MWILI WA MAREHEMU MZEE FRANCIS KITIME WASAFIRISHWA KWA MAZISHI

Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wa familia ya marehemu Mzee Francis Raphael Kitime wakiwa katika ibada ya kumuombea jana jij...










Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wa familia ya marehemu Mzee Francis Raphael Kitime wakiwa katika ibada ya kumuombea jana jijini Dar es Salaam. Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wa familia ya marehemu Mzee Francis Raphael Kitime wakiwa katika ibada ya kumuombea jana jijini Dar es Salaam. 

Padre wa Kanisa Katoliki Parokia ya Huruma ya Wagonjwa Muhimbili akizunguka kulibariki jeneza lenye mwili wa Marehemu Mzee Francis Raphael Kitime kwenye ibada ya kumuombea iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana kabla ya kusafirishwa kwenda Iringa kwa Mazishi. Padre wa Kanisa Katoliki Parokia ya Huruma ya Wagonjwa Muhimbili akinyunyizia maji ya baraka kwenye jeneza lenye mwili wa marehemu mzee Francis Raphael Kitime wakati wa ibada ya kumuombea iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana, kabla ya kusafirishwa kwenda Iringa kwa Mazishi.

Familia ya marehemu Mzee Francis Raphael Kitime (mbele) wakiwa kwenye ibada ya kumuombea marehemu. Familia ya marehemu Francis Raphael Kitime (mbele) wakiwa kwenye ibada ya kumuombea marehemu.

Mwanamuziki mkongwe na nguli nchini Tanzania, John Kitime ambaye ni mtoto wa marehemu Mzee Francis Raphael Kitime akitoa historia fupia ya marehemu baba yake mara baada ya ibada. Mwanamuziki mkongwe 'Nguli' nchini Tanzania, John Kitime ambaye ni mtoto wa marehemu Francis Raphael Kitime akitoa historia fupi ya baba yake mara baada ya ibada.

Familia ya marehemu Mzee Francis Raphael Kitime (mbele) wakiwa kwenye ibada ya kumuombea marehemu. Familia ya marehemu Francis Raphael Kitime (mbele) wakiwa kwenye ibada ya kumuombea marehemu.

Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wa familia ya marehemu Mzee Francis Raphael Kitime wakiwa katika ibada ya kumuombea jana jijini Dar es Salaam. Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wa familia ya marehemu Francis Raphael Kitime wakiwa katika ibada ya kumuombea jana jijini Dar es Salaam. 
Mmoja wa marafiki akitoa pole kwa, John Kitime (kulia) ambaye ni mtoto wa marehemu Mzee Francis Raphael Kitime wakati wa waombolezaji kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu. Mmoja wa marafiki akitoa pole kwa, John Kitime (kulia) ambaye ni mtoto wa marehemu Francis Raphael Kitime wakati waombolezaji wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu. Baba wa mwanamuziki mkongwe nchini, ndugu John Kitime aliyefariki Agosti Mosi, 2015 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam umesafirishwa kwenda nyumbani kwao mkoa wa Iringa kwa mazishi.

Marehemu Francis Raphael Kitime alisafirishwa jana baada ya kufanyika ibada ya kumuombea na kutoa heshima za mwisho kwa ndugu na jamaa wa familia ya marehemu waishio Dar es Salaam, ibada iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya huruma kwa wagonjwa lililopo viwanja vya hospitali ya hiyo.

Akisoma historia fupi ya marehemu, mtoto wa marehemu John Kitime alisema Francis Kitime alizaliwa Juni 16, 1931 Tosamaganga, Iringa katika familia ya watoto watatu yaani Joseph, Isabela na Clementina. Alipata elimu yake ya msingi hadi chuo kati ya mwaka 1939 hadi 1950 katika Shule za Misheni na Vyuo vya Elimu Tosamaganga, Iringa na mnamo mwaka 1951 hadi 1963 alifundisha katika shule anuai mkoani hapo.

Kitime alisema mwaka 1964 marehemu alianza kufanya biashara ya kuuza mafuta (Caltex) hadi 1970 ambapo alimiliki kituo hicho na kufanya biashara hiyo hadi mwaka 1979. Mwaka 1980 aliacha biashara na kuajiriwa kwenye idara ya utawala katika Hospitali ya Ipamba hadi alipostaafu.

Marehemu pia amefanya kazi za kitume takribani miaka 20 kama Mwenyekiti wa Baraza la Walei na Mwenyekiti wa Lions Club katika Mkoa wa Iringa na pia mtunzi na mwimbaji nyimbo mbalimbali hasa za lugha ya Ki-Hehe. Marehemu kaacha watoto sita, wajukuu nane na vitukuu wawili.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MWILI WA MAREHEMU MZEE FRANCIS KITIME WASAFIRISHWA KWA MAZISHI
MWILI WA MAREHEMU MZEE FRANCIS KITIME WASAFIRISHWA KWA MAZISHI
http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2015/08/IMG_0024.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2015/08/mwili-wa-marehemu-mzee-francis-kitime.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2015/08/mwili-wa-marehemu-mzee-francis-kitime.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy