DAWASCO WAFANYA USAFI WA MAZINGIRA KATIKA UTEKELEZAJI WA USAFI KILA JUMAMOSI YA MWISHO WA WMEZI

  Baadhi ya Wafanyakazi wa DAWASA jijini Dar es Salaam waliokutwa wakifanya usafi wa mazingira kutii agizo la Kufanya ...









 Baadhi ya Wafanyakazi wa DAWASA jijini Dar es Salaam waliokutwa wakifanya usafi wa mazingira kutii agizo la Kufanya Usafi kwa kila Jumamosi ya kila mwisho wa mwezi  ili kuyaweka maeneo ya Ofisi za Malamka hiyo katika hali ya usafi.
(PICHA NA ARON MSIGWA – MAELEZO).



Baadhi ya Wakazi wa Mwananyamala wakipakia Taka walizozoa katika mitaa yao katika gari la kuzoa Taka la Manispaa ya Kinondoni.


Baadhi ya Wafanyakazi wa DAWASA jijini Dar es Salaam waliokutwa wakifanya usafi wa mazingira kutii agizo la Kufanya Usafi kwa kila Jumamosi ya kila mwisho wa mwezi  ili kuyaweka maeneo ya Ofisi za Malamka hiyo katika hali ya usafi.

Baada ya usafi
NA ARON MSIGWA-MAELEZO.
Wito umetolewa kwa Taasisi,mashirika, makampuni na watu binafsi kuanzia ngazi ya familia kuendelea kuitumia Siku ya jumamosi ya kila mwisho wa mwezi kufanya usafi wa mazingira, kupanda miti na kutunza vyanzo vya maji kwa hiari bila kusubiri kushurutishwa  na sheria  kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kizazi kijacho.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi wakiwemo wafanyabiashara na wafanyakazi   wa  taasisi na mashirika mbalimbali  waliokuwa wakitekeleza wakifanya usafi katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam leo wamesema kuwa hatua ya  Serikali kuirasimisha Siku ya jumamosi ya kila mwisho wa mwezi  kuwa siku ya usafi wa mazingira  kitaifa inaweka msisitizo kuhusu jukumu la kila mwananchi kuwa mlinzi na mwangalizi wa mazingira katika sehemu anayoishi.
Wamesema Suala la usafi wa mazingira linawahusu watu wote, hivyo kila mwananchi anao wajibu wa kushiriki kikamilifu kufanya Usafi wa Mazingira kwenye Makazi yake, Maeneo ya Biashara, maeneo ya Taasisi za Umma na maeneo yenye mikusanyiko ya watu mbalimbali kama masoko na minada.
Bi. Zaituni Musa mkazi wa Mwananyamala, Kinondoni jijini Dar es salaam aliyekuwa akisafisha mifereji eneo la mtaa anaoishi akishirikiana na wananchi wenzake amesema kuwa suala la usafi wa mazingira ni jukumu la kila mwananchi bila kuangalia cheo au nafasi yake katika jamii kwa kuwa kuishi katika mazingira machafu kuna athari kubwa kiafya hususan kuchangia milipuko ya magonjwa ikiwemo Kipindupindu.
" Suala la usafi wa mazingira linatuhusu sote, ni wakati wa kuchukua hatua na kuacha kuishi kwa mazoea,nawaomba watanzania wenzangu tufanye usafi bila kulazimishwa na Serikali kila mmoja atimize wajibu wake" Amesisitiza Bi.Zaituni.
Nao  baadhi ya wafanyabiashara wenye maduka eneo la Mwananyamala na  wale wa Soko la vyakula la Buguruni, Manispaa ya Ilala waliokuwa wamefunga maduka na biashara zao kupisha muda wa kufanya usafi wa mazingira kuanzia saa 12 hadi saa 4 asubuhi wamesema kuwa uamuzi wa Serikali kuitangaza Jumamosi ya kila mwisho wa mwezi kuwa Siku ya Usafi wa mazingira unatoa fursa kwao Kufanya Usafi wa mazingira katika maeneo wanayofanyia biashara tofauti na awali.
" Watanzania wote wa Mijini na Vijijini tujenge desturi ya kuweka mazingira yetu katika hali ya usafi wakati wote na katika jambo hili kila mmoja wetu awe mlinzi wa kukemea watu wenye tabia za kutupa taka hovyo ili maeneo yetu yawe katika hali ya usafi na yakuvutia wakati wote" Amesisitiza Bw. Haule John mmoja wa wafanyabiashara hao.
Aidha, wamesisitiza kuwa ili kuyaweka maeneo mbalimbali katika hali ya usafi  Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 lazima itumike kwa mtu yeyote atakayekaidi kufanya usafi siku hiyo kutozwa faini isiyopungua shilingi elfu hamsini au kifungo cha kuanzia miezi mitatu mpaka miaka saba, faini ya shilingi laki mbili ya papo hapo na shilingi milioni tano    kwa kampuni au taasisi  itakayotupa taka hovyo atatozwa.
Ikumbukwe kuwa Desemba 23 mwaka jana, Serikali kupitia kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Luhaga Mpina ilitangaza kuwa usafi wa mazingira nchi nzima utakuwa ukifanyika kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi.
Mhe.Mpina alisema kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya viongozi na watendaji wanaopuuzia kusimamia shughuli za usafi katika siku hiyo pia kwa wananchi wanaoshindwa kufanya usafi katika maeneo yao kwa mujibu wa sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake pamoja na Sheria ndogo.
Aidha, kabla ya jumamosi ya kila mwezi kutangazwa kuwa siku ya Usafi nchini, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kwa kuzingatia sheria ya Sikukuu za Kitaifa, aliamua maadhimisho ya sherehe za Uhuru , 9 Desemba 2015 kwa upande wa Tanzania Bara yatumike kufanya usafi wa mazingira nchi nzima na kuhamasisha watu kujituma kufanya kazi.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: DAWASCO WAFANYA USAFI WA MAZINGIRA KATIKA UTEKELEZAJI WA USAFI KILA JUMAMOSI YA MWISHO WA WMEZI
DAWASCO WAFANYA USAFI WA MAZINGIRA KATIKA UTEKELEZAJI WA USAFI KILA JUMAMOSI YA MWISHO WA WMEZI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhA0RSH3SmMCxZc6SS0Rol2fyRQutWdVAaIM2SZWilDCxX6exmS8UqL5xsYwKX7OcmBhwsf8ttRTHksxOfL6hWLqBOrwLHoy0rlYbyvDKK0G7xkQDhWEE0qkg7ZjuG2LxKVgyISY4NVfKU/s640/image.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhA0RSH3SmMCxZc6SS0Rol2fyRQutWdVAaIM2SZWilDCxX6exmS8UqL5xsYwKX7OcmBhwsf8ttRTHksxOfL6hWLqBOrwLHoy0rlYbyvDKK0G7xkQDhWEE0qkg7ZjuG2LxKVgyISY4NVfKU/s72-c/image.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2016/06/dawasco-wafanya-usafi-wa-mazingira.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/06/dawasco-wafanya-usafi-wa-mazingira.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy