Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Bahame Tom Nyanduga akiambatana na baadhi ya viongozi wa Tume hiyo am...
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Bahame Tom Nyanduga akiambatana na baadhi ya viongozi wa Tume hiyo ametembelea Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wake, Mhe. Jaji (Mstaafu), Damian Lubuva Februari 12 2016, kuhusu uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25, 2015.
Katika ziara hiyo, Mhe.
Nyanduga alipata fursa pia ya kumweleza Mhe. Lubuva kuhusu uangalizi uliofanywa
na Tume katika uchaguzi huo katika Mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Lindi na
Zanzibar.
Mwenyekiti wa THBUB, Mhe. Bahame Tom Nyanduga na Katibu Mtendaji wa Tume, Bi. Mary Massay wakimsikiliza kwa makini Mhe. Jaji (Mstaafu) Lubuva. |
Mhe. Jaji (Mstaafu) Lubuva
akimsikiliza Mhe. Nyanduga (hayupo pichani) wakati wa mazungumzo yao.
|
Mhe. Bahame Tom Nyanduga na Mhe. Jaji (Mstaafu), Damian Lubuva wakiwa katika picha ya pamoja na Kamishna wa Tume, Mhe. Dkt. Kelvin Mandopi na Bibi Mary Massay. |
Mhe. Bahame Tom Nyanduga na Mhe. Jaji (Mstaafu), Damian Lubuva wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa THBUB na baadhi ya maafisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. |
Mwenyekiti wa THBUB, Mhe. Bahame Tom Nyanduga akiagana na Mwenyeji wake, Mhe. Jaji (Mstaafu), Damian Lubuva (kushoto) mara baada ya kumaliza mazungumzo yao. |
Mwenyekiti wa THBUB, Mhe. Bahame Tom Nyanduga akiagana na Mwenyeji wake, Mhe. Jaji (Mstaafu), Damian Lubuva mara baada ya kumaliza mazungumzo yao. |
Mhe. Jaji (Mstaafu), Damian Lubuva akiagana na Katibu
Mtendaji wa THBUB, Bibi Mary Massay.
(Picha zote na Germanus Joseph wa THBUB).
COMMENTS