RAIS KIKWETE AREJEA NYUMBANI BAADA YA ZIARA RASMI YA AUSTRALIA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Raymond Mushi katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius...







Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Raymond Mushi katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam usiku wa Jumamosi Agosti 1, 2015 mara baada ya kurejea kutoka Australia kwa mwaliko rasmi wa Kiserikali kutoka kwa Gavana Mkuu wa nchi hiyo Mh. Peter Cosgrove. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar, Saidi Meck Sadiki na viongozi wengine.

Rais Jakaya Kikwete akiongea na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Saidi Meck Sadiki baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam usiku wa Jumamosi Agosti 1, 2015  akitokea Australia alikozuru kwa mwaliko rasmi wa Kiserikali kutoka kwa Gavana Mkuu wa nchi hiyo, Mhe. Peter Cosgrove.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Paul Makonda na viongozi wengine waliofika kumpokea alipowasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam usiku wa Jumamosi Agosti 1, 2015  akitokea  Australia alikozuru kwa mwaliko rasmi wa Kiserikali kutoka kwa Gavana Mkuu wa nchi hiyo Mh. Peter Cosgrove.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Dar es Salaam Ndg. Ramadhani Madabida  alipowasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam usiku wa Jumamosi Agosti 1, 2015  akitokea Australia alikozuru kwa mwaliko rasmi wa Kiserikali kutoka kwa Gavana Mkuu wa nchi hiyo Mh. Peter Cosgrove. (PICHA NA IKULU)


Akiwa nchini Australia Rais Kikwete alikutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Australia, Bwana Tony Abbot ambaye alimpongeza kwa kuamua kukabidhi madaraka kwa kiongozi mwingine kwa mujibu wa  Katiba nchini Tanzania.

Rais Kikwete pia alikutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake  Gavana Mkuu wa Australia Mheshimiwa Peter Cosgrove, kabla ya kukutana na wawekezaji wakubwa wa Australia ambao tayari wanawekeza nchini Tanzania ambapo walizungumzia  namna ya kuendeleza sekta mpya ya gesi nchini na jinsi Tanzania inavyoweza kunufaika  kutokana na kupata gesi.

Tayari Serikali ya Australia na makampuni binafsi ya gesi na mafuta, yanaisaidia Tanzania hasa katika vyuo vya ufundi stadi VETA na  tafiti mbalimbali katika Kilimo.

Rais Kikwete alihitimisha ziara yake kwa kutunukiwa digrii ya udaktari wa heshima ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Newcastle, kwa mchango wake mkubwa alioutoa katika uongozi kwa kipindi cha miaka 10 aliyokaa madarakani nchini Tanzania na Dunia kwa ujumla.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: RAIS KIKWETE AREJEA NYUMBANI BAADA YA ZIARA RASMI YA AUSTRALIA
RAIS KIKWETE AREJEA NYUMBANI BAADA YA ZIARA RASMI YA AUSTRALIA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgX23tmmRCI_Pu5k3876oTCer3YjrOF8x14FwqfOT9GpTrOT5BBM4Ugcewn5wlbGBITcRi5NIxDospV2WYYAjdNBRO77287j7QhsyTEzjW5vvjopoR90AFMJZZLai4ugKpsvi7zbvk7XxH2/s640/a1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgX23tmmRCI_Pu5k3876oTCer3YjrOF8x14FwqfOT9GpTrOT5BBM4Ugcewn5wlbGBITcRi5NIxDospV2WYYAjdNBRO77287j7QhsyTEzjW5vvjopoR90AFMJZZLai4ugKpsvi7zbvk7XxH2/s72-c/a1.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2015/08/rais-kikwete-arejea-nyumbani-baada-ya.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2015/08/rais-kikwete-arejea-nyumbani-baada-ya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy