TANZANIA KUIUZIA UMEME ZAMBIA - ASEMA WAZIRI MKUU MAJALIWA

  Wasanii wa Lusaka wakicheza ngoma ya asili ya Zambia katika mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika - ADB uliofany...


















 Wasanii wa Lusaka wakicheza ngoma ya asili ya Zambia katika mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika - ADB uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Mlungushi Zambia Mei 24, 2016. Tanzania iliwakilishwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
 Na Mwandishi Wetu

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania ina mpango wa kujenga njia ya umeme kutoka Mbeya hadi Zambia kupitia Tunduma ili kupunguza tatizo la umeme linaloikabili nchi hiyo.

“Serikali ya Tanzania inajenga njia ya umeme ya msongo wa KV 400 kutoka Iringa - Dodoma – Singida – Shinyanga ambayo ni sehemu ya mradi mkubwa wa umeme unaolenga kuunganisha Zambia, Tanzania na Kenya,” amesema.
Amesema  upembuzi yakinifu kwa ajili KV400 kutoka Iringa hadi Mbeya umekwishakamilika tangu mwaka 2012, na hivi sasa Serikali inatafuta fedha kwa ajili kuunganisha kipande cha kutoka Mbeya na gridi ya Taifa ya Zambia.
Waziri Mkuu ambaye anahudhuria mkutano huo kwa niaba ya Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli, ametoa ufafanuzi huo leo mchana (Jumanne, Mei 24, 2016) wakati akichangia hoja kwenye mjadala wa wakuu wa nchi na Serikali uliohusu Nishati na Mabadiliko ya TabiaNchi kwenye ukumbi wa mikutano cha kimataifa wa Mulungushi.

Amesema ili kukabiliana na changamoto ya nishati barani Afrika, nchi za bara hili zinahitaji kuwa na fedha ama mitaji, teknolojia ya kisasa na wataalamu wenye ujuzi wa kutosha jambo ambalo amesema ni gumu kulikamilisha kila nchi peke yake.

Amesema ili kukaribisha wawekezaji kwenye sekta ya umeme, Tanzania inafanyia marekebisho sheria zake ili kuruhusu uwekezaji kwenye sekta hiyo.

Akizungumzia kuhusu hali ya nishati Tanzania, Waziri Mkuu alisema Tanzania imebarikiwa kuwa na gesi asilia yenye ujazo wa futi trilioni 57.25 (tcf), makaa ya mawe yenye uhjazo wa tani bilioni 1.9 (asilimia 25 imevumbuliwa), umeme wa nguvu ya maji wa gigawati 4.7 ambazo ni asilimia 12 tu ndiyo inatumika. Pia alisema Tanzania ina deposits za urani yenye ujazo wa ratili milioni 200 (200 million pounds), joto la ardhini (geothermal) linaloweza kuzalisha umeme wa megawati zaidi ya 5,000. “Hivyo ni mbali na vyanzo vya umeme utokanao ua upepo na jua,” alisema.

Akizungumzia kuhusu usambazaji wa umeme vijijini, Waziri Mkuu alisema Tanzania kupitia REA imefanikiwa kusambaza umeme kwenye asilimia 52 ya vijiji vyote na inatarajia kufikia asilimia 90 ifikapo mwaka 2025.

Akishiriki mjadala huo, Makamu wa Rais wa Nigeria, Bw. Yemi Osinbajo alisema bara la Afrika linahitaji kuwa na vyanzo vikubwa vya umeme kama kweli linataka kufanikiwa kukamilisha kuwa na viwanda vya kutosha.
“Hatuwezi kuwaza kuwa na viwanda vingi wakati tukitegemea umeme wa nguvu ya jua peke yake… huu unahitaji uwekezaji mkubwa na eneo kubwa la kuweka mitambo,” alisema.
Naye Waziri Mkuu wa Msumbiji, Bw. Carlos Agostinho do Rosário
                                                                                                 
Akishiriki mjadala huo, Makamu wa Rais wa Nigeria, Bw. Yemi Osinbajo alisema bara la Afrika linahitaji kuwa na vyanzo vikubwa vya umeme kama kweli linataka kufanikiwa kukamilisha kuwa na viwanda vya kutosha.

“Hatuwezi kuwaza kuwa na viwanda vingi wakati tukitegemea umeme wa nguvu ya jua peke yake… huu unahitaji uwekezaji mkubwa na eneo kubwa la kuweka mitambo,” alisema.

Naye Waziri Mkuu wa Msumbiji, Bw. Carlos Agostinho do Rosário alisema masuala ya nishati yanahitaji uwekezaji mkubwa kwa hiyo akashauri makampuni kuungana kwenye uwekezaji na kuibua miradi ambayo ina tija (feasible and viable).

Waziri Mkuu amefuatana na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Asantu Kijaji, wachumi kadhaa pamoja na wataalamu wa sekta ya fedha.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, MEI 24, 2016.



  Wasanii wa Lusaka wakicheza ngoma ya asili ya Zambia katika mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika - ADB uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Mlungushi Zambia Mei 24, 2016. Tanzania iliwakilishwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Zambia, Edgar Lungu katika Mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika - ADB kwenye Kituo cha Mikutano cha Mlungushi kilichopo Lusaka Zambia , Mei 24, 2016.
 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu wa Msumbiji, Carlos Agostino do Rosario katika Mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika - ADB kwenye Kituo cha Mikutano cha Mlungushi kilichopo Lusaka Zambia , Mei 24, 2016.
 Rais wa Zambia, Edgar Lungu akifungua Mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika - ADB kwenye Kituo cha Mikutano cha Mlungushi kilichopo Lusaka Zambia , Mei 24, 2016. Kushoto kwake ni Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa ambaye alimwakilisha Rais John Magufuli kwenye mkutano huo, Rais wa ADB, Akinwumi Adesina (wa tatu kushoto), Rais wa Chad amabaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), IdrissaDeby Itno ((katikati), Rais wa Rwanda, Paul Kagame na viongozi wengine.
 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Mkutano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika - ADB kwenye Kituo cha Mikutano cha Mlungushi kilichopo Lusaka Zambia , Mei 24, 2016. Wengine pichani kutoka kushoto ni Makamu wa Rais wa Nigeria, Prof. Yemi Osinbojo, Rais wa Chad,  Idriss Debyo, Rais wa Zambia, Edgar Lungu na Waziri Mkuu wa Msumbiji,  Carlos Agostino do Rosario (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TANZANIA KUIUZIA UMEME ZAMBIA - ASEMA WAZIRI MKUU MAJALIWA
TANZANIA KUIUZIA UMEME ZAMBIA - ASEMA WAZIRI MKUU MAJALIWA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgN4S2HyuZFaUrGughl3gf6na_R9KdkQJiaQuRN-QN4d750WgISO3ZvmI6LfLkYPTaBY6qfLkNdjJ4xg5j1wL6Yh5EJxaI91NKi3YY5a3EMooIwx5PuhN1fpqkPl9wqTwgoPG8R1NI2GAA/s640/IMGS8954.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgN4S2HyuZFaUrGughl3gf6na_R9KdkQJiaQuRN-QN4d750WgISO3ZvmI6LfLkYPTaBY6qfLkNdjJ4xg5j1wL6Yh5EJxaI91NKi3YY5a3EMooIwx5PuhN1fpqkPl9wqTwgoPG8R1NI2GAA/s72-c/IMGS8954.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2016/05/tanzania-kuiuzia-umeme-zambia-asema.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/05/tanzania-kuiuzia-umeme-zambia-asema.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy