DKT MAGUFULI AZIDI KUCHANJA MBUGA MKOANI NJOMBE

AWATAKA WANANCHI WAWEKE IMANI KUBWA KWAKE NA KUMPA KURA NYINGI ZA USHINDI.  Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kup...



AWATAKA WANANCHI WAWEKE IMANI KUBWA KWAKE NA KUMPA KURA NYINGI ZA USHINDI.




 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Njombe mjini katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa saba saba. Magufuli amesema akichaguliwa kuwa rais wa awamu ya tano ataendeleza juhudi zake za kujenga barabara kwa kiwango cha lami,amesema dhamira yake aliokuwa nayo ya Uwaziri wa Ujenzi katika kujenga barabara za lami katika maeneo yote hapa nchini.

Amesema tangu kupewa kuwa waziri wa ujenzi ameweza kujenga barabara  zaidi kilomita 7000 nchi nzima,ambapo ilipelekea kuongeza kuongeza pato la mfuko wa barabara kutoka bilioni 73,3 hadi kufikia bilini 866 kwa mwaka huu hivyo ameahidi akiwa rais atajenga zaidi barabara za lami.

Dkt Magufuli ambae anaendelea na mikutano ya kampeni za Urais mikoa ya nyanda za juu kusini , amelalamikia udanganyifu wa baadhi ya mitandao ya kijamii  na baadhi ya vyombo vya habari kuripoti  kuwa amelazwa wodi ya wagonjwa mahututi katika hospitali ya mkoa wa mbeya wakati sio kweli.

Aidha pia Magufuli  amewaomba wananchi waweke imani kubwa kwake kwa  kumpa kura nyingi  zitakazomwezesha kuwa raisi wa awamu ya tano,na kIsha alipe fadhira hizo kwa kutatua kero zinazowakabili hasa wananchi wenye kipato cha chini.

PICHA NA MICHUZI JR-NJOMBE
 Mgombea Urais wa CCM, Dkt John Pombe Magufuli akipeana mkono na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Ndugu Phillip Mangula mara baada ya kumkaribisha mgombea huyo jukwaani kuwahutubia wananchi wa njombe na kuzinadi sera za chama chake na kuomba ridhaa ya kuiongoza Tanzania katika kipindi cha awamu ya tano
 Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Ndugu Phillip Mangula akiwashukuru wananchi wa Njombe waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni,uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa sabasaba mjini humo,ambapo pia Ndugu Mangula alimkaribisha mgombea Urais wa CCM, Dkt John Pombe Magufuli kuwahutubia wananchi wa njombe na kuzinadi sera za chama chake na kuomba ridhaa ya kuiongoza Tanzania katika kipindi cha awamu ya tano
 Wananchi wa Njombe wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM, Dkt John Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa sabasaba mjini Njombe.
 Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM na Mgombea Ubunge wa jimbo la Kyela, Dkt. Harrison Mwakyembe akiwahutubia wananchi wa Njombe kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni
 Wananchi wakishangilia jambo kwenyemkutano wa kampeni wa CCM.

 Mgombea Urais wa CCM, Dkt John Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Wanging'ombe, Mhandisi Gerson Lwenge kwa wananchi wa Makoga ndani ya wilaya hiyo ya Wanging'ombe
 Mgombea Urais wa CCM, Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi Ilani ya CCM mgombea Ubunge wa jimbo la Wanging'ombe, Mhandisi  Gerson Lwenge kwa wananchi wa Makoga ndani ya wilaya hiyo ya Wanging'ombe kwa ajili ya kuwaambia wananchi ni namna gani wataiongoza Tanzania katika awamu ya tano. 
  Mgombea Urais wa CCM, Dkt John Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Makete, Dkt Norman Msigala kwa wananchi wa Makoga ndani ya wilaya hiyo ya Wanging'ombe
 Mkutano wa Kampeni ukiendelea. 
 Wananchi wakisikiliza sera za mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli,hayupo pichani alipowahutubia jioni ya leo mjini Njombe. 
 Wananchi wakiwa katika mkutano wa hadhara wa kampeni.
 Wananchi wakiwa na mabango yao ya kumsifu na kumkaribisha mgombea Urais wa CCM, Dkt. John Pombe Magufuli,mara baada ya kufunga barabara alipokuwa akipita katika kijiji cha Mgagala akielekea mkoani Njombe kwenye mkutano wa kampeni.
 Wananchi na Mabango yako
 Mgombea Urais wa CCM, Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Makoga katika wilaya ya Wanging'ombe.
 Wananchi  wa kijiji cha Ikonda wakimsikiliza, Dkt Magufuli 
Umati ukifuatilia mkutano huo.



COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: DKT MAGUFULI AZIDI KUCHANJA MBUGA MKOANI NJOMBE
DKT MAGUFULI AZIDI KUCHANJA MBUGA MKOANI NJOMBE
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh_BiH2Xl6yvqe-JJaxyY7JRXaYhdG8VsRdmFF0iVoYZI4-Iz6S5uAB0YOAhW3vhM4_HYIhZbh-X4fOSYpWA9PQZJcGAA66YxW_c-qjkxVJbhMA-770g94-1KbXrAsbB9KbLwGw3Pu_w9U/s640/3.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh_BiH2Xl6yvqe-JJaxyY7JRXaYhdG8VsRdmFF0iVoYZI4-Iz6S5uAB0YOAhW3vhM4_HYIhZbh-X4fOSYpWA9PQZJcGAA66YxW_c-qjkxVJbhMA-770g94-1KbXrAsbB9KbLwGw3Pu_w9U/s72-c/3.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2015/08/dkt-magufuli-azidi-kuchanja-mbuga.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2015/08/dkt-magufuli-azidi-kuchanja-mbuga.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy