TBL GROUP NA TUICO WATILIANA SAHIHI MKATABA BORA WA MASLAHI YA WAFANYAKAZI

    Katibu mkuu wa TUICO Boniface Nkakatisi (kushoto) akisaini mkataba wa hiari wa hali bora na maslahi ya wafanyakazi na Mkuru...





 
 Katibu mkuu wa TUICO Boniface Nkakatisi (kushoto) akisaini mkataba wa hiari wa hali bora na maslahi ya wafanyakazi na Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group   Roberto Jarrin (kulia) jana mjini Dodoma  katikati anayeshuhudia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri mkuu sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira,na Watu wenye ulemavu Mh. Jenista Mhagama.
 
 Mkurugenzi Mkuu  wa TBL Group  Roberto Jarrin (kulia) akikabidhiana mkataba  wa hiari wa  hali bora na maslahi ya wafanyakazi na  Katibu Mkuu wa TUICO Boniface Nkakatisi (kushoto) jana mjini Dodoma mara baada ya kutiliana saini  mjini Dodoma,  katikati anayeshuhudia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri mkuu sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira,na Watu wenye ulemavu, Mh.Jenista Mhagama
 Baadhi ya Wafanyakazi wa kampuni ya  TBL Group wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira,na Watu wenye ulemavu ,Jenista Mhagama baada ya kusaini rasmi mkataba wa hiari wa hali bora na maslahi ya wafanyakazi kati ya kampuni hiyo  na TUICO
Meneja Masoko na Udhamini kampuni ya  TBL Group, George Kavishe (kushoto) akimwonyesha  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri mkuu sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira,na Watu wenye ulemavu Jenista Mhagama bidhaa zinazozalishwa na kampuni hiyo alipotembelea banda hilo jana kabla ya kusaini kwa mkataba wa hiari kati ya TBL na TUICO katika hoteli ya St Gaspar Mjini Dodoma jana.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi,Vijana, Ajira na Watu wenye ulemavu Jenista Mhagama  akiangalia moja ya bidhaa zinazozalishwa na kampuni hiyo. Kushoto ni Meneja Masoko na Udhamini kampuni ya  TBL Group, George Kavishe
 
Mtaalamu wa ubora kampuni ya bia  TBL Rebecca Semoka akimwonyesha zao la shayiri ambalo linatumika kutengenezea bia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira,na Watu wenye ulemavu Jenista Mhagama (kushoto)
*********************
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu sera,bunge,kazi,vijana,ajira Watu wenye ulemavu Jenista Mhagama amesema kuwa njia pekee ya kuleta ufanisi sehemu za kazi na kuondoa migogoro ni kuwepo na uhusiano mzuri baina ya waajiri na wafanyakazi wao.

Akihutubia Uongozi na wafanyakazi wa TBL Group wakati wa hafla ya kampuni hiyo kusaini mkataba na Chama Cha kutetea maslahi ya  wafanyakazi cha TUICO unaohusiana na maslahi bora ya wafanyakazi iliyofanyika jana katika ukumbi wa Mt.Gaspar Mjini Dodoma,Waziri Mhagama alisema hakuna mafanikio yanayoweza kupatikana katika mazingira yenye uhusiano mbaya  baina ya mwajiri na wafanyakazi wake. katika sehemu za kazi.

“Nawapongeza waajiri wanaokaa na wafanyakazi wao na kukubaliana kuhusiana na masuala ya maslahi kama ambavyo TBL mnafanya na waajiri wote wanapaswa kuzingatia suala hili ili kuleta tija na ufanisi sehemu zao kazi ili kuongeza uzalishaji na kuchangia kukuza uchumi wa Taifa”.Alisema Mhagama.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin alisema kuwa mtazamo wa kampuni hiyo ni kuwa kioo na mfano wa uwekezaji mzuri nchini na mbali na kuongeza ubora na uzalishaji kwenye bidhaa zake imejikita pia katika kuboresha maslahi ya wafanyakazi wake,kuongeza ajira nchini,kuwezesha vikundi vya wafanyabiashara wadogo na wa kati,kuchangia pato la serikali kwa njia ya kodi.

Alisema TBL itaendelea kuunga mkono jitihada za serikali kuleta maendeleo kwa kushiriki kusaidia miradi mbalimbali ya kuinua maisha ya wananchi huusani wakulima na kuchangia pato la serikali kwa njia ya kodi “Tunayo mikakati  ya kuboresha maisha ya wakulima nchini ambayo tayari tumeanza kuitekeleza ikiwemo kulipa kodi ambako tumekuwa tukiongoza kulipa kodi na kutunukiwa tuzo mbalimbali”.Alisema.

 Katibu  mkuu wa TUICO Taifa,  Boniface Nkakatisi alipongeza hatua ya TBL kutiliana saini ya makubaliano ya ubora wa maslahi na wafanyakazi wake kwa kuwa italeta ufanisi na kuondoa migogoro na malalamiko  “Mara nyingi chama chetu kimekuwa kikishughulikia migogoro baina ya wafanyakazi na waajiri wao ,tukio kama hili la leo linafurahisha na viwanda na  makampuni yote yanapaswa kutekeleza jambo hili”.Alisema.

Kabla ya kushuhudia utiwaji saini makubaliano haya,Waziri Mhagama alitembelea maonyesho ya  kampuni yaTBL Group na kupatiwa maelezo kuhusiana na jinsi inavyoendesha shughuli zake na maelezo ya bidhaa ambazo  inazalisha.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TBL GROUP NA TUICO WATILIANA SAHIHI MKATABA BORA WA MASLAHI YA WAFANYAKAZI
TBL GROUP NA TUICO WATILIANA SAHIHI MKATABA BORA WA MASLAHI YA WAFANYAKAZI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEizv64N2IieGrH7IuRC-haiuDLEDAYfc1nJTPxn8Qo4FsAEUTT77utgrEuFEoNac119bj2sbXGDMgWt0rzPpjk1_-3ieVBcCIgYayOY9SpaSSLkzUfWTUNAYuv5yXEUOSfHniEcJwimB-1o/s640/tbl+tuico+7.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEizv64N2IieGrH7IuRC-haiuDLEDAYfc1nJTPxn8Qo4FsAEUTT77utgrEuFEoNac119bj2sbXGDMgWt0rzPpjk1_-3ieVBcCIgYayOY9SpaSSLkzUfWTUNAYuv5yXEUOSfHniEcJwimB-1o/s72-c/tbl+tuico+7.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2016/05/tbl-group-na-tuico-watiliana-sahihi.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/05/tbl-group-na-tuico-watiliana-sahihi.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy