WALIOMUUA ALBINO MWAKAJILA WA MBEYA LEO WAMEHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA

Hakimu Mwakalinga siku alipohukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa mauaji ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe. Leo amehu...





Hakimu Mwakalinga siku alipohukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa mauaji ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe. Leo amehukumiwa tena kunyongwa mpaka kufa katika mauaji ya mlemavu wa ngozi Henry Mwakajila.


Na Daniel Mbega
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Mbeya leo hii imewahukumu kunyongwa mpaka kufa watu wanne kati ya watano waliomuua Henry Mwakajila (17) ambaye ni mlemavu wa ngozi (albino).

Waliohukumiwa kunyongwa mpaka kufa ni Asangalwisye Kayuni maarufu kama Katiti au Mwakatoga na Gerard Korosso Kalonge (wakazi wa Kijiji cha Mbembati wilayani Ileje), na Leonard Msalage Mwakisole na Hakimu Mselem Mwakalinga (wakazi wa Kiwira wilayani Rungwe).

Mshtakiwa wa nne, Mawazo Philemon Figomole, ameachiliwa huru na mahakama hiyo baada ya ushahidi wa upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha pasi na shaka kwamba alihusika katika mauaji hayo.

Akisoma hukumu ya kesi hiyo ya mauaji yenye kumbukumbu Namb. KIW/IR/49/2008 na PI 5/2013, Jaji wa Mahakama Kuu Dk. Revila, amesema mahakama imejiridhisha pasi na shaka na ushahidi wa upande wa mashtaka kwamba washtakiwa hao wanne walitenda kosa hilo na hivyo wanastahili adhabu hiyo.

Hii ni kesi ya saba ya mauaji ya albino kutolewa hukumu ambapo mpaka sasa jumla ya watuhumiwa 15 wamehukumiwa kunyongwa mpaka kufa. Ililezwa mahakamani hapo kwamba, mnamo Februari 5, 2008 majira ya saa 12:00 na saa 1:00 jioni huko katika Kijiji cha Ilolo, Kata ya Kiwira, tarafa ya Ukukwe, wilayani Rungwe katika Mkoa wa Mbeya, washtakiwa hao walimteka nyara kijana Henry Mwakajila, ambaye ni mlemavu wa ngozi aliyekuwa akisoma kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Ukukwe na kisha kumuua.

Wakati wa mwenendo wa kesi, ilielezwa na mashahidi wa upande wa mashtaka kwamba mshtakiwa wa kwanza Asangalwisye Kayuni maarufu kama Katiti au Mwakatoga ambaye ni mganga wa jadi, mkazi wa Kijiji cha Mbembati, Wilaya ya Ileje, alikutwa na utumbo unaodhaniwa kuwa wa binadamu na ulipopelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ukathibitika kwamba ni utumbo wa marehemu Henry.

Mshtakiwa wa pili, Gerard Korosso Kalonge wa Kijiji cha Mbembati wilayani Ileje alikutwa na vidole vinne na mifupa kumi (10) vyote vinavyodhaniwa kuwa vya binadamu na baada ya uchunguzi wa Mkemia Mkuu wa Serikali ilibainika kwamba ni viungo vya marehemu Henry Mwakajila.
Ilielezwa pia kwamba, washtakiwa Leonard Msalage Mwakisole, Mawazo Philemon Figomole na Hakimu Mselem Mwakalinga ndio waliodaiwa kumteka nyara mtoto huyo na kumuua, kisha kupeleka viungo kwa mganga wa kienyeji Asangalwisye Kayuni.

Mshtakiwa wa tano, Hakimu Mselem Mwakalinga, tayari alikwishahukumiwa kunyongwa katika kesi nyingine ya mauaji ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, John Mwankenja, ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi nyumbani kwake. Hukumu ya kesi hiyo namba 131/2012 ilitolewa Novemba 13, 2013 ambapo inaelezwa kwamba watuhumiwa walitenda kosa hilo Mei 19, 2011 katika kijiji cha Mpandapanda, Kata ya Kiwira Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.

Ingawa watuhumiwa walikuwa wanne, lakini Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya chini ya Jaji Samwel Karua iliwahukumu kunyongwa mpaka kufa mshtakiwa wa kwanza Hakimu Mwakalinga na mshtakiwa wa pili Daudi Mwasipasa kwa maelezo kwamba walihusika moja kwa moja na mauaji hayo ya kukusudia.

Mshtakiwa namba tatu Obote Mwanyingili yeye alitiwa hatiani kutokana na kosa la kumhifadhi mtuhumiwa namba moja baada ya kutoka kufanya mauaji wakati mshtakiwa namba nne Kelvin Myovela alitiwa hatiani kutokana na kuhifadhi silaha iliyotumika katika mauaji hayo ingawa hakusika na kitendo hicho moja kwa moja, hivyo wote wawili walihukumiwa kifungo cha miaka saba jela.

Hata hivyo, Myovela tayari alikwishahukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kwa kukutwa na silaha kinyume cha sheria. 

Inadaiwa kwamba, chanzo cha mauaji hayo ya John Mwankenja, ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Rungwe, kilitokana na kiongozi huyo kufahamu kwamba hao ndio waliomuua mlemavu wa ngozi Henry Mwakajila, hivyo aliuawa ili kupoteza ushahidi.

Imeandaliwa na mtandao wa www.brotherdanny.com

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WALIOMUUA ALBINO MWAKAJILA WA MBEYA LEO WAMEHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA
WALIOMUUA ALBINO MWAKAJILA WA MBEYA LEO WAMEHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhdvLacVqtKIShlF9S_dqcxnHYyKaw8l7rCq7UmyNtSopAICEzJ28_yPfcwWCEHKIJH7iwKj_b2_jkcXZNIAGBKZnTCEdGhQn70XQzWk-oMJpzpzlEbHGXzRkk4mf_35r2XuN91OpDcXmnF/s640/Hakimu+Mwakalinga.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhdvLacVqtKIShlF9S_dqcxnHYyKaw8l7rCq7UmyNtSopAICEzJ28_yPfcwWCEHKIJH7iwKj_b2_jkcXZNIAGBKZnTCEdGhQn70XQzWk-oMJpzpzlEbHGXzRkk4mf_35r2XuN91OpDcXmnF/s72-c/Hakimu+Mwakalinga.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2015/07/waliomuua-albino-mwakajila-wa-mbeya-leo.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2015/07/waliomuua-albino-mwakajila-wa-mbeya-leo.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy