Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Wilson Masilingi akiwa na Mchumi mwambata, Paul Mwafongo pamoja na Afi...
Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Wilson Masilingi akiwa na Mchumi mwambata, Paul Mwafongo pamoja na Afisa
Mawasiliano Wizara ya Fedha, Eva Valerian katika eneo la mikutano ya kimataifa ya Benki ya Dunia na
shirika la fedha la kimataifa nchini Peru- Lima.
Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt.
Servacius Likwelile (wa pili kutoka kulia) kwa nafasi ya uwaziri na
Ugavana wa Benki ya Dunia) akiwa kwenye picha ya pamoja ya Mawaziri wa
Fedha wa nchi 20 wanachama ( V20 - Vulnerable Twenty) watakao asirika
zaidi na mabadiliko ya tabia nchi (climate change).Mawaziri hao wanatoka
nchini Afghanistan, Bangladesh, Barbados, Bhutan, Costa Rica, Ethiopia,
Ghana, Kenya, Kiribati, Madagascar, Maldives, Nepal, Philippines,
Rwanda, Saint Lucia, Tanzania, Timor-Leste, Tuvalu, Vanuatu and Vietnam.
Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Servacius
Likwelile (aliyeweka kidole shavuni) akiwa pamoja na ujumbe wa Tanzania
kwa niaba ya Waziri wa Fedha wakiwa katika ufunguzi wa mkutano wa kundi
la nchi 20 zitakazo athirika zaidi na mabadiliko ya tabia nchi.
Ujumbe
wa Tanzania ukiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu
wa serikali, Dkt. Servacius Likwelile (wa pili kulia) akitoa ufafanuzi
kwenye majadiliano na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kanda ya Afrika
Bw. Makhtar Diop (kushoto) na Mkurugenzi wa Mipango na Uratibu Bi. Mamta
Murth (kushoto kwake). Kutoka (kulia) ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Wilson Masilingi na baada ya katibu Mkuu (kulia) kwake Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar, Khamis Mussa na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Natujwa Mwamba.
Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia kwa makini mafunzo ya namna ya kuzuia matumizi mabaya ya fedha.
Ujumbe
wa Tanzania ukiongozwa na Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Wizara ya
Fedha Dkt. Servacius Likwelile wakiwa katika semina ya mafunzo ya namna
ya kuzuia matumizi mabaya ya fedha.
Gavana
wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu akitoa ufafanuzi katika
majadiliano hayo pamoja na ujumbe wa Tanzania nchini Peru –Lima.
Baadhi
ya ujumbe wa Tanzania wakijadiliana yaliyojiri kwenye mikutano ya Benki
ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa inayoendelea nchini Peru.
Kutoka (kushoto) ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Wilson
Masilingi, Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Servacius
Likwelile, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Rished Bade,
Kamishna wa Fedha za nje Wizara ya Fedha Bw. Said Magonya na Mchumi
Mwambata wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Bw. Paul Mwafongo.
COMMENTS