WAZIRI MBARAWA AWATAKA AIR TANZANIA KUANZA KUFANYA KAZI

Na Mwandishi Wetu. Serikali imezungumzia umuhimu wa kulifufua upya Shirika la Ndege nchini Air Tanzania (ATC) kwa kulinunulia n...











Na Mwandishi Wetu.
Serikali imezungumzia umuhimu wa kulifufua upya Shirika la Ndege nchini Air Tanzania (ATC) kwa kulinunulia ndege mpya na kulipa mtaji ili lifanye kazi kibiashara na kutengeneza faida kama ilivyokusudiwa awali.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na menejimenti na wafanyakazi wa Shirika hilo alipolitembelea jijini Dar es Salaam leo.
“Tutawekeza kwenye Air Tanzania ili kuongeza fursa za kiuchumi na kuvutia wasafiri wengi kufika nchini moja kwa moja na kuvutia sekta ya utalii”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Waziri Prof. Mbarawa amewataka wafanyakazi wa Shirika hilo ambao sio waadilifu na wavivu kuondoka mara moja ili kupisha wafanyakazi wabunifu na wenye mawazo ya kibiashara kuendesha shirika hilo kwa faida.
“Tunataka watu watakaolitoa shirika hili kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa kuliwezesha kiuchumi na kujitegemea ili kushindana na mashirika mengine ya ndege katika biashara“, amesisitiza Prof. Mbarawa.
Prof. Mbarawa amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Magufuli yuko tayari kununua ndege mpya ili kulifufua shirika hili hivyo amewataka wafanyakazi hao kuwa na mtazamo chanya wa kufanya biashara ili kuiletea taifa tija.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa ATC Bw. Johnson Mfinanga amemwambia Waziri Prof. Mbarawa kuwa kwa sasa shirika hilo lipo katika hali mbaya kiuchumi na hivyo kuhitaji nguvu ya Serikali kulikwamua ili litoe huduma inayoshahili.
Aidha, Waziri Prof. Mbarawa amesisitiza kuwa Serikali itaangalia upya taratibu za ajira katika shirika hilo na watakaobainika kuajiriwa kinyume cha taratibu watafukuzwa kazi mara moja.
“Tutanataka watu waadilifu, wabunifu na wenye sifa stahiki ili wafanye kazi kwa maslahi ya shirika na taifa kwa ujumla”, amefafanua Waziri Mbarawa.
Shirika la Ndege nchini ATC toka mwaka 2009 limekuwa likijiendesha kwa hasara na Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kulifufua shirika hilo ili lifanye kazi kwa faida na kuboresha usafiri wa anga ndani na nje ya nchi na hivyo kuvutia wasafiri wengi kuja nchini moja kwa moja.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAZIRI MBARAWA AWATAKA AIR TANZANIA KUANZA KUFANYA KAZI
WAZIRI MBARAWA AWATAKA AIR TANZANIA KUANZA KUFANYA KAZI
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2016/02/waziri-mbarawa-awataka-air-tanzania.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/02/waziri-mbarawa-awataka-air-tanzania.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy