NCHI WAHISANI WATOA DOLA ZA MAREKANI MILIONI 802.15 KUKABILI MABADILIKO YA TABIA NCHI

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akimkaribisha ofisini kwake Mwakilishi wa ...






IMG_1116
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akimkaribisha ofisini kwake Mwakilishi wa mtandao wa FANPRAN, Sithembile Ndema kwa ajili ya kusaini kitabu cha wageni kabla ya kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano. (Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).

Na Mwandishi wetu
JUMLA ya dola za Marekani milioni 802.15 zimetolewa na nchi wahisani katika kusaidia mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi katika kipindi cha miaka miaka mine iliyopita.
Hayo yalielezwa na Mkurugenzi wa Kituo cha Mabadiliko ya tabia nchi Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Profesa Pius Yanda wakati alipokuwa akitoa mada kuhusu utafiti alioufanya yeye na wenzake kuhusu mchango wa uwezeshaji mapambano hayo kutoka nchi marafiki.
Alisema kiasi hicho cha fedha ni sawa na wastani wa dola milioni 200 kila mwaka zilizokuwa zikipelekwa katika sekta mbalimbali nchini.
Alisema utafiti walioufanya ambao ulilenga kuona kiasi cha fedha zilizotoka kwa wafadhili kwa ajili ya miradi mbalimbali ni awamu ya pili ya utafiti ambao awali ulijikita kuona bajeti ya taifa inavyotumika kukabili mabadiliko ya tabia nchi.
Profesa Yanda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere cha Mazingira amesema kwamba sehemu kubwa ya fedha ipo katika miradi ya maendeleo ambayo utekelezaji wake pamoja na kutosema kwamba unakabili mabadiliko ya tabia nchi, matokeo yake ndiyo yanayobainisha.
IMG_1128
Mkurugenzi wa Kituo cha Mabadiliko ya tabia nchi Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Profesa Pius Yanda (kushoto) akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (wa pili kushoto) huku wengine wakishuhudia zoezi hilo, Kulia ni Mwakilishi wa FANPRAN, Sithembile Ndema na wa pili kulia Mtafiti msaidizi kutoka ESRF, Ian Shanghvi.
Alitolea mfano kuwa miradi ya kusambaza umeme vijijini ( REA) nchini ambayo ilipata fedha nyingi katika miaka ya 2011 na 2012 ni miradi ya maendeleo lakini hatima yake ni kuzuia ukataji hovyo wa miti kwa ajili ya nishati.
Akifafanua fedha hizo zaidi alisema kwamba Tanzania mwaka 2010 jumuiya ya kimataifa zilitoa dola za Marekani milioni 171.93, mwaka 2011 dola za Marekani milioni 225.35, mwaka 2012 dola za Marekani milioni 229.74 na mwaka 2013 Tanzania ilipata dola za Marekani milioni 175.14.
Utafiti huo ambao uligharamiwa na COMESA, EAC na SADC umewasilishwa katika mkutano wa kitaifa wa uwezeshaji wa miradi ya kukabili tabia nchi kwa mfumo wa ndani ambapo pia Mwakilishi wa mtandao wa FANRPAN, Sithembile Ndema alikuwepo kuelezea maana ya mikutano ya kisera katika nchi zinazounda mtandao huo.
Mtandao huo ambao ulianzishwa mwaka 1994 baada ya mkutano wa mawaziri wa kilimo wa nchi za SADC, EAC na COMESSA na makao makuu yake kuwa nchini Zimbabwe ulianza kazi mwaka 1997 na sasa makao makuu yapo nchini Afrika Kusini.
Mtandao huo umelenga kuwezesha mataifa ya Afrika kuendesha kilimo na ufugaji unaozingatia mabadiliko ya tabia nchi na hivyo kutunza mazingira na kuongeza tija.
Mikutano ya aina hiyo pia inafanyika Uganda, Ethiopia, Kenya na Zambia.
Profesa Yanda alisema kwamba pamoja na fedha hizo kuonekana nyingi kiukweli ni haba kutokana na hali halisi ilivyo sasa na hasa ikizingatiwa kwamba kunatakiwa pia fedha za mabadiliko tabia nchi yenyewe badala ya kutumia miradi ya maendeleo ambao matokeo ni kukabili mabadiliko ya tabia nchi.
IMG_1149
Mshehereshaji Hanif Tuwa kutoka ESRF, akitoa mwongozo wa yatakayojiri kwenye mkutano wa kitaifa wa kujadili sera ya uwezeshaji kifedha mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika jana jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za ESRF.
Alisema takwimu walizopata kuhusu fedha zilizofika nchini kutoka katika jumuiya ya kimataifa zililingana na taarifa zilizopo Hazina na kuonesha kwamba fedha hizo zilienda kutumika katika makadirio yaliyokusudiwa.
“tofauti iliyopo ni tafsiri ya miradi ya mabadiliko ya tabianchi. Miradi ya maendeleo, inatamkwa kama miradi ya maendeleo lakini ukiangalia mwishoni ni miradi hiyo kusaidia katika kukabili mabadiliko ya tabia nchi” alisema katika mahojiano baadae na na waandishi wa habari.
Alisema kama Mkurugenzi wa Kituo cha mabadiliko ya tabia nchi anashauri serikali kuhimiza wananchi wake kuendelea kusimamia mazingira vyema huku wakulima na wafugaji wakisikiliza maofisa ugani kwa ajili ya kuwa na kilimo na ufugaji bora usioharibu mazingira..
Alisema tafiti mbalimbali zinaonesha kuwepo kwa athari kubwa ya mabadiliko ya tabia nchi ambapo sasa hata sehemu za baridi za nyanda za juu zimeanza kuwa na magonjwa ya Malaria huku wakulima wakiwa hawajui muda wa kupanda kutokana na mabadiliko ya joto na pia unyeshaji wa mvua.
Alisema pia nyanda za juu sasa zinakabiliwa na wadudu waharibifu wa mazao vitu ambavyo awali havikuwepo.
Alisema kwamba bado taifa linahitaji kufanya tafiti nyingi zaidi na kuzitumia kuelimisha umma kuhusu nini kinatokea na nini kinastahili kufanywa kukabili mabadiliko hayo.

IMG_1174
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akihutubia mkutano wa kitaifa wa kujadili sera ya uwezeshaji kifedha mabadiliko ya tabia nchi. Mkutano huo umefanyika jana jijini Dar es salaam katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za ESRF na kujadili taarifa ya utafiti uliofanywa kwa miaka minne kuhusiana na uwezeshaji.

Mkutano huo wa kitaifa ulifunguliwa na Mkurugenzi wa Taasisi huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) Dk. Tausi Kida ambaye alisema lengo la mkutano huo ni kuchambua utafiti uliofanywa na kuja na maazimio yatakayosaidia kuboresha kilimo na kuhifadhi mazingira katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.
Aliwaambia washiriki kuiangalia kwa makini tafiti ya Profesa Pius Yanda na kuhakikisha kwamba wanakuwa na uelewa wa maudhui na kuwezesha kutoa dira ya utekelezaji katika siku za usoni.
Alisema wakati taifa linajipanga kutekeleza mpango wake wa maendeleo wa kuelekea katika uchumi wa viwanda suala la mabadiliko tabia nchi haliwezi kuachwa na hivyo wajumbe wa mkutano walitakiwa kuangalia na kuja na mapendekezo yao.
Mapendekezo hayo ni pamoja na kuwa na kilimo na ufugaji wenye tija unazoingatia ufanisi katika hifadhi ya mazingira na namna uwezeshaji wa ndani unavyoweza kuendeleza mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.
Alisema ni muhimu kilimo kuwa ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
ESRF ni taasisi yinayojishughulisha na tafiti mbalimbali za jiuchumi na kijamii zinazotoa mwelekeo wa utekelezaji wa sera na kanuni mbalimbali za maendeleo na ustawi wa jamii.
Pmaoja na kuratibu mkutano huo pia ilitoa nafasi ya ukumbi wake kutumika na kutoa mwelekeo wa mkutano na umuhimu wake katika mpango wa pili wa maendeleo wa taifa ambao unatakiwa uzingatie mabadiliko ya tabia nchi.
IMG_1161
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akisoma hotuba na kuwakaribisha washiriki wa mkutano wa kitaifa wa kujadili sera ya uwezeshaji kifedha mabadiliko ya tabia nchi. Kulia ni Mwakilishi wa FANPRAN, Sithembile Ndema na kushoto ni Mkurugenzi wa Kituo cha Mabadiliko ya tabia nchi Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Profesa Pius Yanda.
IMG_1203
Mwakilishi wa FANPRAN, Sithembile Ndema akielezea mradi wa COMESA wa uwezashaji wa ndani wa fedha kwa ajili ya mabadiliko ya tabia nchi katika mkutano huo.
IMG_1249
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (katikati) na Mkurugenzi wa Kituo cha Mabadiliko ya tabia nchi Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Profesa Pius Yanda (kulia) wakifuatilia ka umakini 'presentation' ya Mwakilishi wa FANPRAN, Sithembile Ndema (hayupo pichani).
IMG_1318
Mkurugenzi wa Kituo cha Mabadiliko ya tabia nchi Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM), Prof. Pius Yanda, akitoa mada ya ufadhili wa kimataifa wa uwezeshaji wa kifedha wa mabadiliko ya tabianchi Tanzania katika mkutano huo.
IMG_1370
Pichani juu na chini washiriki wakichangia mawazo yao kuhusu namna sera ya uwezeshaji kifedha mabadiliko ya tabia nchi inavyopaswa kuwa katika mkutano huo.
IMG_1343
IMG_1150
Pichani juu na chini ni washiriki kutoka taasisi mbalimbali za serikali na zisizo za serikali, watafiti, na wadau wa maendeleo waliohudhuria mkutano wa kitaifa wa kujadili sera ya uwezeshaji kifedha mabadiliko ya tabia nchi.
IMG_1155
IMG_1231

IMG_1260
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano wa kitaifa wa kujadili sera ya uwezeshaji kifedha mabadiliko ya tabianchi.
IMG_1256
Picha ya pamoja ya washiriki.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: NCHI WAHISANI WATOA DOLA ZA MAREKANI MILIONI 802.15 KUKABILI MABADILIKO YA TABIA NCHI
NCHI WAHISANI WATOA DOLA ZA MAREKANI MILIONI 802.15 KUKABILI MABADILIKO YA TABIA NCHI
http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2015/08/IMG_1116.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2015/08/nchi-wahisani-watoa-dola-za-marekani.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2015/08/nchi-wahisani-watoa-dola-za-marekani.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy