KONGAMANO LA JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA WANAWAKE TANZANIA (TANZANIA BUSINESS ENTREPRENEURS) LAFANYIKA JIJINI DAR

 Mwenyekiti wa Tanzania Business Entrepreneurs for Women,  Haika Lawere akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa Kongaman...




 Mwenyekiti wa Tanzania Business Entrepreneurs for Women,  Haika Lawere akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa Kongamano hilo lililofanyika Hoteli ya Mbezi Garden Dar es Salaam.
 
 Wadau wa kongamano hilo wakiwa wamejipanga kisawasawa. Kutoka Kulia ni Getrude Kilyabusebu, Haika Lawere, Hilda Mgaja na  Julieth Mjale.
 Mwezeshaji wa Kongamano hilo, James Mwang'amba 
akitoa mada.
 Muwezeshaji wa kongamano hilo, Chriss Rupia (kulia), akitoa maelezo juu ya namna ya kuanzisha Kampuni na hatua mbalimbali ambazo mtu anatakiwa azifuata wakati wa kufungua kampuni hasa binafsi.
 Mwenyekiti wa Tanzania Business Entrepreneurs for Women Haika Lawere (wa kwanza kulia) pamoja na wadau wengine wakiangalia bidhaa mbalimbali wakati wa kongamano hilo. 
 Mmoja wa majaji akiangalia bidhaa mbalimbali zilizopangwa kwenye meza zilizotokana na ubunifu wa wanawake waliohudhuria kongamano hilo.
Kongamano likiendelea
Baadhi ya wajasiriamali na wadau mbalimbali wakiwa katika Kongamano hilo.
Mmoja wa waratibu wa kongamano hilo Getrude Kilyabusebu (Kulia) akiweka sawa  kumbukumbu ya wadau waliofika katika kongamano hilo.
Bidhaa mbalimbali zikioneshwa.
Maonyesho ya bidhaa mbalimbali yakiendelea.

Baadhi ya wajasiriamali wakionesha kazi zao.
  Wadau mbalimbali wakitizama bidhaa mbalimbali katika Kongamano hilo.

Na Dotto Mwaibale

WAJASIRIAMALI wanawake nchini wametakiwa kuwa na moyo wa uthubutu ili kupiga hatua ya maisha na kiuchumi badala ya kuwa waoga.

Mwito huo umetolewa na Mratibu wa Kongamano la Jumuia ya Wafanyabiashara Wanawake Tanzania, Julieti Mjale wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kongamano hilo lililofanyika Hoteli ya Mbezi Garden Dar es Salaam jana.

"Uthubutu katika jambo lolote ni muhimu kwani unamfanya muhusika kupiga hatua ya maendeleo" alisema Mjale

Alisema wajasiriamali waliowengi wamekuwa na mipango mizuri ya kubuni biashara fulani lakini wanakuwa na hofu ya kupoteza fedha zao na hiyo inatokana na kushindwa kuthubutu au kuchukua maamuzi magumu ya kuanza kufanya biashara waliyoikusudia.

Akijitolea mfano yeye alisema alithubutu kwa kuanza kufanya biashara za chini lakini leo hii ana nyumba za kupangisha na kufikia hatua ya kufanya biashara za kwenda nje ya nchi na kuandaa makongamana ya namna hiyo kwa ajili ya kutoa elimu ya biashara.

Mwenyekiti wa Jumuia hiyo, Haika Lawere alisema lengo la kongamano hilo ni kuwakutanisha wajasiriamali wanawake ili kupeana uzoefu wa biashara na kujua changamoto walizonazo na kuzitafutia ufumbuzi pamoja na kupanua wigo wa shughuli zao na kutafuta masoko mapya ya bidhaa zao.

Katibu wa Jumuia hiyo, Hilda Ngaja, alisema changamoto kubwa waliyonayo wajasiriamali wanawake ni kutokuwa na uelewa mkubwa wa kufanyabiashara zao na kujikuta wakirudi nyuma kimaendeleo na ndio maana wamekuwa wakitumia fursa za semina na makongamano kwa ajili ya kuelimishana.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: KONGAMANO LA JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA WANAWAKE TANZANIA (TANZANIA BUSINESS ENTREPRENEURS) LAFANYIKA JIJINI DAR
KONGAMANO LA JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA WANAWAKE TANZANIA (TANZANIA BUSINESS ENTREPRENEURS) LAFANYIKA JIJINI DAR
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhkqRfksSXtiseBv0pj44df6NYLt3rIdat4_YJsCoaZmEo-U1pxSMBH8DtkcaVVUdkEEW4ERke_sLLxTxhJxT-rUX4MmKxbAdG0aGCXr2h_tXbJOtz395lQiMPcHZIKm2ZLa8hk839eCWI/s640/7.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhkqRfksSXtiseBv0pj44df6NYLt3rIdat4_YJsCoaZmEo-U1pxSMBH8DtkcaVVUdkEEW4ERke_sLLxTxhJxT-rUX4MmKxbAdG0aGCXr2h_tXbJOtz395lQiMPcHZIKm2ZLa8hk839eCWI/s72-c/7.JPG
Okandablogs
http://robertokanda.blogspot.com/2015/06/kongamano-la-jumuiya-ya-wafanyabiashara.html
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2015/06/kongamano-la-jumuiya-ya-wafanyabiashara.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy