TIGO YADHAMINI ONESHO LA MWANAMUZIKI MOUSSA DIALLO KUTOKA NCHINI MALI LITANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM KESHO

Meneja wa Mawasiliano wa Kampuni ya Simu ya Tigo, John Wanyancha, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam ...








Meneja wa Mawasiliano wa Kampuni ya Simu ya Tigo, John Wanyancha, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo kuhusu kampuni hiyo kudhamini onesho la mwanamuziki Mousa Diallo kutoka nchini Mali litakalofanyika kesho katika Mgahawa wa Chakula na Vinywaji wa Samaki Samaki, Masaki jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Mkuu wa Masoko wa Mgahawa wa Samaki Samaki, Saum Wengert na Mwanamuziki, Moussa Diallo.
Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Simu ya Tigo, John Wanyanja (kushoto), akizungumza na Mwanamuziki, Moussa Diallo (kulia). Katikati ni Mmiliki wa Mgahawa wa Samaki Samaki, Carlos Bastos.

Mwanamuziki Moussa Diallo wa nchini Mali anayeishi Denmark (katikati), akiimba mbele ya waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akijitambulisha ambapo leo atafanya onesho lake Ukumbi wa Samaki Samaki, Masaki jijini Dar es Slaam. Kulia ni Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Simu ya Tigo, John Wanyanja ambao wamewezesha ujio wa mwanamuziki huyo na kushoto ni Ofisa  Mkuu wa Masoko wa Mgahawa wa Samaki Samaki, Saum Wengert.
Ofisa Mkuu wa Masoko wa Mgahawa wa Samaki Samaki, Saum Wengert, akizungumza katika mkutano huo kuhusu onesho hilo.

Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Warembo wa Samaki Samaki wakifuatilia matukio mbalimbali ya mkutano huo.


Na Dotto Mwaibale



MWANAMUZIKI maarufu toka Afrika Magharibi anayeishi Denmark, Moussa Diallo, leo anatarajia kufanya onesho lake hilo leo (Novemba 26) katika Mgahawa wa Chakula na Vinywaji wa  Samaki Samaki uliopopo Masaki jijijini Dar es Salaam ambapo litaenda sanjari na ziara ya kutembelea  miradi mbalimbali ya kijamii hapa nchini.


Onesho hilo lililodhaminiwa na Kampuni  ya simu za mikononi ya Tigo ikishirikiana na Mgahawa huo wa  Samaki Samaki litafanywa na Mwanamuziki huyo toka nchini Mali mwenye asili ya Denmark, ambaye amewasili nchini leo.


 Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi kwenye mkutano wa waandishi wa habari, Ofisa Mkuu wa Masoko wa Samaki Samaki, Saum Wengert, alisema mwanamuziki huyo anapiga muziki wa aina ya soul iliyochanganywa na vionjo vya kiafrika na muziki wa Magharibi unaopendwa ulimwenguni kote.


 Alisema onesho hilo pia linatarajiwa kufanyika kesho kutwa (Novemba 27) katika Hoteli ya Melia jijini Zanzibar na baadae watafanya Full Moon Party kwenye Hotel ya Kendwa Rocks iliyopo jijini Zanzibar. 


Moussa alizaliwa jijini Paris nchini Ufaransa na kukulia Bamako nchini Mali ambapo hivi sasa anamakazi yake Copenhagen nchini Denmark.


Katika juhudi za kukuza utamaduni, Diallo anachanganya muziki wake kwa kushirikisha vikundi mbalimbali vya utamaduni ikiwemo; Dawda Jobarten (Kora, Mwimbaji), Preben Carlsen (gitaa), Salieu Dibba (Percussions, Sauti), na Marco Diallo (Ngoma).


Kwa upande wake, Meneja uhusiano wa Tigo, John Wanyacha alisema kampuni hiyo na wadhamini wengine wamekubali Diallo kufanya onesho nchini ikiwa ni pamoja na kuweka mahusiano mazuri yaliyopo na maonesho yanayokuja.


Alisema kuwa wanafahamu wanachopenda wateja wao kwenye muziki na kwamba wana eneo ambalo linaweza kuwawezesha kuzuia miziki wasioyoipenda hivyo ujio wa Diallo nchini utaendeleza makubaliano mazuri kati ya kampuni hizo kwa kuwapa wateja wanachokihitaji ikiwa ni pamoja na vionjo. 




Wengine waliodhamini ziara hiyo ni pamoja ni; Johnnie Walker, French Kiss, Heineken na Ledger Plaza Bahari Beach.


(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)


COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TIGO YADHAMINI ONESHO LA MWANAMUZIKI MOUSSA DIALLO KUTOKA NCHINI MALI LITANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM KESHO
TIGO YADHAMINI ONESHO LA MWANAMUZIKI MOUSSA DIALLO KUTOKA NCHINI MALI LITANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM KESHO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEizny7kLnUR5hATkgZXe8GHSYZumNIcPLIG5aXkwBBbEU806jev9HCGz_shUf8_ZM5egBvotaIQqHR0pstMIubYsLJ3n1ETMTwGeEr7k0Be9izEzFAk2cXd_3osLtRvmetijLma7WHTYJOh/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEizny7kLnUR5hATkgZXe8GHSYZumNIcPLIG5aXkwBBbEU806jev9HCGz_shUf8_ZM5egBvotaIQqHR0pstMIubYsLJ3n1ETMTwGeEr7k0Be9izEzFAk2cXd_3osLtRvmetijLma7WHTYJOh/s72-c/1.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2015/11/tigo-yadhamini-onesho-la-mwanamuziki.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2015/11/tigo-yadhamini-onesho-la-mwanamuziki.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy