TANAPA YAANDAA SEMINA YA WAJIBU WA VYOMBO VYA HABARI KATIKA KUKUZA UTALII LEO JIJINI MWANZA

 Mkurugenzi wa Utalii na Masoko TANAPA, Ibrahim Mussa akifafanua jambo katika Warsha ya...

 Mkurugenzi wa Utalii na Masoko TANAPA, Ibrahim Mussa akifafanua jambo katika Warsha ya siku tatu ya Wahariri wa Habari na Wana habari kutoka vyombo mbalimbali, inayofanyika jijini Mwanza katika hotel ya Gold Crest. Kauli mbiu ya Mkutano wa mwaka huu ni  “Wajibu wa Vyombo vya Habari katika kukuza utalii”. Pamoja na kuelezea shughuli za TANAPA, ambapo mada zitakazowasilishwa zitahusu masuala ya Utalii, Uhifadhi na namna wanahabari wanavyoweza kushirikiana katika kuhimiza uhifadhi na kuendeleza utalii.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa,Ndugu Allan Kijazi akizungumza jambo,wakati wa ufunguzi wa Warsha ya Wahariri wa Habari Tanzania,mapema leo asubuhi jijini Mwanza.Ndugu Kijazi alisema kuwa Utalii ni sekta mtambuka na inachochea ukuaji wa sekta nyingine ikiwa ni pamoja na kilimo, usafirishaji wa anga na barabara, huduma za fedha, huduma za chakula na malazi kudorora kwa sekta nyinginezo.  "Hivyo kudorora kwa sekta hii huchangia kwa kiasi kikubwa kudorora kwa sekta nyingine.  Aidha, hadi sasa, Utalii unaongoza katika kuingiza fedha za kigeni ikiwa ya kwanza na kufuatiwa na sekta ya madini na kilimo.  

 Kwa  na kwa ujumla unachangia asilimia 17.5 ya Pato la Taifa lakini tathmini inaonyesha sekta hii inaweza ikachangia zaidi ya 30% ya pato la Taifa.  Asilimia zaidi ya 80 ya utalii nchini ni utalii wa kutembelea kwenye Hifadhi za Taifa, na hii inaonyesha kuwa hifadhi hizi ni muhimu kwa ustawi wa taifa letu.  Ni zaidi ya mara tatu ya idadi ya wanaotembelea Hifadhi hizi'',alisema Ndugu Kijazi.

Alisema kuwa  Maeneo yaliyo chini ya Hifadhi za Taifa yana faida nyingi za kiikolojia (ecosystem services) kama vile kuwa vyanzo vya maji (mfano; Hifadhi za Kilimanjaro, Arusha na Udzungwa). Maji hayo pia hutumiwa kwa ajili ya kuzalisha umeme unaotumika kwenye gridi ya Taifa. Hivyo faida za kusimamia Hifadhi hizi haziishii tu kwa watalii kufurahia bali pia kuna faida nyingine za kiuchumi ambazo sio rahisi sana kuziainisha katika mfumo wa kifedha (i.e. other values which are not easily tagged in financial terms).

Ndugu Kijazi alisema mwaka huu 2015, mtandao maarufu wa kimataifa unaojulikana kwa jina la “Safari Bookings” uliiteua Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kuwa “The best park for African safaris” na hii ni baada ya kushindanishwa na hifadhi nyingine 50 Barani Afrika zikiwemo za Afrika Kusini.Aidha, Hifadhi za Mikumi na Arusha zilitunukiwa “Certificate of Excellence” na mtandao maarufu duniani ujulikanao kama TripAdvisor.

Katika ufunguzi wa Warsha hiyo,Ndugu Kijazi alisema kuwa, Kauli mbiu ya Mkutano wa mwaka huu ni  “Wajibu wa Vyombo vya Habari katika kukuza utalii”. aliongeza kusema kuwa pamoja na kuelezea shughuli za TANAPA, mada zitakazowasilishwa zitahusu masuala ya Utalii na Uhifadhi na namna wanahabari wanavyoweza kushirikiana na TANAPA katika kuhimiza uhifadhi na kuendeleza utalii.  

"Mada kuu nne zitawasilishwa na viongozi wa TANAPA na wanazuoni maarufu akiwemo Nd. Jenerali Ulimwengu na Dkt. Alfred Kikoti. Inatarajiwa kuwa washiriki watapata fursa ya kuchangia na mwishoni watatushauri namna ya kuboresha utekelezaji wa majukumu yetu",alisema Kijazi.


 Baadhi ya Wahariri wa Habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika Warsha ya siku tatu ya Wahariri wa Habari kutoka vyombo mbalimbali,inayofanyika jijini Mwanza katika hotel ya Gold Crest. Kauli mbiu ya Mkutano wa mwaka huu ni  “Wajibu wa Vyombo vya Habari katika kukuza utalii”. Pamoja na kuelezea shughuli za TANAPA.
Meneja Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA),Pascal Shelutete akifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye semina hiyo mapema leo asubuhi jijini Mwanza
  Baadhi ya Wahari wa Habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika Warsha ya siku tatu ya Wahariri wa Habari kutoka vyombo mbalimbali,inayofanyika jijini Mwanza katika hotel ya Gold Crest. Kauli mbiu ya Mkutano wa mwaka huu ni  “Wajibu wa Vyombo vya Habari katika kukuza utalii”. Pamoja na kuelezea shughuli za TANAPA.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA),Ndugu Allan Kijazi pichani kati na Meneja Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchni (TANAPA),Pascal Shelutete akizungumza jambo na  Mkurugenzi wa Utalii na Masoko TANAPA,Bwa.Ibrahim Mussa katika Warsha ya siku tatu ya Wahariri wa Habari na Wana habari kutoka vyombo mbalimbali,inayofanyika jijini Mwanza katika hotel ya Gold Crest. Kauli mbiu ya Mkutano wa mwaka huu ni  “Wajibu wa Vyombo vya Habari katika kukuza utalii”.
Uongozi wa juu wa TANAPA wakiwa katika picha ya pamoja na Wahariri wa Habari kutoka vyombo mbalimbali.
Uongozi wa juu wa TANAPA wakiwa katika picha ya pamoja. (Imeandaliwa na Jiachie Blogs)

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TANAPA YAANDAA SEMINA YA WAJIBU WA VYOMBO VYA HABARI KATIKA KUKUZA UTALII LEO JIJINI MWANZA
TANAPA YAANDAA SEMINA YA WAJIBU WA VYOMBO VYA HABARI KATIKA KUKUZA UTALII LEO JIJINI MWANZA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhh_u14ndZOxlQaMID5gab1J1pk6nIkk9N5W8zr8vQV69X52VCtw5clSsHDkW7eZE3bWMRy2Ifw_pQrBmrDchBdAru8ESfd81WDzgsUUbmmepD4ER6LjlbqjqjJCl7987LJI-zA9EJPbMgA/s640/_MG_5006.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhh_u14ndZOxlQaMID5gab1J1pk6nIkk9N5W8zr8vQV69X52VCtw5clSsHDkW7eZE3bWMRy2Ifw_pQrBmrDchBdAru8ESfd81WDzgsUUbmmepD4ER6LjlbqjqjJCl7987LJI-zA9EJPbMgA/s72-c/_MG_5006.jpg
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2015/06/tanapa-yaandaa-semina-ya-wajibu-wa.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2015/06/tanapa-yaandaa-semina-ya-wajibu-wa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy