dar es Salaam leo Juni 29, 2016  kabla ya kwenda kuapishwa na wakuu wa Mikoa katika vituo vyao vya kazi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro baada kuwaapisha Wakuu wa mikoa mara baada ya kumaliza kuwaapisha wakuu wa mikoa ya Shinyanga, Mara na Ruvuma Ikulu jijini Dar es Salaam.

Wakuu wa wilaya wapya wakila kiapo cha maadili ya viongozi Ikulu jijini Dar es Salaam leo Juni 29, 2016  kabla ya kwenda kuapishwa na wakuu wa Mikoa katika vituo vyao vya kazi.

Wakuu wa wilaya wapya wakila kiapo cha maadili ya viongozi Ikulu jijini Dar es Salaam leo Juni 29, 2016  kabla ya kwenda kuapishwa na wakuu wa Mikoa katika vituo vyao vya kazi.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA WAKUU WA WATATU WA MIKOA NA KUZUNGUMZA NA WAKUU WAPYA WA WILAYA IKULU DAR ES SALAAM
RAIS DKT. MAGUFULI AWAAPISHA WAKUU WA WATATU WA MIKOA NA KUZUNGUMZA NA WAKUU WAPYA WA WILAYA IKULU DAR ES SALAAM
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjF1PEIrM4l8VRhisxKKvWVRCz_w8_kFuGABDdqDiuHg3_bV5KPtmnTGtQDcSk1mHbSRUcqyzT956PzZUIxWd7KHPoUevkabQTowCp4AvC5tZQVctwdNVhZZGmbUJaCnyHTnwZAh1IdtJ6y/s640/Rais+Magufuli+awasihi+watanzania+kuungana+na+waislamu+kuliombea+taifa.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjF1PEIrM4l8VRhisxKKvWVRCz_w8_kFuGABDdqDiuHg3_bV5KPtmnTGtQDcSk1mHbSRUcqyzT956PzZUIxWd7KHPoUevkabQTowCp4AvC5tZQVctwdNVhZZGmbUJaCnyHTnwZAh1IdtJ6y/s72-c/Rais+Magufuli+awasihi+watanzania+kuungana+na+waislamu+kuliombea+taifa.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2016/06/rais-dkt-magufuli-awaapisha-wakuu-wa.html
http://robertokanda.blogspot.com/

true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy