HATIMA YA MWILI WA MAWAZO KUAGWA AMA KUTOAGWA JIJINI MWANZA KUJULIKANA KESHO

Na:George Binagi-GB Pazzo wa Binagi Media Group Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza leo imeahirisha kesi ya madai ya kuomba ridhaa ya k...








Na:George Binagi-GB Pazzo wa Binagi Media Group
Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza leo imeahirisha kesi ya madai ya kuomba ridhaa ya kufanya ibada ya Mazishi ya aliekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mkoani Geita Marehemu Alphonce Mawazo iliyowasilishwa na Mchungaji Charles Lugiko ambae ni baba mlezi
wa marehemu Mawazo.




Katika kesi hiyo, mlalamikaji anaiomba mahakama kuondoa zuio la jeshi la polisi Mkoani Mwanza la kutoruhusu shughuli ya kuuaga mwili wa marehemu Mawazo kufanyika jijini Mwanza, kabla ya kwenda kuzikwa Mkoani Geita.

John Mallya ambae ni miongoni mwa Mawakili watatu wa Chadema ambao wanaitetea kesi hiyo, amebainisha kuwa Mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi kesho majira ya saa saba
mchana, ambapo Jaji wa Mahakama hiyo Mhe.Lameck Mlacha anatarajiwa kutoa maamuzi yake baada ya leo kusikiliza utetezi wa pande zote mbili zinazohusika.

Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema bara Salum Mwalimu, amewasihi wanafamilia pamoja na wafuasi wa chama hicho kuendelea kuwa watulivu, wakati maamuzi ya mahakama hiyo yakisubiriwa ambapo ameeleza kuridhika na mwenendo wa kesi hiyo.

Nje ya Mahakama, ulinzi ulikuwa umeimarishwa zaidi ambapo kulikuwa na polisi wa kutuliza ghasia waliokuwa na bunduki za risasi za moto, mabomu ya machozi pamoja na mbwa ambapo baada ya kesi hiyo kuahirishwa, umati mkubwa wa wananchi
uliokuwa umetanda mita chache kutoka Mahakamani hapo ulianza kuimba nyimbo za maombolezo na kuwasindikiza viongozi mbalimbali wa chedema hadi katika hoteli waliyofikia. 


BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA BINAGI RADIO-HABARI 
John Mallya ambae ni mmoja wa Mawakili wa Chadema akizungumza baada ya kesi kuahirishwa
Katibu Mkuu Msaidizi Chadema bara, Salum Mwalimu akizungumza baada ya kesi kuahirishwa
Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe akizungumza baada ya kesi kuahirishwa
Viongozi na makada wa Chadema wakiwa mahakamani
Viongozi na makada wa Chadema wakiwa mahakamani
Mawakili na Viongozi/Makada wa Chadema wakitoka Mahakamani
Wananchi na wafuasi wa Chadema wakitoka Mahakamani huku wakiimba nyimbo za maombolezo
Wananchi na wafuasi wa Chadema wakitoka Mahakamani huku wakiimba nyimbo za maombolezo.
Wananchi hawa waliwasindikiza viongozi wa chadema hadi hotelini.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: HATIMA YA MWILI WA MAWAZO KUAGWA AMA KUTOAGWA JIJINI MWANZA KUJULIKANA KESHO
HATIMA YA MWILI WA MAWAZO KUAGWA AMA KUTOAGWA JIJINI MWANZA KUJULIKANA KESHO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEicfG7-ylLgfqeF8ZmcqU0F8cVudqpIFWfTD6qiLi5bs_HVNEh_-nWl6DXYF8Tc_u5IA0phzgVkvfccyXL2QqEqfAPdVad2oMa8ra2r5rpAdSg5uugqdOi2Du1sqGr5iKxwlVTdk8Zup8SU/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEicfG7-ylLgfqeF8ZmcqU0F8cVudqpIFWfTD6qiLi5bs_HVNEh_-nWl6DXYF8Tc_u5IA0phzgVkvfccyXL2QqEqfAPdVad2oMa8ra2r5rpAdSg5uugqdOi2Du1sqGr5iKxwlVTdk8Zup8SU/s72-c/1.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2015/11/hatima-ya-mwili-wa-mawazo-kuagwa-ama.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2015/11/hatima-ya-mwili-wa-mawazo-kuagwa-ama.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy